Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wanadamu Wataiharibu Dunia Kabisa?
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Septemba 1
    • Je, Wanadamu Wataiharibu Dunia Kabisa?

      “Kizazi kinaenda, kizazi kinakuja; lakini dunia inasimama mpaka wakati usio na kipimo.”—MFALME SULEMANI, KARNE YA 11 K.W.K.a

      Mwandikaji huyo wa Biblia, alitambua tofauti kubwa kati ya maisha mafupi ya wanadamu na umilele wa dunia. Kwa kweli, kwa maelfu ya miaka, vizazi vimekuja na kwenda, na bado Dunia imedumu na kuendelea kutegemeza uhai—hadi leo.

      Watu wameita miaka ya tangu Vita vya Pili vya Ulimwengu kuwa Kipindi cha Maendeleo Makubwa. Katika kipindi cha miaka 70 hivi baada ya vita hivyo, wanadamu wamefanya maendeleo makubwa katika usafiri, mawasiliano, na teknolojia, ambayo yameleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi. Watu wengi wanaishi maisha ambayo zamani hayakuwaziwa. Wakati huohuo, idadi ya watu duniani imeongezeka karibu mara tatu.

      Ingawa hivyo, maendeleo hayo yametokeza uharibifu. Inasemekana kwamba shughuli za wanadamu zinavuruga mifumo ya asili ya dunia. Kwa kweli, baadhi ya wanasayansi wanasema kwamba tumefikia kipindi ambacho wanadamu wanaharibu dunia kwa kiwango kikubwa sana.

      Biblia ilitabiri kipindi ambacho wanadamu ‘wangeiharibu dunia.’ (Ufunuo 11:18) Watu wengine wanajiuliza ikiwa tunaishi katika kipindi hicho. Je, dunia itazidi kuharibiwa? Je, inawezekana kuzuia uharibifu huo? Je, wanadamu wataiharibu dunia kabisa?

      JE, INAWEZEKANA KUZUIA UHARIBIFU?

      Je, dunia inaelekea kuharibiwa kabisa? Wanasayansi fulani wanafikiri ni vigumu kutabiri madhara ya uharibifu wa dunia. Kwa hiyo, wanahofu kwamba huenda tukafikia kipindi ambacho mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yataleta uharibifu mkubwa.

      Dububarafu akiwa juu ya kilima cha barafu

      Kwa mfano, fikiria kuhusu barafu kwenye eneo la magharibi ya Antaktika. Baadhi ya wataalamu wanasema kwamba kuna wakati ambapo haitawezekana kuzuia kuyeyuka kwa barafu katika eneo hilo. Hii ni kwa sababu barafu hiyo husaidia kuakisi miale ya jua. Lakini kadiri barafu inavyozidi kupungua, ndivyo bahari iliyo chini ya barafu ambayo haina uwezo mkubwa wa kuakisi inavyozidi kuonekana. Bahari hufyonza joto na kufanya barafu izidi kuyeyuka. Huenda hali hii ikashindwa kuzuilika. Kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari kwa sababu ya kuyeyuka kwa barafu kunaweza kuleta maafa kwa watu wengi sana.

  • Je, Wanadamu Wataiharibu Dunia Kabisa?
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Septemba 1
    • Wanadamu Wameiharibu Dunia

      • Angahewa. “Kuna uthibitisho ulio wazi wa ongezeko la joto katika angahewa la Dunia, bahari, na nchi kavu . . . Chanzo kikuu cha ongezeko hilo tangu miaka ya 1950 ni shughuli za wanadamu.”—Shirika la Hali ya Hewa la Marekani, 2012.

      • Ardhi. “Karibu asilimia 50 ya ardhi imeharibiwa moja kwa moja na binadamu na kusababisha athari kubwa kwa viumbe hai, mzunguko wa virutubisho kati ya mimea na udongo, . . . na hali ya hewa.”—Kitabu Global Change and the Earth System.

      • Bahari. “Asilimia 85 hivi ya maeneo ya uvuvi duniani yamevuliwa kupita kiasi, hayana samaki wa kutosha, yametumiwa sana, au yanalindwa ili samaki wazaane.”—Shirika la BBC, Septemba 2012.

      • Viumbe hai. “Wanasayansi wengi wanasema . . . wanadamu ndio kisababishi kikuu cha maangamizi makubwa ya viumbe hai Duniani, yanayohofiwa kutokea siku zijazo.”—Kulingana na science.nationalgeographic.com.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki