Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 14. Ni farasi na mpandaji gani anayefuata kuonwa na Yohana, nayo njozi hii inatoa picha ya nini?

      14 Basi, mwito huu “Njoo!” unajibiwaje? Katika njia hii: “Na mwingine akatokea, farasi wa rangi-moto; na yule mmoja aliyeketi juu yake alipewa ruhusa ya kuondolea mbali amani kutoka dunia ili wao wapaswe kuchinja mmoja na mwenzake; na upanga mkubwa akapewa yeye.” (Ufunuo 6:4, NW) Ni njozi ya kutia hofu kweli kweli! Na hakuna shaka juu ya inachotolea picha: vita! Si vita ya uadilifu, yenye ushindi wa Mfalme wa Yehova mwenye kushinda bali ni vita yenye ukatili ya kimataifa, yenye kufanyizwa na binadamu, yenye umwagaji-damu na maumivu ya bure. Inafaa kama nini kwamba mpandaji huyu anampanda farasi wa rangi-nyekundu kama moto!

      15. Ni kwa nini haitupasi sisi tutake sehemu yoyote ya upandaji wa yule mwana-farasi wa pili?

      15 Kwa hakika, Yohana hangetaka sehemu yoyote ya mwana-farasi na upandaji wake wenye haraka isiyo na akili, kwa kuwa unabii ulitolewa kuhusu watu wa Mungu hivi: “Wala hawatajifunza vita tena kamwe.” (Isaya 2:4) Ingawa wangali “katika ulimwengu,” Yohana na, kwa upanuzi, ile jamii ya Yohana na umati mkubwa leo wao “si sehemu” ya huu mfumo wenye madoa ya damu. Silaha zetu ni za kiroho na “zinajaa nguvu kwa njia ya Mungu” kwa ajili ya kupiga mbiu ya ukweli kwa bidii, bila vita ya kimwili.—Yohana 17:11, 14; 2 Wakorintho 10:3, 4, NW.

      16. Ni lini na jinsi gani mpandaji-farasi mwekundu alipewa “upanga mkubwa”?

      16 Kulikuwa kumekuwa na vita vingi kabla ya 1914, ule mwaka Mpandaji-farasi mweupe alipopokea taji lake. Lakini sasa mpandaji-farasi mwekundu anapewa “upanga mkubwa.” Hiyo inadokeza nini? Kwa mlipuko wa Vita ya Ulimwengu 1, vita vya binadamu vimekuwa vyenye umwagaji-damu mwingi zaidi, vyenye uharibifu mwingi zaidi ya vilivyopata kuwa kabla ya hapo. Wakati wa mwosho-damu wa 1914-18, matanki, gesi zenye sumu, eropleni, sabmarini, mizinga mikubwa, na silaha za otomatiki zilitumiwa ama kwa mara ya kwanza ama kwa kadiri isiyotangulia kufanywa. Katika mataifa yapata 28, idadi ya watu wa nchi kwa ujumla, si wale tu ambao kazi yao ya maisha ni askari-jeshi, walisukumizwa kwenye jitihada za vita. Majeruhi walikuwa kadiri ya kuogopesha. Askari-jeshi zaidi ya milioni tisa walichinjwa, na majeruhi ya raia walikuwa wengi mno. Hata ilipokwisha vita, hakukuwa na kurudia amani halisi duniani. Zaidi ya miaka 50 baada ya vita, Konrad Adenauer waziri wa serikali Mjeremani alitoa elezo hili: “Usalama na utulivu vimetoweka katika maisha ya watu tangu 1914.” Kweli kweli yule mpandaji-farasi wa rangi-moto alipewa ruhusa aondolee mbali amani duniani!

      17. Utumizi wa huo “upanga mkubwa” umeendeleaje, kufuata Vita ya Ulimwengu 1?

      17 Halafu, kiu yake ya kutaka kuona damu ikimwagwa ikiwa imechochewa, yule mpandaji-farasi mwekundu alijitumbukiza ndani ya Vita ya Ulimwengu 2. Zana za uchinjaji zilizidi kuwa za kishetani zaidi, nayo majeruhi yakapanda juu kuwa mara nne ya yale ya Vita ya Ulimwengu 1. Katika 1945 bomu mbili za atomu zililipuka juu ya Japani, kila mojapo ilifutilia mbali—kwa dharuba moja—makumi ya maelfu ya majeruhi. Katika pindi ya vita ya pili ya ulimwengu, yule mpandaji-farasi mwekundu alivuna mavuno makubwa ya maisha zapata milioni 55, na hata wakati huo yeye hakutosheka. Imeripotiwa kwa njia yenye kuaminika kwamba nafsi zaidi ya milioni 20 zimeanguka chini ya ule “upanga mkubwa” tangu Vita ya Ulimwengu 2.

      18, 19. (a) Badala ya huo kuwa ushindi wenye shangwe wa tekinolojia ya kivita, lile chinjo tangu Vita ya Ulimwengu 2 ni uhakika wa ushuhuda gani? (b) Ni hatari gani inayokabili aina ya binadamu, lakini yule Mpandaji-farasi mweupe atafanya nini kuisawazisha?

      18 Je! sisi tungeweza kuita huu kuwa ushindi wenye shangwe wa tekinolojia ya kivita? Badala ya hivyo, huo ni ushuhuda wa kwamba yule farasi mwekundu asiye na rehema yuko katika mwendo. Na mwendo huo utaishia wapi? Baadhi ya wanasayansi wanasema kwamba kuna uwezekano wa vita ya nyukilia kutokea kiaksidenti—achia mbali mteketezo mkubwa wa kinyukilia uliopangwa! Lakini kwa furaha yule Mpandaji-farasi mweupe mwenye kushinda ana fikira tofauti juu ya jambo hili.

      19 Maadamu msingi wa jamii ya watu ni kiburi cha kitaifa na chuki, lazima aina ya binadamu iendelee kukalia kipipa cha hatari ya nyukilia. Hata kama mataifa yangekwangulia mbali silaha zayo za nyukilia kwa kutamauka, yangebaki na huo ujuzi. Kwa muda mfupi sana, wangeunda tena vidude vyao vya nyukilia vya uuaji-makusudi; kwa sababu hiyo, vita yoyote ikitumia silaha za kadiri ingevuvumuka upesi kama uyoga na kuwa maangamizi makubwa. Kile kiburi na chuki inayofunika mataifa leo lazima viongoze kwenye ujiuaji wa binadamu, isipokuwa—aha, ndiyo, isipokuwa yule Mpandaji-farasi mweupe ageuzie mbali mwendo wa kichaa wa yule mpandwaji wa rangi-moto. Acheni sisi tuwe na uhakika kwamba Kristo Mfalme atapanda, ili akamilishe ushindi wake juu ya ulimwengu wenye kudhibitiwa na Shetani na pia ili asimamishe jamii mpya ya kidunia ambayo msingi wayo ni upendo—upendo kwa Mungu na kwa jirani—kani kwa ajili ya amani, iliyo ya juu zaidi ya ile yenye kutikisika ya mazuio ya vita ya nyakati zetu zenye kichaa.—Zaburi 37:9-11; Marko 12:29-31; Ufunuo 21:1-5.

  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 94]

      “Alipewa Ruhusa Kuondolea Mbali Amani Kutoka Dunia”

      Tekinolojia inaongoza wapi? The Globe and Mail, Toronto, Kanada, Januari 22, 1987, iliripoti yafuatayo kutokana na hotuba ya Ivan L. Head, msimamizi wa International Development Research Centre:

      “Inakadiriwa kwa njia yenye kutegemeka kwamba mmoja wa kila wanasayansi na wanatekinolojia wanne katika ulimwengu wanaofanya utafiti na usitawishi anafanya kazi ya kuunda silaha. . . . Kwa makadirio ya 1986, gharama ni zaidi ya dola milioni 1.5 kwa dakika. . . . Je! sisi sote ni wenye usalama zaidi kama tokeo la mkazo wa aina hii ya tekinolojia? Silaha za nyukilia yalizo nazo yale mataifa yenye nguvu zaidi zina kani ya baruti ya zana zote za vita zilizotumiwa na wapiganaji wote katika Vita ya Ulimwengu 2 yote—mara 6,000. Vita ya Ulimwengu 2 elfu sita. Tangu 1945, kumekuwa na [muda] ulio punde ya majuma saba wakati ulimwengu umekuwa bila utendaji wa kivita. Kumekuwako zaidi ya vita 150 vya asilia ya kimataifa au vya raia wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vimekadiriwa kuwa vilidai maisha milioni 19.3, vingi vyavyo vikiwa ni tokeo la tekinolojia mpya zenye usahihi zaidi ambazo zimezuka katika wakati huu wa Umoja wa Mataifa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki