Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Januari 15
    • Farasi Mweusi

      Farasi mwingine wa masimulizi hayo anaelezwa na Yohana kwa maneno haya: “Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.”​—Ufunuo 6:5, 6.

      Je, wewe una njaa? Mamilioni wana njaa. Wanapatwa moja kwa moja na matokeo ya mpandaji wa farasi mweusi, anayefananisha njaa kubwa. Kila dakika watoto 30 wanakufa kwa ajili ya ukosefu wa chakula cha kutosha au dawa​—zaidi ya milioni 15 kwa mwaka! Mamia ya mamilioni ya watu wengine wanaishi katika hali za kusikitisha sana. Kulingana na aliyekuwa Mkuu wa Benki ya Ulimwengu Robert McNamara wana ‘vizuizi vingi vya kutokuwa na elimu ya kusoma, kukosa chakula kinachofaa, maradhi, hesabu kubwa ya vifo vya watoto na miaka michache ya maisha na hivyo kuwanyang’anya ule uwezekano wenyewe wa chembe za tabia wanazozaliwa nazo.’

      Katika miezi ya karibuni, limekuwa jambo la kawaida kuona picha za wanaume, wanawake, na watoto Waafrika wanaokufa njaa. Akieleza waziwazi mweneo wa taabu hiyo, Katibu-Mkuu wa U.M. Javier Perez de Cuellar, alionya hivi: “Wanadamu wengi zaidi huenda wakafa katika Afrika inayokaribia kuwa jangwa la Sahara zaidi ya kipindi chote cha Vita ya Ulimwengu ya Pili. Hata wale wanaopona huenda wakawa na kasoro maishani mwao mwote, ama ya kimwili au kiakili.” Watu hao wenye kupatwa na shida hiyo wanapatwa na matokeo ya moja kwa moja ya upandaji wa yule farasi mweusi.

      Huenda usiwe na njaa, lakini bila shaka umepatwa na matokeo ya picha zenye kusikitisha za watu waliokumbwa na njaa. Kulingana na makala ya mhariri ya New York Times la Mei 20, 1985, dola zaidi ya bilioni moja kufikia wakati huo zilikuwa zimechangwa ili kuwapa msaada wenye njaa. lngawa huenda ikawa hukuchanga moja kwa moja, serikali fulani zimetoa michango mikubwa, zikitumia pesa za kodi. Ndiyo, upandaji wa farasi mweusi una matokeo ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja juu ya watu wote.

  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Januari 15
    • FARASI MWEUSIL: Mpandaji farasi huyo anafananisha upungufu wa chakula na njaa kubwa. Ingawa mamilioni wanakufa njaa, wengine wangali wanaweza kununua chakula cha anasa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki