-
Fumbo Lenye Kutia Hofu LafumbuliwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
mimba; na wao hawataponyoka kwa vyovyote.”—1 Wathesalonike 5:2, 3, NW.
14. Huenda kilio cha “Amani na usalama!” kitakuwa cha namna gani, na mmoja anaweza kuepukaje kuongozwa vibaya?
14 Katika miaka ya hivi karibuni, wanasiasa wametumia maneno “amani na usalama” kuelezea mipango mbalimbali ya wanadamu. Je! jitihada hizo za viongozi wa ulimwengu zinaonyesha mwanzo wa utimizo wa andiko la 1 Wathesalonike 5:3? Au je, Paulo alikuwa akizungumzia tukio hususa na lenye kutokeza sana hivi kwamba lingetambuliwa ulimwenguni? Kwa kuwa mara nyingi unabii wa Biblia hueleweka kikamili tu baada ya kutimia au wakati unapoendelea kutimia, itatubidi tungoje tuone itakuwaje. Kwa sasa, Wakristo wanajua kwamba hata ingawa huenda ikaonekana kana kwamba mataifa yamepata amani na usalama, hakuna kitu ambacho kwa kweli kitakuwa kimebadilika. Ubinafsi, chuki, uhalifu, mvunjiko wa jamaa, ukosefu wa adili, magonjwa, huzuni, na kifo bado vitakuwapo. Ndiyo sababu si lazima wewe uongozwe vibaya na kilio chochote cha “amani na usalama,” ikiwa umeamka kuona maana ya matukio ya ulimwengu na unatii maonyo ya kiunabii katika Neno la Mungu.—Marko 13:32-37; Luka 21:34-36.
-
-
Kufisha Babuloni MkubwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Sura ya 35
Kufisha Babuloni Mkubwa
1. Malaika anaelezaje habari ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na ni hekima ya aina gani inayohitajiwa kuelewa mifananisho ya Ufunuo?
KATIKA kueleza zaidi habari ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu wa Ufunuo 17:3, malaika anamwambia Yohana: “Hapa ndipo elimu iliyo na hekima inapofaa: Vichwa saba humaanisha milima saba, ambako mwanamke huketi juu ya kilele. Na wako wafalme saba: watano wameanguka, mmoja yupo, mwingine hajawasili bado, lakini yeye awasilipo lazima yeye abaki kitambo kifupi.” (Ufunuo 17:9, 10, NW) Malaika anawasilisha hekima kutoka juu, hekima pekee inayoweza kutoa uelewevu wa mifananisho katika Ufunuo. (Yakobo 3:17) Hekima hii inaipa jamii ya Yohana na waandamani wayo nuru juu ya hatari ya nyakati tunamoishi. Inajenga katika mioyo yenye kujitoa uthamini wa hukumu za Yehova, ambazo sasa karibu kutimizwa, na inakaza kikiki hofu yenye afya kuelekea Yehova. Kama Mithali 9:10, NW inavyotaarifu: “Hofu ya Yehova ndio mwanzo wa hekima, na maarifa ya kumjua Mmoja Aliye Mtakatifu Zaidi Sana ndio uelewevu.” Hekima ya kimungu inatufunulia nini juu ya hayawani-mwitu?
2. Ni nini maana ya vichwa saba vya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na inakuwaje kwamba “watano wameanguka, mmoja yupo”?
2 Vichwa saba vya hayawani-mwitu mkali sana husimamia “milima” saba, au “wafalme” saba. Semi zote mbili hutumiwa Kimaandiko kurejezea mamlaka za kiserikali. (Yeremia 51:24, 25; Danieli 2:34, 35, 44, 45) Katika Biblia, serikali za ulimwengu sita hutajwa kuwa zikiathiri mambo ya watu wa Mungu: Misri, Ashuru, Babuloni, Umedi-Uajemi, Ugiriki, na Roma. Kati ya hizi, tano zilikuwa tayari zimekuja na zikaenda kufikia wakati Yohana alipopokea Ufunuo, lakini Roma ilikuwa ingali sana serikali ya ulimwengu. Hii inalingana vizuri na maneno haya, “watano wameanguka, mmoja yupo.” Lakini namna gani juu ya “mwingine” aliyekuwa akitazamiwa kuja?
3. (a) Milki ya Roma ilikujaje kugawanywa? (b) Ni matukio gani yaliyotukia katika Magharibi? (c) Milki Takatifu ya Roma yapasa ionweje?
3 Milki ya Roma ilidumu na hata ikapanuka kwa mamia ya miaka baada ya siku ya Yohana. Katika 330 W.K. Maliki Konstantino alihamisha jiji kuu lake kutoka Roma kwenda Bizanshamu, ambalo alilipa jina Konstantinopo. Katika 395 W.K., Milki ya Roma iligawanywa ikawa sehemu za Mashariki na Magharibi. Katika 410 W.K., Roma liliangushwa na Alariki, mfalme wa Wavisigothi (kabila la Kijeremani ambalo lilikuwa limeongolewa kuwa la “Ukristo” wa aina ya Aria). Makabila ya Kijeremani (ya “Kikristo” pia) yalishinda Hispania na eneo lililo kubwa zaidi la Roma katika Afrika Kaskazini. Zilikuwako karne za misukosuko, kutotulia, na kujirekebisha upya katika Ulaya. Wamaliki wenye sifa waliinuka katika Magharibi, kama vile Charlemagne, ambaye alifanya fungamano na Papa Leo 3 katika karne ya 9, na Frederick 2, ambaye alitawala katika karne ya 13. Lakini milki yao, ingawa iliitwa Milki Takatifu ya Roma ilikuwa ndogo zaidi ya ile Milki ya Roma ya mapema zaidi, wakati wa kilele cha usitawi wayo. Ilikuwa zaidi mrudisho au mwendelezo wa hiyo serikali ya kale kuliko kuwa milki mpya.
4. Milki ya Mashariki ilikuwa na mafanikio gani, lakini kulitukia nini kwa sehemu kubwa ya lililokuwa eneo la Roma ya kale katika Afrika Kaskazini, Hispania, na Siria?
4 Milki ya Mashariki ya Roma, yenye kitovu katika Konstantinopo, iliendelea ikiwa na uhusiano wenye wasiwasi na Milki ya Magharibi. Katika karne ya sita, maliki wa Mashariki Justiniani 1 aliweza kushinda sehemu kubwa ya Afrika ya Kaskazini, na pia akaingilia Hispania na Italia. Katika karne ya saba, Justiniani 2 alikombolea Milki hiyo maeneo ya Makedonia ambayo yalikuwa yameshindwa na wanamakabila wa Kislavi. Hata hivyo, Kufikia karne ya nane eneo kubwa la zamani la Roma ya kale katika Afrika Kaskazini, Hispania, na Siria lilikuwa limekuja chini ya milki mpya ya Islamu na hivyo likapita kutoka udhibiti wa Konstantinopo na Roma pia.
5. Ingawa jiji la Roma lilianguka 410 W.K., ilikuwaje kwamba ilichukua karne nyingi zaidi kabla ya visehemu vyote vya Milki ya Roma ya kisiasa kutoweka katika mandhari ya ulimwengu?
5 Jiji la Konstanipo lenyewe lilidumu kwa muda mrefu zaidi kidogo. Liliokoka mashambulizi ya mara nyingi kutoka kwa Waajemi, Waarabu, Wabulgari, na Warusi mpaka mwishowe katika 1203 likaangushwa—si na Waislamu bali na Wakrusedi kutoka Magharibi. Ingawa hivyo, katika 1453, lilikuja chini ya mamlaka ya mtawala Mwislamu wa Ottomani Mehmedi 2 na upesi likawa jiji kuu la Milki ya Ottomani, au ya Kituruki. Hivyo, ijapokuwa jiji la Roma lilianguka katika 410 W.K., ilichukua karne nyingi zaidi kabla ya visehemu vyote vya Milki ya Roma ya kisiasa kutoweka katika mandhari ya ulimwengu. Na hata hivyo, uvutano wayo bado ulitambulikana katika milki za kidini zenye msingi wa upapa wa Roma na makanisa ya Orthodoksi ya Mashariki.
