Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je! Wewe Utatii Onyo la Mungu?
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Machi 1
    • Katika miaka ya hivi majuzi mengi yamesemwa juu ya kisababishi kingine tena cha msononeko: Kuharibu mazingira kwa mwanadamu. Ingawa Yesu hakutaja hilo kimahususi katika unabii wake, Ufunuo 11:18 huonyesha kwamba kabla ya uharibifu kuja, mwanadamu angekuwa ‘akiiharibu dunia.’ Uthibitisho wa kwamba uharibifu huo unatukia ni mwingi. Akinukuliwa katika kitabu State of the World 1988, mshauri wa kimazingira Norman Myers atoa ujumbe huu wenye kuhofisha: “Hakuna kizazi kingine katika wakati uliopita ambacho kimekabili taraja la utokomeo mkubwa kikiwa kingali hai. Hakuna kizazi katika wakati ujao kitakachokabili ugumu uo huo: kizazi kilichopo kikishindwa kushughulikia tatizo hilo, uharibifu utakuwa tayari umefanywa na hakutakuwa ‘fursa ya pili.’”

      Fikiria ile ripoti katika toleo la gazeti Newsweek la Februari 17, 1992 juu ya upungufu wa ozoni katika angahewa. Mstadi wa ozoni wa shirika la Greenpeace Alexandra Allen alinukuliwa akionya kwamba upungufu wa ozoni “umefikia sasa kuwa tisho kwa wakati ujao wa uhai wote duniani.”—Ona Sanduku kwenye ukurasa huu ili kupata uthibitisho zaidi wa kuharibiwa kwa dunia kimazingira.

  • Je! Wewe Utatii Onyo la Mungu?
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Machi 1
    • [Sanduku katika ukurasa wa 6]

      Matatizo ya Kimazingira—Ishara ya Nyakati

      ◻ Ngao ya ozoni yenye kukinga katika latitudo za Kizio cha Kaskazini zenye wakaaji wengi inapungua kwa mwendo wa mara mbili zaidi ya vile wanasayansi walivyofikiri miaka michache tu iliyopita.

      ◻ Kiasi cha chini zaidi cha jamii ya wanyama na mimea 140 yanatokomea kila siku.

      ◻ Viwango vya kaboni dayoksaidi yenye kunasa joto katika angahewa sasa ni asilimia 26 juu zaidi ya kabla ya mweneo wa usitawi wa viwanda, navyo vyaendelea kupanda.

      ◻ Uso wa dunia ulikuwa wenye ujoto zaidi katika 1990 kuliko katika mwaka mwingine wowote tangu rekodi ilipoanza kuwekwa katikati ya karne ya 19; sita kati ya ile miaka saba yenye ujoto zaidi ambayo imepata kurekodiwa imetukia tangu 1980.

      ◻ Misitu inatokomea kwa kadiri ya hektari milioni 17 kwa mwaka, eneo lililo karibu nusu ukubwa wa Finland.

      ◻ Idadi ya wakaaji wa ulimwengu inakua kwa kadiri ya watu milioni 92 kwa mwaka—karibu sawa na kuongeza watu wengi kadiri ya idadi ya wakaaji wa Meksiko kila mwaka; kati ya jumla hiyo, milioni 88 wanaongezwa katika nchi zinazositawi.

      ◻ Watu bilioni 1.2 hivi hukosa maji safi ya kunywa.

      Kulingana na kitabu State of the World 1992, cha Worldwatch Institute, kurasa 3, 4, W. W. Norton & Company, New York, London.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki