Wimbo Na. 132
Wimbo wa Ushindi
Makala Iliyochapishwa
1. Mwimbieni Yah! Anastahili kusifiwa.
Majeshi ya Wamisri, kafa baharini.
Mutukuze Yah. Mungu asiye na kifani.
Yeye ni Yehova, Amepata ushindi.
(KORASI)
Yah Yehova, Uliye juu,
Yuleyule wa tangu milele,
Utaharibu adui zako,
2. Wote ambao wanashindana na Yehova,
Atawafedhehesha. Wataangamia.
Har-Magedoni, Hawataiokoka kamwe.
Wote watajua Anaitwa Yehova.
(KORASI)
Yah Yehova, Uliye juu,
Yuleyule wa tangu milele,
Utaharibu adui zako,
Jina lako litakaswe.
(Ona pia Zab. 2:2, 9; 92:8; Mal. 3:6; Ufu. 16:16.)