6. Ni milki zipi mpya kabisa zilizotokea, na ni ipi iliyopata kuwa yenye kufanikiwa zaidi sana?
6 Hata hivyo, kufikia karne ya 15, nchi fulani zilikuwa zikijenga milki mpya kabisa. Ingawa baadhi ya serikali hizi mpya za kibepari zilipatikana katika maeneo ambayo hapo kwanza yalikuwa makoloni ya Roma, milki zazo hazikuwa mwendelezo vivi hivi wa Milki ya Roma. Ureno, Hispania, Ufaransa, na Uholanzi zote zikawa makao ya milki zilizotapakaa sana. Lakini iliyofanikiwa zaidi sana ilikuwa Uingereza, ambayo ikaja kusimamia milki kubwa mno ambayo juu yayo ‘jua halikutua kamwe.’ Milki hii ilienea katika nyakati mbalimbali juu ya sehemu kubwa ya Amerika Kaskazini, Afrika, India, na Esia Kusini-mashariki, pamoja na maeneo ya Pasifiki Kusini.
7. Serikali ya ulimwengu ya uwili ilikujaje kuwako, na Yohana alisema ni kwa muda gani ‘kichwa’ au serikali ya ulimwengu ya saba ingeendelea?
7 Kufikia karne ya 19, baadhi ya makoloni katika Amerika Kaskazini yalikuwa yamekwisha kujitenga na Uingereza yakaunda United States ya Amerika yenye kujitawala. Kisiasa, hitilafu fulani ziliendelea kati ya taifa jipya na iliyokuwa nchi-mama yao. Hata hivyo, vita ya ulimwengu ya kwanza ilizilazimisha hizo nchi zote mbili kutambua masilahi yazo ya pamoja na zikatia nguvu uhusiano maalumu kati yazo. Hivyo, namna ya serikali ya ulimwengu ya uwili ikatokea, ikiwa inafanyizwa na United States ya Amerika, sasa ikiwa ndilo taifa la ulimwengu lenye ukwasi zaidi sana, na Uingereza, kao la milki ya ulimwengu iliyo kubwa zaidi sana. Basi, hiki, ndicho ‘kichwa’ cha saba, au serikali kubwa ya ulimwengu, ambayo inaendelea mpaka ndani ya wakati wa mwisho na katika maeneo ambamo Mashahidi wa ki-siku-hizi wa Yehova walijiimarisha kwanza. Kikilinganishwa na utawala mrefu wa kichwa cha sita, hiki cha saba ‘chabaki kitambo kifupi’ mpaka Ufalme wa Mungu uangamizapo mataifa yote.
Kwa Nini Huitwa Mfalme wa Nane?
8, 9. Malaika anamwitaje hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu na ni katika njia gani huchipuka kutoka kwa wafalme saba?
8 Malaika anamweleza Yohana zaidi hivi: “Na hayawani-mwitu ambaye alikuwako lakini hayuko, yeye pia mwenyewe ni mfalme wa nane, lakini huchipuka kutoka kwa wale saba, na yeye huenda zake ndani ya uharibifu.” (Ufunuo 17:11, NW) Hayawani-mwitu wa ufananisho rangi-nyekundu-nyangavu “huchipuka kutoka” kwa vichwa saba; yaani, yeye anazaliwa na, au yuko kwa sababu ya vichwa hivyo vya ‘hayawani-mwitu kutoka bahari,’ ambaye hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu ni mfano wake. Kwa njia gani? Basi, katika 1919 serikali ya Uingereza-Amerika ilikuwa ndiyo kichwa chenye kutawala. Vile vichwa sita vilivyotangulia vilikuwa vimeanguka, nacho cheo cha serikali kubwa ya ulimwengu yenye kutawala kilikuwa kimepitishwa kwenye kichwa hiki cha uwili na sasa kikawa katika kitovu chacho. Hiki kichwa cha saba, kikiwa ndicho mwakilishi wa sasa wa mstari wa serikali za ulimwengu, kilikuwa ndicho kani yenye kutenda katika kusimamisha Ushirika wa Mataifa na kingali ndicho mwendelezaji na mtegemezaji kifedha mkuu wa Umoja wa Mataifa. Hivyo, kwa njia ya ufananisho hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu—mfalme wa nane—“huchipuka kutoka” kwa vile vichwa saba vya kwanza. Ikionwa katika njia hii, taarifa ya kwamba yeye alichipuka kutoka kwa vichwa saba inapatana vizuri na ufunuo wa mapema zaidi kwamba hayawani-mwitu mwenye pembe mbili mithili ya mwana-kondoo (Serikali ya Ulimwengu Uingereza-Amerika, kichwa cha saba cha hayawani-mwitu wa kwanza) alihimiza kufanyizwa kwa huo mfano na akaupa uhai.—Ufunuo 13:1, 11, 14, 15.
