Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
    • 2. Ni nani wanaotawala pamoja na Yesu?

      Yesu anatawala pamoja na wengine. “Watu kutoka katika kila kabila na lugha na watu na taifa . . . watatawala wakiwa wafalme juu ya dunia.” (Ufunuo 5:9, 10) Ni watu wangapi watakaotawala pamoja na Kristo? Tangu Yesu alipokuja duniani, mamilioni ya watu wamekuwa wafuasi wake. Lakini watu 144,000 ndio tu wanaoenda mbinguni kutawala pamoja na Yesu. (Soma Ufunuo 14:1-4.) Wakristo wengine wote walio duniani watakuwa raia wa Ufalme huo.​—Zaburi 37:29.

  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
    • 6. Watawala wa Ufalme wa Mungu wanaelewa hali yetu

      Kwa kuwa Mfalme wetu, Yesu, aliwahi kuwa mwanadamu, anaweza ‘kuusikitikia udhaifu wetu.’ (Waebrania 4:15) Wanaume na wanawake waaminifu 144,000 ambao watatawala pamoja na Yesu wamechaguliwa na Yehova “kutoka katika kila kabila na lugha na watu na taifa.”​—Ufunuo 5:9.

      • Je, unafarijika kujua kwamba Yesu na watawala wenzake wanaelewa hali za wanadamu? Kwa nini?

      Wanaume na wanawake watiwa mafuta kutoka malezi mbalimbali ambao waliishi katika vipindi tofauti.

      Yehova amewachagua wanaume na wanawake kutoka katika malezi mbalimbali watawale pamoja na Yesu

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki