Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 27. (a) Kunatukia nini wakati malaika mwenye mundu anapokusanya “mzabibu wa dunia”? (b) Ni unabii gani katika Maandiko ya Kiebrania unaoonyesha kadiri ya vuno hilo?

      27 Lazima hukumu itekelezwe! “Na malaika akatia mundu wake ndani ya dunia na kukusanya mzabibu wa dunia, na yeye akavurumisha huo ndani ya shinikizo la divai kubwa la kasirani ya Mungu. Na shinikizo la divai likakanyagwa nje ya jiji, na damu ikaja nje ya shinikizo la divai mpaka juu kabisa kwenye hatamu za wale farasi, kwa kitalifa cha farlong’i elfu moja mia sita.” (Ufunuo 14:19, 20, NW) Ghadhabu ya Yehova dhidi ya mzabibu huu imetangazwa kwa muda mrefu uliopita. (Sefania 3:8) Unabii katika kitabu cha Isaya hauachi shaka lolote kwamba mataifa mazima mazima yataharibiwa wakati shinikizo la divai linapokanyagwa. (Isaya 63:3-6) Yoeli vilevile alitoa unabii kwamba “umati wa watu” mkubwa, mataifa mazima mazima, yangekanyagwa na kuharibiwa katika “shinikizo la divai,” katika “uwanda-bonde wa uamuzi.” (Yoeli 3:12-14, NW) Kwa kweli, ni vuno kubwa sana ambalo mfano walo hautatukia tena kamwe! Kulingana na njozi ya Yohana, si zabibu tu zinazovunwa bali mzabibu wote mzima wa ufananisho unakatwa na kutupwa ndani ya shinikizo la divai ukanyagwe. Hivyo mzabibu wa dunia utang’olewa wote na hautaweza kamwe kukua tena.

  • “Babuloni Mkubwa Ameanguka!”
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 30. Ni matunda gani ya mzabibu wa Shetani, na azimio letu limepaswa kuwa nini?

      30 Sisi tukiwa tunaishi ndani sana ya wakati wa mwisho, hiyo njozi ya haya mavuno mawili ni yenye maana sana. Tunaloweza kufanya tu ni kutazama pande zetu zote tuone yaliyo matunda ya mzabibu wa Shetani. Utoaji-mimba na namna nyinginezo za uuaji kimakusudi; ugoni-jinsia-moja, uzinzi, na namna nyingine za utovu wa adili, utovu wa haki, utovu wa shauku asilia—mambo yote kama hayo hufanya ulimwengu huu kuwa mbaya sana machoni pa Yehova. Mzabibu wa Shetani huzaa “tunda la pando lenye sumu na pakanga.” Mwendo wao wa uangamivu, wenye kuabudu sanamu hukosa kuheshimu Muumba mtukufu wa aina ya binadamu. (Kumbukumbu 29:18; 32:5; Isaya 42:5, 8, NW) Lo! ni pendeleo lililoje kuwa tukishirikiana kiutendaji na jamii ya Yohana katika kuvuna tunda zuri ambalo Yesu anatokeza kwa sifa ya Yehova! (Luka 10:2) Sisi sote na tuazimie kwamba hatutatiwa mawaa kamwe na mzabibu wa ulimwengu huu, na hivyo sisi na tuepuke kukanyagwa pamoja na huo mzabibu wa dunia wakati hukumu mbaya ya Yehova inapotekelezwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki