-
Azikwa Ijumaa—Ziara Tupu JumapiliYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Mapema asubuhi ya Jumapili Mariamu Magdalene, Mariamu mama yake Yakobo, pamoja na Salome, Yoana, na wanawake wengine, waja na viungo kwenye ziara ili wautie viungo mwili wa Yesu. Wakiwa njiani wanaambiana: “Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?” Lakini wafikapo, wakuta kwamba tetemeko la dunia limetokea na malaika wa Yehova amevingirisha mbali lile jiwe. Walinzi wameondoka, na ziara liko tupu! Mathayo 27:57–28:2; Marko 15:42–16:4; Luka 23:50–24:3, 10; Yohana 19:14, 31–20:1; 12:42; Walawi 23:5-7; Kumbukumbu 21:22, 23; Zaburi 34:20; Zekaria 12:10.
-
-
Yesu Yu Hai!Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 128
Yesu Yu Hai!
WANAWAKE wapatapo ziara la Yesu likiwa tupu, Mariamu Magdalene akimbia kuambia Petro na Yohana. Hata hivyo, wanawake wale wengine kwa wazi wabaki kwenye ziara. Baada ya muda mfupi, malaika atokea na kuwaalika ndani.
Hapa wanawake waona malaika mwingine bado, na mmoja wa malaika hao asema kwao hivi: “Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa [aliyetundikwa mtini, NW]. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu.” Hivyo basi wakiwa na hofu na shangwe kubwa, wanawake hao wakimbia pia kwenda zao.
Kufikia wakati huu, Mariamu amewapata Petro na Yohana, naye aripoti kwao hivi: “Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.” Mara hiyo wale mitume wawili waondoka mbio. Yohana ni mwepesi zaidi wa miguu—yaonekana kwa kuwa ni mchanga zaidi—naye afika kwanza kwenye ziara. Kufikia wakati huu wale wanawake wameondoka, hivyo basi hapo hapana mtu. Akiinama chini, Yohana achungulia ndani ya ziara na kuona vile vitambaa vya kufungia, lakini akaa nje.
Petro awasilipo, hasitisiti bali aingia moja kwa moja. Aona vitambaa vya kufungia vimelala hapo na pia ile nguo iliyotumiwa kufunga kichwa cha Yesu. Imekunjwa mviringo ikawekwa mahali pamoja. Sasa Yohana pia aingia ndani ya ziara, naye aiamini ripoti ya Mariamu. Lakini wala Petro wala Yohana haelewi kwamba Yesu ameinuliwa, hata ingawa Yeye alikuwa amewaambia mara nyingi kwamba angefanyiwa hivyo. Kwa kushangaa sana, hao wawili warudi nyumbani, lakini Mariamu, ambaye amerudi kwenye ziara, abaki.
Wakati wa sasa, wale wanawake wengine wanafanya haraka kuwaambia wanafunzi kwamba Yesu amefufuliwa, kama vile malaika walivyowaamuru kufanya. Wanapokuwa wakikimbia upesi wawezavyo, Yesu awakuta na kusema hivi: “Salamu!” Wakianguka miguuni pake, wamsujudia. Halafu Yesu asema hivi: “Msiogope; enendeni, mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona.”
Mapema kidogo, wakati tetemeko la dunia lilipotukia na malaika wakatokea, askari walinzi waliduwaa wakawa kama wanaume wafu. Waliporudiwa na fahamu, waliingia jijini mara hiyo wakawaambia makuhani wakuu yaliyokuwa yametendeka. Baada ya kushauriana na “wazee” wa Wayahudi, uamuzi wafanywa kujaribu kunyamazisha jambo hilo kwa kuwahonga askari. Wao waagizwa hivi: “Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.”
Kwa kuwa askari Waroma waweza kuadhibiwa kwa kifo kwa kulala usingizi wakiwa kwenye vituo vyao, makuhani waahidi hivi: “Neno hili [la kulala usingizi kwenu] likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.” Kwa kuwa hongo hilo ni la kiasi cha kutosha, askari hao wafanya kama vile wameagizwa. Tokeo ni kwamba, ripoti hiyo bandia juu ya wivi wa mwili wa Yesu yaenezwa kotekote miongoni mwa Wayahudi.
Mariamu Magdalene, ambaye abaki nyuma kwenye ziara, ashindwa na huzuni. Yesu angeweza kuwa wapi? Akiinama mbele atazame ndani ya ziara, aona wale malaika wawili waliovaa meupe, ambao wametokea tena! Mmoja ameketi kichwani na mwingine miguuni pa mahali ambapo mwili wa Yesu umekuwa ukilala. “Mama, unalilia nini?” wao wauliza.
“Wamemwondoa Bwana wangu,” Mariamu ajibu, “wala mimi sijui walikomweka.” Halafu ageuka na kuona mtu ambaye arudia swali hilo: “Mama, unalilia nini?” Naye pia auliza: “Unamtafuta nani?”
Akiwazia mtu huyo ndiye mtunzi wa bustani ambamo ziara limo, amwambia hivi: “Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.”
“Mariamu!” asema mtu huyo. Na mara hiyo, kutokana na njia anayoijua sana ambayo yeye huongea naye, ajua kwamba ni Yesu. “Raboni!” (maana yake “Mwalimu!”) mwanamke huyo apaaza sauti. Na kwa shangwe isiyo na mipaka, amshika sana Yesu. Lakini Yesu asema: “Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.”
Sasa Mariamu akimbia kwenda mahali ambapo mitume na wanafunzi wenzi wamekusanyika. Aongezea usimulizi wake kwenye ripoti ambayo wale wanawake wengine wametoa tayari juu ya kumwona Yesu aliyefufuliwa. Hata hivyo, wanaume hao, ambao hawakuwaamini wale wanawake wa kwanza, yaonekana hawamwamini hata Mariamu. Mathayo 28:3-15; Marko 16:5-8; Luka 24:4-12; Yohana 20:2-18.
▪ Baada ya kupata ziara likiwa tupu, Mariamu Magdalene afanya nini, na wale wanawake wengine wapatwa na jambo gani?
▪ Petro na Yohana watendaje wapatapo ziara likiwa tupu?
▪ Wale wanawake wengine wakuta nini wakiwa njiani kwenda kuripoti kwa wanafunzi juu ya ufufuo wa Yesu?
▪ Ni jambo gani lawapata askari walinzi, na ripoti yao kwa makuhani yapata itikio gani?
▪ Ni jambo gani latendeka Mariamu Magdalene awapo peke yake penye ziara, na ni nini itikio la wanafunzi kwa ripoti za wanawake hao?
-
-
Yesu Atokea Mara ZaidiYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
WANAFUNZI wangali wameshuka moyo. Hawafahamu maana ya lile ziara (kaburi) tupu, wala hawaamini habari za wale wanawake. Basi baadaye Jumapili, Kleopa na mwanafunzi mwingine waondoka Yerusalemu kwenda Emau, umbali wa karibu kilometa 11.
Wakiwa njiani, wanapozungumza matukio ya siku hiyo, mtu wasiyemjua ajiunga nao. “Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea?” auliza.
Wanafunzi hao wasimama, nyuso zao zikiwa na huzuni, naye Kleopa ajibu hivi: “Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?” Auliza: “Mambo gani?”
“Mambo ya Yesu wa Nazareti,” wao wajibu. “Wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha [wakamtundika mtini, NW]. Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli.”
Kleopa na mwandamani wake waeleza matukio ya kustaajabisha ya siku hiyo—ile habari juu ya kuonekana kusiko kwa kawaida kwa malaika na lile ziara tupu—halafu waungama kwamba wametatanishwa na maana ya mambo hayo. Mtu huyo wasiyemjua awakemea hivi: “Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?” Halafu awafasiria vifungu vya kutoka maandishi matakatifu ambavyo vyamhusu Kristo.
Mwishowe wafika karibu na Emau, na mtu yule wasiyemjua afanya kana kwamba asonga mbele na safari yake. Wakitaka kusikia zaidi, wanafunzi wahimiza hivi: “Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha.” Basi yeye akaa apate mlo. Asemapo sala na kumega mkate na kuwapokeza, wao watambua kwamba yeye kwa kweli ni Yesu akiwa katika mwili wa kibinadamu aliouvaa. Kisha atoweka.
Sasa wao waelewa ni jinsi gani mtu huyo wasiyemjua alivyojua mengi sana! “Je! mioyo yetu haikuwaka ndani yetu,” wao wauliza, “hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?” Bila kukawia, wao wainuka na kufanya haraka wakishika njia yote kurudi Yerusalemu, ambako wawakuta mitume na wale waliokusanyika pamoja nao. Kabla Kleopa na mwandamani wake hawajaweza kusema kitu, wale wengine watoa habari hii kwa msisimuko: “Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni.” Halafu wawili hao wasimulia jinsi Yesu alivyowatokea pia. Hiyo yafanya ziwe ni mara nne katika mchana huo ambazo amewatokea wanafunzi wake tofauti-tofauti.
Ghafula Yesu atokea mara ya tano. Hata ingawa milango imefungwa kwa kufuli kwa sababu wanafunzi wawahofu Wayahudi, aingia, na kusimama mle mle katikati yao, na kusema: “Amani iwe kwenu.” Wao waogopa mno, wakiwazia kwamba wanaona roho fulani. Basi, akieleza kwamba yeye si mzuka, Yesu asema hivi: “Mbona mnafadhaika? na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikeni-shikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.” Bado, wao hawataki kuamini.
Ili kusaidia akili zao zifahamu kwamba kwa kweli yeye ni Yesu, auliza hivi: “Mna chakula cho chote hapa?” Baada ya kukubali kipande cha samaki aliyekaangwa na kukila, asema hivi: “Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii, na Zaburi.”
Akiendeleza kile ambacho, kwa kweli, ni sawa na funzo la Biblia pamoja nao, Yesu afundisha hivi: “Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.”
-