Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 11. Yohana anaelezaje habari za uzawa wa huyo mtoto wa mwanamke, na ni kwa nini mtoto huitwa “mwana, wa kiume”?

      11 Wakati uliowekewa mataifa kutawala bila kukatizwa na Mungu ulikuja kwenye kikomo katika 1914. (Luka 21:24) Ndipo, kwa wakati barabara, mwanamke anajifungua mtoto wake: “Na yeye akazaa mwana, wa kiume, ambaye anapaswa kuchunga mataifa yote kwa ufito wa chuma. Na mtoto wake akadakwa mbali hadi kwa Mungu na kwenye kiti cha ufalme chake. Na yule mwanamke akakimbia kwenda katika jangwa, ambako yeye ana mahali palipotayarishwa na Mungu, ili wao wapaswe kulisha yeye huko siku elfu moja mia mbili na sitini.” (Ufunuo 12:5, 6, NW) Mtoto ni “mwana, wa kiume.” Ni kwa nini Yohana anatumia usemi huu wa maradufu? Yeye anafanya hivyo kuonyesha kufaa kwa mtoto, uwezo wake wa kutawala mataifa kwa uweza wa kutosha. Unakazia pia jinsi uzawa huu ulivyo pindi ya tukio lenye maana sana, la shangwe! Una daraka la maana sana katika kuleta siri takatifu ya Mungu kwenye tamati. Kwani, mtoto huyu wa kiume hata ‘atachunga mataifa yote kwa ufito wa chuma’!

  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 13. Ni nini kinachofananishwa na huyo mtoto wa kiume ‘kudakwa mbali hadi kwa Mungu na kwenye kiti cha ufalme chake’?

      13 Yehova hangeweza kamwe kuruhusu Shetani ameze mke Wake au mwana Wake aliyezaliwa hivi sasa! Wakati wa uzawa, mtoto huyo wa kiume ‘anadakwa mbali kwa Mungu na hadi kwenye kiti cha ufalme chake.’ Yeye anakuja hivyo chini ya himaya ya Yehova, ambaye ataangalia kikamili huu Ufalme uliozaliwa hivi sasa, chombo Chake cha kutakasia jina Lake takatifu. Wakati ule ule, huyo mwanamke anakimbilia mahali alipotayarishiwa na Mungu jangwani. Tutapata habari zaidi juu ya hilo baadaye! Kwa habari ya Shetani, sasa jukwaa limetayarishwa kwa ajili ya tukio lenye maana kubwa ambalo litafanya isiwezekane kabisa kwake kutisha tena hata kidogo Ufalme ulio katika mbingu. Ni tukio gani hilo?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki