-
Biblia Inasema Nini Kuhusu Magonjwa ya Mlipuko?Maswali ya Biblia Yajibiwa
-
-
Je, Biblia ilitabiri kuhusu magonjwa ya mlipuko?
Biblia haitabiri magonjwa hususa ya mlipuko, kama vile ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19), UKIMWI, au homa ya Hispania. Lakini inatabiri kuhusu “magonjwa” (au “tauni,” UV) na “ugonjwa hatari.” (Luka 21:11; Ufunuo 6:8) Matukio hayo ni sehemu ya ishara ya “siku za mwisho,” inayorejelewa pia kuwa “umalizio wa mfumo wa mambo.”—2 Timotheo 3:1; Mathayo 24:3.
-
-
Biblia Inasema Nini Kuhusu Magonjwa ya Mlipuko?Maswali ya Biblia Yajibiwa
-
-
Ufunuo 6:8: “Tazama! farasi wa rangi ya kijivu, na yule aliyeketi juu yake alikuwa na jina Kifo. Na Kaburi lilikuwa likimfuata kwa ukaribu. Nao wakapewa mamlaka . . . ili kuua kwa . . . ugonjwa hatari.”
Maana: Unabii kuhusu wapanda-farasi wanne wa Ufunuo unaonyesha kwamba magonjwa ya mlipuko yangetokea katika siku zetu.
-