Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Fidia ya Kristo Njia ya Mungu ya Wokovu
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Februari 15
    • kabla ya kukamatwa kwake, Yesu alisema: “Ikiwa yeyote anipenda mimi, atashika neno langu.” (Yohana 14:23) “Neno” la Yesu latia ndani amri yake kwamba tushiriki kwa bidii katika kutimiza utume huu: “Nendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote, [na] kuwabatiza.” (Mathayo 28:19) Kumtii Yesu pia kwatutaka tuonyeshe ndugu zetu wa kiroho upendo.—Yohana 13:34, 35.

      21. Kwa nini yatupasa kuhudhuria sherehe ya Ukumbusho itakayokuwa Aprili 1?

      21 Njia moja nzuri zaidi ambayo twaweza kuonyesha uthamini kwa fidia ni kwa kuhudhuria Ukumbusho wa kifo cha Kristo, ambao mwaka huu utaadhimishwa Aprili 1.a Kuhudhuria pia ni sehemu ya “neno” la Yesu, kwa kuwa alipokuwa akianzisha sherehe hiyo, Yesu aliamuru wafuasi wake hivi: “Fulizeni kufanya hili katika ukumbuko wangu.” (Luka 22:19) Kwa kuhudhuria tukio hili lenye umuhimu mkubwa na kuwa makini sana kuelekea yale yote ambayo Kristo aliamuru, tutaonyesha usadikisho wetu thabiti kwamba fidia ya Yesu ni njia ya Mungu ya wokovu. Kwa kweli, “hakuna wokovu katika mwingine yeyote.”—Matendo 4:12.

  • Njia ya Upendo Haishindwi Kamwe
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Februari 15
    • Njia ya Upendo Haishindwi Kamwe

      “Fulizeni kutafuta kwa bidii zawadi zilizo kubwa zaidi. Na bado nawaonyesha nyinyi njia izidiyo.”—1 WAKORINTHO 12:31.

      1-3. (a) Kujifunza kuonyesha upendo ni sawa na kujifunza lugha mpya jinsi gani? (b) Ni mambo gani yawezayo kufanya kujifunza kuonyesha upendo kuwe jambo gumu?

      JE, UMEWAHI kujaribu kujifunza lugha mpya? Hilo ni jambo gumu, bila kutia chumvi! Bila shaka, mtoto mchanga aweza kujifunza lugha kwa kuisikia tu ikizungumzwa. Ubongo wake hushika sauti na maana ya maneno, hivi kwamba baada ya muda mfupi, mtoto huyo anaizungumza kwa ustadi sana, labda bila kusitasita. Sivyo ilivyo kwa watu wazima. Sisi huchunguza kamusi ya lugha ya kigeni tena na tena, ili tu kufahamu barabara mafungu machache ya maneno ya msingi katika lugha ya kigeni. Ingawa baada ya muda, na tukiwa tumejizoeza lugha hiyo mpya vya kutosha, sisi huanza kufikiri katika lugha hiyo na kuizungumza huwa rahisi zaidi.

      2 Kujifunza kuonyesha upendo ni kama vile kujifunza lugha mpya. Ni kweli kwamba kiasili wanadamu wana kadiri fulani ya sifa hiyo ya kimungu. (Mwanzo 1:27; linganisha 1 Yohana 4:8.) Na bado, kujifunza kuonyesha upendo huhitaji jitihada ya pekee—hasa siku hizi, ambapo shauku ya kiasili haionyeshwi sana. (2 Timotheo 3:1-5) Nyakati nyingine hali huwa hivyo hasa katika familia. Naam, wengi hukulia katika mazingira yenye ukatili ambapo maneno ya upendo husemwa mara chache, ikiwa hayo kwa vyovyote husemwa. (Waefeso 4:29-31; 6:4) Basi, sisi twaweza kujifunzaje kuonyesha upendo—hata ikiwa ni mara chache tumepata kuonyeshwa upendo huo?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki