-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
7. Ni ishara gani nyingine ambayo Yohana aona katika mbingu?
7 Baada ya hapo Yohana aona nini? “Na ishara nyingine ikaonekana katika mbingu, na, tazama! drakoni mkubwa wa rangi-moto, mwenye vichwa saba na pembe kumi na juu ya vichwa vyake mataji saba; na mkia wake huburuta theluthi ya nyota za mbingu, na ukazivurumisha chini kwenye dunia. Na drakoni akafuliza kusimama mbele ya mwanamke ambaye alikuwa karibu kuzaa, kwamba, wakati ambapo yeye angezaa, apate kumeza mtoto wake.”—Ufunuo 12:3, 4, NW.
-
-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
9. Ni nini kinachoonyeshwa na uhakika wa kwamba mkia wa huyo drakoni “huburuta theluthi ya nyota za mbingu” kuziangusha chini kwenye dunia?
9 Pia drakoni ana mamlaka katika milki ya kiroho. Kwa mkia wake, yeye “huburuta theluthi ya nyota za mbingu.” Nyota zaweza kuwakilisha malaika. (Ayubu 38:7) Mtajo “theluthi” ungekazia kwamba idadi kubwa sana ya malaika wameongozwa vibaya na Shetani. Mara hawa walipokuja chini ya udhibiti wake, hawakuwa na njia ya kuponyoka. Hawangeweza kurudi kwenye tengenezo takatifu la Mungu. Wakaja kuwa roho waovu, wakawa kana kwamba wameburutwa na Shetani, mfalme, au mtawala wao. (Mathayo 12:24) Shetani pia aliwatupa duniani. Hii bila shaka inarejezea siku ya Noa kabla ya Furiko, wakati Shetani alipowashawishi hawa wana waasi wa Mungu waende chini duniani wakaishi pamoja na binti za wanadamu. Ikiwa adhabu, hawa “malaika ambao walifanya dhambi” wametupwa na Mungu katika hali iliyo kama gereza inayoitwa Tartaro.—Mwanzo 6:4; 2 Petro 2:4; Yuda 6, NW.
10. Ni matengenezo gani yenye kupingana yanayoonekana, na ni kwa nini drakoni hutafuta kumeza mtoto wakati mwanamke anapozaa?
10 Hivyo, matengenezo mawili yenye kupingana yamekuja kuonekana waziwazi—tengenezo la Yehova la kimbingu kama linavyotolewa picha na mwanamke na tengenezo la Shetani la roho waovu ambalo hupinga enzi kuu ya Mungu. Lile suala kubwa la enzi kuu lazima limalizwe. Jinsi gani? Shetani, akiwa angali anaburuta roho waovu pamoja naye, ni kama hayawani mkali wa mawindo mwenye kutupia jicho windo liwezekanalo. Yeye anangojea mwanamke azae. Yeye anataka kumeza hiki kitoto kichanga kinachotarajiwa kwa sababu yeye anajua kwamba kinatokeza tisho baya sana katika kuendelea kuwako kwake na kule kwa ulimwengu ambao juu yao yeye anatumia utawala.—Yohana 14:30.
-