-
Mwanzo wa Siku ya Mambo MakubwaYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 105
Mwanzo wa Siku ya Mambo Makubwa
YESU aondokapo Yerusalemu jioni ya Jumatatu, arudi Bethania juu ya mwinamo wa mashariki wa Mlima wa Mizeituni. Amemaliza siku mbili za huduma yake ya mwisho katika Yerusalemu. Bila shaka Yesu akaa tena usiku huo pamoja na Lazaro rafiki yake. Tangu alipowasili kutoka Yeriko siku ya Ijumaa, huu ndio usiku wa nne ambao amekaa katika Bethania.
Sasa, asubuhi na mapema Jumanne, Nisani 11, yeye na wanafunzi wake wako njiani tena. Hii yathibitika kuwa siku ya mambo makubwa ya huduma ya Yesu, iliyo na shughuli nyingi zaidi kufikia hapo. Ndiyo siku ya mwisho ya kuonekana kwake hekaluni. Nayo ndiyo siku ya mwisho ya huduma yake ya peupe kabla ya kujaribiwa na kuuawa kwake.
Yesu na wanafunzi wake wafuata njia ile ile ya kupita juu ya Mlima wa Mizeituni kuelekea Yerusalemu. Kando ya njia hiyo kutoka Bethania, Petro aona mti ambao Yesu aliulaani asubuhi iliyotangulia. “Rabi, tazama,” yeye apaaza sauti, “mtini ulioulaani umenyauka.”
Lakini kwa nini Yesu akaua mti ule? Yeye aonyesha sababu aendeleapo kusema: “Amin, nawaambia, Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu [Mlima wa Mizeituni ambao juu yao wasimama], Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.”
Kwa hiyo kwa kusababisha mti huo unyauke, Yesu anaandalia wanafunzi wake somo la kutumia kitu chenye kuonekana ili waone uhitaji wao wa kuwa na imani katika Mungu. Kama vile ambavyo ataarifu: “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Lo, ni somo la maana kama nini kwao kujifunza, hasa kwa sababu ya mitihani ya kuogofya itakayokuja karibuni! Hata hivyo, kuna uhusiano mwingine kati ya kunyauka kwa mtini na ubora wa imani.
Taifa la Israeli, kama mtini huu, lina sura ya udanganyifu. Ingawa taifa hilo limo katika uhusiano wa agano pamoja na Mungu na huenda likaonekana kinje-nje kuwa lashika virekebi vyake, limethibitika kuwa bila imani, likiwa na utasa wa kukosa matunda mema. Kwa sababu ya ukosefu wa imani, hata limo katika hatua ya kukataa Mwana wa Mungu mwenyewe! Kwa hiyo, kwa kusababisha mtini ule usiozaa unyauke, Yesu aonyesha kwa udhihirisho tokeo la mwisho kwa taifa hili lisilozaa matunda, lisilo na imani.
Punde si punde, Yesu na wanafunzi wake waingia Yerusalemu, na kama ilivyo desturi yao, waenda hekaluni, ambako Yesu aanza kufundisha. Wakuu wa makuhani na wanaume wazee wa watu, bila shaka wakifikiria kitendo ambacho Yesu alifanya siku iliyotangulia dhidi ya wavunja fedha, wamkaidi wakimuuliza: “Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri hii?”
Katika kujibu Yesu asema hivi: “Na mimi nitawauliza neno moja; ambalo mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa amri gani ninatenda haya. Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu?”
Makuhani na wanaume wazee waanza kushauriana miongoni mwao wenyewe watajibu jinsi gani. “Tukisema, Ulitoka mbinguni, atatuambia, Mbona basi hamkumwamini? Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii.”
Viongozi hawajui la kujibu. Kwa hiyo wamjibu Yesu hivi: “Hatujui.”
Yesu, naye, asema: “Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa amri gani ninatenda haya.” Mathayo 21:19-27; Marko 11:19-33; Luka 20:1-8.
▪ Ni jambo gani la maana kuhusu Jumanne, Nisani 11?
▪ Yesu aandaa masomo gani asababishapo mtini unyauke?
▪ Yesu awajibuje wale wenye kuuliza yeye afanya mambo kwa mamlaka gani?
-
-
Kufichuliwa na Vielezi vya Shamba la MizabibuYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 106
Kufichuliwa na Vielezi vya Shamba la Mizabibu
YESU yuko hekaluni. Sasa hivi tu ndipo amevuruga viongozi wa kidini waliodai kujua yeye anafanya mambo kwa mamlaka ya nani. Kabla wao hawajatulia kutoka kwenye vurugu yao, Yesu auliza hivi: “Nyinyi mwafikiri nini?” Halafu kwa njia ya kielezi, yeye awaonyesha wao ni watu wa aina gani hasa.
“Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili,” Yesu asimulia. “Akiendea yule wa kwanza, akasema, ‘Mtoto, enda ukafanye kazi leo katika shamba la mizabibu.’ Kwa kujibu huyu akasema, ‘Nitaenda, bwana,’ lakini hakwenda. Akikaribia yule wa pili, akasema ivyo hivyo. Kwa kujibu huyu akasema, ‘Mimi sitaenda.’ Baadaye akahisi majuto na kwenda. Ni yupi wa wale wawili aliyefanya penzi la baba yake?” Yesu auliza.
“Ni yule wa mwisho,” wapinzani wake wakajibu.
Kwa hiyo Yesu aeleza hivi: “Kwa kweli mimi nasema kwenu nyinyi kwamba wakusanya kodi na makahaba wanaenda mbele yenu nyinyi kuingia katika ufalme wa Mungu.” Kwa kweli, wakusanya kodi na makahaba walikataa kutumikia Mungu hapo kwanza. Lakini ndipo, kama yule mtoto wa pili, wakatubu na kumtumikia. Kwa upande mwingine, viongozi wa kidini, kama yule mtoto wa kwanza, walijidai kuwa wamtumikia Mungu, hata hivyo, kama vile Yesu aarifuvyo: “Yohana [Mbatizaji] aliwajia nyinyi katika njia ya uadilifu, lakini nyinyi hamkumwamini. Hata hivyo, wakusanya kodi na makahaba walimwamini, na nyinyi, ingawa mliona jambo hili, hamkuhisi majuto baadaye ili mmwamini.”
Ndipo Yesu aonyesha kwamba jambo ambalo limewashinda viongozi hawa wa kidini si kutojali tu kutumikia Mungu. Sivyo, bali kwa kweli wao ni watu waovu. “Kulikuwa mtu mmoja, mwenye nyumba,” Yesu asimulia, “aliyepanda shamba la mizabibu na kuweka ugo kulizunguka na akachimba shinikizo la divai humo na kusimamisha mnara, na kulikodisha kwa walimaji, na kusafiri ng’ambo. Majira ya matunda yalipofika, yeye alipeleka watumwa wake kwa walimaji ili watwae matunda yake. Hata hivyo, walimaji walichukua wale watumwa wake, na mmoja wakampiga sana, mwingine wakaua, mwingine wakampiga kwa mawe. Tena yeye akapeleka watumwa wengine, wengi kuliko wale wa kwanza, lakini wakawafanya hawa ivyo hivyo.”
“Watumwa” hao ni manabii ambao “mwenye nyumba,” Yehova Mungu, aliwatuma kwa “walimaji” wa ‘shamba lake la mizabibu.’ Walimaji hawa ni wawakilishi wenye kuongoza wa taifa la Israeli, taifa ambalo Biblia yalitambulisha kuwa ‘shamba la Mungu la mizabibu.’
Kwa kuwa “walimaji” wawatenda vibaya na kuwaua “watumwa,” Yesu aeleza hivi: “Mwisho [mwenye shamba la mizabibu] aliwapelekea mwana wake, akisema, ‘Watastahi mwana wangu.’ Kwa kumwona mwana walimaji wakasema miongoni mwao wenyewe, ‘Huyu ndiye mrithi; njoni, acheni tumuue tupate urithi wake!’ Kwa hiyo wao wakamtwaa na kumtupa nje ya shamba la mizabibu na kumuua.”
Sasa, akiwaambia viongozi hao wa kidini, Yesu auliza hivi: “Wakati mwenye shamba la mizabibu ajapo, yeye atawafanya nini walimaji hao?”
“Kwa sababu ni waovu,” viongozi wa kidini wajibu “yeye ataleta uharibifu mwovu juu yao na atakodisha shamba la mizabibu kwa walimaji wengine, ambao watamtolea yeye matunda uwapo ni wakati wayo.”
Kwa njia hiyo bila kujua viongozi hao wa kidini wapiga mbiu ya kujihukumu wenyewe, kwa maana wao wamo miongoni mwa “walimaji” Waisraeli wa “shamba la mizabibu” la Yehova ambalo ni taifa la Israeli. Tunda ambalo Yehova atarajia kutoka kwa walimaji hao ni imani katika Mwana wake, yule Mesiya wa kweli. Kwa sababu ya wao kushindwa kuandaa tunda hilo, Yesu aonya hivi: “Je! nyinyi hamjasoma kamwe katika Maandiko [kwenye Zaburi 118:22, 23], ‘Jiwe ambalo wajenzi walikataa ndilo lile ambalo limekuwa jiwe kuu la pembeni. Jambo hili limetoka kwa Yehova, nalo ni zuri sana machoni petu’? Hii ndiyo sababu mimi nasema kwenu nyinyi, ufalme wa Mungu utachukuliwa kutoka kwenu nyinyi na kupewa taifa linalotokeza matunda yalo. Pia, mtu anayeanguka juu ya jiwe hili atavunjika-vunjika kabisa. Kwa habari ya yeyote ambaye hilo laanguka juu yake, litamsaga-saga kabisa.”
Sasa waandishi na wakuu wa makuhani watambua kwamba Yesu ananena kuwahusu, nao wataka kumuua, yule “mrithi” halali. Kwa hiyo pendeleo la kuwa watawala katika Ufalme wa Mungu litatwaliwa kutoka kwao wakiwa taifa, na taifa jipya la ‘walimaji wa shamba la mizabibu’ litafanyizwa, moja ambalo litatokeza matunda yafaayo.
Kwa sababu viongozi wa kidini wahofu umati wa watu, ambao wamwona Yesu kuwa nabii, hawajaribu kumuua katika pindi hii. Mathayo 21:28-46; Marko 12:1-12; Luka 20:9-19; Isaya 5:1-7, NW.
▪ Wale watoto wawili katika kielezi cha Yesu cha kwanza wawakilisha nani?
▪ Ni nani wanaowakilishwa na “mwenye nyumba,” “shamba la mizabibu,” “walimaji,” “watumwa,” na “mrithi” katika kielezi cha pili?
▪ Itakuwaje kwa ‘walimaji wa shamba la mizabibu,’ na ni nani watachukua mahali pao?
-
-
Kielezi cha Karamu ya NdoaYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 107
Kielezi cha Karamu ya Ndoa
KWA njia ya vielezi viwili, Yesu amefichua waandishi na wakuu wa makuhani, nao wataka kumuua. Lakini Yesu angali hajamaliza mambo nao. Yeye aendelea kuwaambia kielezi kingine zaidi, akisema:
“Ufalme wa mbingu umekuwa kama mtu, mfalme, aliyefanya karamu ya ndoa kwa ajili ya mwana wake. Naye akatuma watumwa wake wakaite wale walioalikwa kwenye karamu ya ndoa, lakini wao hawakuwa na nia ya kuja.”
Yehova Mungu ndiye Mfalme ambaye atayarisha karamu ya ndoa kwa ajili ya Mwana wake, Yesu Kristo. Hatimaye, bibi-arusi wa wafuasi wapakwa-mafuta 144,000 wataungana na Yesu mbinguni. Raia za Mfalme ni watu wa Israeli, ambao, walipoingizwa ndani ya agano la Sheria katika 1513 K.W.K., walipokea fursa ya kuwa “ufalme wa makuhani.” Hivyo, katika pindi hiyo, hapo mwanzoni walitolewa mwaliko wa karamu ya ndoa.
Hata hivyo, wito wa kwanza kwa wale walioalikwa haukupelekwa mpaka vuli ya 29 W.K., wakati Yesu na wanafunzi wake (watumwa wa mfalme) walipoanza kazi yao ya kuhubiri Ufalme. Lakini Waisraeli wa asili waliopokea wito huu uliotolewa na watumwa hao kuanzia 29 W.K. hadi 33 W.K. hawakuwa na nia ya kuja. Kwa hiyo Mungu alilipa fursa nyingine taifa hilo la waalikwa, kama vile Yesu asimuliavyo:
“Tena akatuma watumwa wengine, akisema, ‘Ambieni wale walioalikwa: “Tazameni! Mimi nimetayarisha mlo wangu mkuu, ng’ombe ndume wangu na wanyama waliononeshwa wamechinjwa, na mambo yote yako tayari. Njoni kwenye karamu ya ndoa.”’” Wito huu wa pili na wa mwisho kwa wale walioalikwa ulianza katika Pentekoste 33 W.K., wakati roho takatifu ilipomiminwa juu ya wafuasi wa Yesu. Wito huu uliendelea mpaka 36 W.K.
Hata hivyo, walio wengi wa Waisraeli walikataa wito huo pia kwa madharau. “Bila kujali wakaenda zao,” Yesu asema, “mmoja kwenye shamba lake mwenyewe, mwingine kwenye shughuli yake ya kibiashara; lakini wale wengine, wakiwashika watumwa wake, waliwatenda kwa ufidhuli na kuwaua.” “Lakini,” Yesu aendelea, “mfalme akawa na hasira kuu, naye akapeleka majeshi yake na kuharibu wauaji hao na kuchoma jiji lao.” Hilo lilitukia katika 70 W.K., Yerusalemu ulipoteketezwa na kuharibiwa kabisa na Waroma, na wauaji hao wakauawa.
Halafu Yesu aeleza ilivyotukia wakati uo huo: “Ndipo [mfalme] akasema kwa watumwa wake, ‘Karamu ya ndoa iko tayari kweli kweli, lakini wale walioalikwa hawakustahiki. Kwa hiyo endeni kwenye barabara zinazoongoza nje ya jiji, na mtu yeyote mmpataye mwalikeni kwenye karamu ya ndoa.’” Watumwa wakafanya hivyo, na “chumba cha sherehe za arusi kikajaa wale wenye kuegemea kwenye meza.”
Kazi hii ya kukusanya wageni kutoka kwenye barabara zilizo nje ya jiji la walioalikwa ilianza katika 36 W.K. Ofisa wa kijeshi Mroma Kornelio na jamaa yake walikuwa ndio wa kwanza kukusanywa wakiwa watu wasiotahiriwa wasio Wayahudi. Mkusanyo wa hawa wasio Wayahudi, wote wakiwa ni wenye kuchukua nafasi za wale ambao hapo mwanzoni waliukataa wito, umeendelea ukaingia katika karne ya 20.
Ni katika karne ya 20 kwamba chumba cha sherehe ya arusi kimepata kujazwa. Yesu asimulia jambo linalotukia wakati huo, akisema: “Mfalme alipokuja ndani ili akague wageni alitupa jicho akaona mtu mmoja asiyevikwa vazi la ndoa. Kwa hiyo yeye akasema kwake, ‘Jamaa, wewe uliingiaje humu bila kuwa na vazi la ndoa?’ Akaduwaa. Ndipo mfalme akasema kwa watumishi wake, ‘Mfungeni mkono na mguu mmtupe nje ndani ya giza lililo nje. Huko ndiko kutakakokuwa kulia kwake machozi na kusaga meno kwake.’”
Mtu huyo asiye na vazi la ndoa afananisha Wakristo wa mwigizo tu wa Jumuiya ya Wakristo. Mungu hajapata kamwe kuwatambua hao kuwa wenye kitambulisho kifaacho cha kuwa Waisraeli wa kiroho. Mungu hakuwapaka mafuta kamwe kwa roho takatifu wawe warithi wa Ufalme. Kwa hiyo wao watupwa nje ndani ya giza ambamo watapatwa na uharibifu.
Yesu amalizia kielezi chake kwa kusema: “Kwa maana kuna wengi walioalikwa, lakini wachache waliochaguliwa.” Ndiyo, kuna wengi walioalikwa kutoka taifa la Israeli wawe washirika wa bibi-arusi wa Kristo, lakini ni Waisraeli wachache tu wa asili waliochaguliwa. Walio wengi wa wale wageni 144,000 ambao hupokea thawabu ya kimbingu huthibitika kuwa ni watu wasio Waisraeli. Mathayo 22:1-14; Kutoka 19:1-6; Ufunuo 14:1-3, NW.
