-
Nunua Dhahabu Iliyosafishwa kwa MotoUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
2 Leo, ungeweza kuona magofu ya Laodikia karibu na Denizli, kilometa zapata 88 kusini-mashariki mwa Alasehiri. Katika karne ya kwanza, Laodikia lilikuwa jiji lenye ufanisi. Likikaa kwenye njia panda kuu, lilikuwa kitovu kikuu cha kazi ya benki na biashara. Uuzaji wa dawa ya macho yenye kujulikana sana uliongezea utajiri walo, na pia lilijulikana sana kwa sababu ya mavazi yalo ya hali ya juu sana yaliyotengenezewa huko kutokana na sufi nyeusi nzuri. Ukosefu wa maji uliokuwa tatizo kubwa kwa jiji hilo, ulikuwa umeshindwa kwa kuleta maji kupitia mifereji kutoka visima vyenye maji moto vilivyokuwa umbali fulani. Hivyo, maji yangekuwa yenye uvuguvugu tu kufikia wakati ambao yangewasili katika jiji hilo.
-
-
Nunua Dhahabu Iliyosafishwa kwa MotoUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
6. (a) Yesu anaelezaje hali ya kiroho ya kundi katika Laodikia? (b) Ni kielelezo gani kizuri cha Yesu ambacho kundi la Laodikia limeshindwa kufuata?
6 Yesu ana ujumbe gani kwa Walaodikia? Yeye hana neno la pongezi. Yeye anawaambia waziwazi hivi: “Mimi najua matendo yako, kwamba wewe si baridi wala moto. Mimi naona laiti ungekuwa baridi au sivyo moto. Kwa hiyo, kwa sababu wewe ni vuguvugu na wala si moto wala baridi, mimi nitatapika wewe utoke katika kinywa changu.” (Ufunuo 3:15, 16, NW) Wewe ungeitikiaje ujumbe kama huo kutoka kwa Bwana Yesu Kristo? Je! wewe hungeamka ujichunguze mwenyewe? Kwa hakika, Walaodikia hao wanahitaji kujiamsha wenyewe, kwa kuwa wamekuwa wavivu kiroho, kwa wazi wakichukua mambo mengi mno vivi hivi tu. (Linga 2 Wakorintho 6:1.) Yesu, ambaye wao wakiwa Wakristo iliwapasa kuiga, sikuzote anaonyesha bidii yenye kuwaka moto kwa ajili ya Yehova na utumishi wake. (Yohana 2:17) Zaidi ya hilo, wasikivu wamempata sikuzote akiwa mwanana na mpole, mwenye kuburudisha kama kikombe cha maji baridi katika siku yenye joto la kutosha jasho jingi. (Mathayo 11:28, 29) Lakini Wakristo katika Laodikia si moto wala baridi. Kama yale maji yanayotiririka kuingia jiji lao, wao wamevuvuwaa, wamekuwa vuguvugu. Wao wanaelekea kukataliwa kabisa na Yesu, ‘kutapikwa watoke katika kinywa chake’! Sisi kwa upande wetu na tujitahidi kwa bidii sikuzote, kuwaandalia wengine burudisho la kiroho, kama alivyofanya Yesu.—Mathayo 9:35-38.
-