-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
13. Ni mwono gani wenye kushangaza anaoona Yohana wakati malaika anapompeleka katika jangwa kwa nguvu ya roho?
13 Unabii hufumbua nini zaidi kwa habari ya kahaba mkubwa na msiba wake? Kama Yohana anavyosimulia sasa, mandhari nyingine iliyo wazi sana yaonekana: “Na yeye [malaika] akapeleka mimi mbali kwa nguvu ya roho kuingia ndani ya jangwa. Na mimi nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ambaye alikuwa amejaa majina ya kufuru na ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”—Ufunuo 17:3, NW.
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
15. Ziko tofauti gani kati ya hayawani-mwitu wa Ufunuo 13:1 na yule wa Ufunuo 17:3?
15 Hayawani-mwitu huyu ana vichwa saba na pembe kumi. Basi, je! yeye ni hayawani-mwitu yule yule ambaye Yohana aliona mapema zaidi, ambaye pia alikuwa na vichwa saba na pembe kumi? (Ufunuo 13:1) La, ziko tofauti. Hayawani-mwitu huyu ni rangi-nyekundu-nyangavu na, tofauti na hayawani-mwitu aliyetangulia, hasemwi kuwa ana mataji. Badala ya yeye kuwa na majina ya kufuru juu ya vichwa vyake saba tu, yeye ‘anajaa majina ya kufuru.’ Hata hivyo, lazima pawe na uhusiano kati ya hayawani-mwitu mpya na yule aliyetangulia; mifanano kati yao ni mingi mno kuwa ya nasibu.
16. Ni nini utambulisho wa huyo hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na imetaarifiwa nini kwa habari ya kusudi lake?
16 Basi, hayawani-mwitu mpya rangi-nyekundu-nyangavu ni nini? Yeye ni lazima awe ule mfano wa hayawani-mwitu ambao ulitokezwa kwa himizo la hayawani-mwitu Uingereza-Amerika aliyekuwa na pembe mbili mithili ya mwana-kondoo. Baada ya mfano huo kuwa umefanywa, huyo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili aliruhusiwa kuupa pumzi huo mfano wa hayawani-mwitu. (Ufunuo 13:14, 15) Yohana anaona sasa mfano ulio hai, unaopumua. Ni picha ya tengenezo la Ushirika wa Mataifa ambalo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alileta kwenye uhai katika 1920. Rais Wilson wa U.S. alikuwa na njozi ya kwamba Ushirika huo “ungekuwa baraza la kutolea watu wote haki na kufutilia mbali milele tisho la vita.” Lilipofufuliwa baada ya vita ya ulimwengu ya pili likiwa Umoja wa Mataifa, kusudi la katiba yalo lilikuwa “kudumisha amani na usalama wa kimataifa.”
-