9 Kwa kuongezea, washiriki wa kwanza kabisa wa Ushirika wa Mataifa walikuwamo, pamoja na Uingereza, serikali ambazo zilitawala katika makao ya baadhi ya vichwa vilivyotangulia, yaani, Ugiriki, Irani (Uajemi), na Italia (Roma). Hatimaye, serikali zenye kutawala maeneo yaliyodhibitiwa na serikali za ulimwengu sita zilizotangulia zikaja kuwa washiriki waungaji mkono wa mfano wa hayawani-mwitu. Katika maana hii, vilevile, ingeweza kusemwa kwamba huyu hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu alichipuka kutoka kwa serikali za ulimwengu saba.
10. (a) Inaweza kusemwaje kwamba hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu “yeye pia mwenyewe ni mfalme wa nane”? (b) Kiongozi mmoja wa nchi zilizokuwa Muungano wa Sovieti alionyeshaje uungaji-mkono wake wa Umoja wa Mataifa?
10 Angalia kwamba hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu “yeye pia mwenyewe ni mfalme wa nane.” Hivyo, Umoja wa Mataifa leo unakusudiwa uonekane kuwa serikali ya ulimwengu. Nyakati fulani hata umetenda hivyo, ukituma majeshi uwanjani kusuluhisha magomvi ya kimataifa, kama vile katika Korea, Peninsula ya Sinai, nchi fulani za Kiafrika, na Lebanoni. Lakini huo ni mfano tu wa mfalme. Kama vile mfano wa kidini, huo hauna uvutano au uwezo halisi isipokuwa ule ambao unapewa na wale ambao waliutokeza na wanaouabudu. Katika pindi fulani, hayawani-mwitu huyu wa ufananisho huonekana dhaifu; lakini hajapatwa kamwe na aina ya kuachwa kwa wingi na washiriki wenye maelekeo ya udikteta ambao walifanya Ushirika wa Mataifa utetereke na kutumbukia ndani ya abiso. (Ufunuo 17:8) Ingawa anashikilia maoni yanayotofautiana sana katika maeneo mengine, kiongozi mmoja mashuhuri wa nchi zilizokuwa Muungano wa Sovieti katika 1987 alijiunga na mapapa wa Roma katika kuonyesha uungaji-mkono wa UM. Yeye hata alitaka kuwe na “mfumo mpana wa usalama wa kimataifa” wenye kutegemea UM. Kama Yohana ajifunzavyo upesi, wakati utakuja ambapo UM utatenda kwa mamlaka kubwa. Kisha huo, katika zamu yao, “huenda zake ndani ya uharibifu.”
Wafalme Kumi kwa Saa Moja
11. Malaika wa Yehova anasema nini juu ya pembe kumi zilizo juu ya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu wa ufananisho?
11 Katika sura ya Ufunuo iliyotangulia, malaika, wa sita na wa saba walimimina mabakuli ya kasirani ya Mungu. Hivyo sisi tuliarifiwa kwamba wafalme wa dunia wanakusanywa kwenye vita ya Mungu kwenye Har–Magedoni na kwamba ‘Babuloni Mkubwa apaswa kukumbukwa katika mwono wa Mungu.’ (Ufunuo 16:1, 14, 19, NW) Sasa tutajifunza kirefu zaidi jinsi hukumu za Mungu juu ya hawa zitatekelezwa. Sikiliza tena malaika wa Yehova anaponena kwa Yohana. “Na pembe kumi ambazo wewe uliona humaanisha wafalme kumi, ambao bado kupokea ufalme, lakini wao hupokea mamlaka wakiwa wafalme saa moja pamoja na hayawani-mwitu. Hawa wana fikira moja, na hivyo wao humpa hayawani-mwitu nguvu na mamlaka yao. Hawa watapigana na Mwana-Kondoo, lakini, kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme, Mwana-Kondoo atashinda wao. Pia, wale wenye kuitwa na wachaguliwa na waaminifu pamoja na yeye watafanya hivyo.”—Ufunuo 17:12-14, NW.
-