▪ Wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi hapo mwanzoni ni nani, nao walitolewa mwaliko huo wakati gani?
▪ Wito wapelekwa lini mara ya kwanza kwa wale walioalikwa, na ni nani watumwa wenye kutumiwa kuutoa?
▪ Wito wa pili watolewa lini, na ni nani ambao waalikwa baadaye?
▪ Ni nani wanaofananishwa na yule mtu asiye na vazi la arusi?
▪ Ni nani wale wengi walioitwa, na wale wachache waliochaguliwa?
-
-
Washindwa Kutega YesuYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 108
Washindwa Kutega Yesu
KWA sababu Yesu amekuwa akifundisha hekaluni, na hivi sasa ndipo tu amemaliza kuwaambia adui zake wa kidini vielezi vitatu ambavyo vyafichua uovu wao, Mafarisayo waingiwa na kasirani na kufanya shauri wamtege aseme jambo fulani ambalo wao waweza kulitumia kufanya akamatwe. Wao watunga hila na kutuma wanafunzi wao, pamoja na wafuasi wa chama cha Herode, kujaribu kumtega ajikwae.
“Mwalimu,” watu hao wasema, “twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu. Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo?”
Yesu hapumbazwi na urairai huo. Yeye ang’amua kwamba akisema, ‘Hapana, si halali au si sawa kulipa kodi hii,’ atakuwa na hatia ya fitina dhidi ya Roma. Na bado, akisema, ‘Ndiyo, mwapaswa kulipa kodi hii,’ Wayahudi, ambao wadharau kutiishwa chini ya mamlaka ya Roma, watamchukia. Kwa hiyo yeye ajibu hivi: “Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? Nionyesheni fedha [sarafu, NW] ya kodi.”
Wamleteapo moja, auliza hivi: “Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii?”
“Ni ya Kaisari,” wao wajibu.
“Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.” Basi, watu hawa wasikiapo jibu la Yesu la ustadi, wastaajabu sana. Nao waenda zao na kumwacha kabisa.
Waonapo kwamba Mafarisayo wameshindwa kupata jambo fulani dhidi ya Yesu, Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, wamfikia na kuuliza: “Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. Vivyo hivyo na wa pili naye, na wa watatu, hata wote saba. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. Basi, katika kiyama [ufufuo, NW], atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.”
Kwa kujibu Yesu asema hivi: “Je! hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu? Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni. Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.”
Hapo tena umati wa watu washangazwa sana na jibu la Yesu. Hata baadhi ya waandishi wakiri hivi: “Mwalimu, umesema vema.”
Mafarisayo waonapo kwamba Yesu amenyamazisha Masadukayo, wao wamjia wakiwa kikundi kimoja. Ili wamjaribu zaidi, mwandishi mmoja miongoni mwao auliza hivi: “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?”
Yesu ajibu hivi: “Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana [Yehova, NW] Mungu wetu ni Bwana [Yehova, NW] mmoja; nawe mpende Bwana [Yehova, NW] Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.” Kwa uhakika, Yesu aongezea hivi: “Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.”
Yule mwandishi aafikiana naye, “Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye; na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia.”
Kwa kutambua kwamba mwandishi huyo amejibu kwa akili, Yesu amwambia: “Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu.”
Kwa siku tatu sasa—Jumapili, Jumatatu, na Jumanne—Yesu amekuwa akifundisha katika hekalu. Watu wamemsikiliza kwa furaha, hata hivyo viongozi wa kidini wataka kumuua, lakini kufikia hapo majaribio yao yamevurugwa. Mathayo 22:15-40; Marko 12:13-34; Luka 20:20-40.
▪ Mafarisayo watunga hila gani ili wamtege Yesu, na tokeo lingekuwa nini akitoa jibu la ndiyo au hapana?
▪ Yesu avurugaje majaribio ya Masadukayo ya kumtega?
▪ Ni jaribio gani zaidi ambalo Mafarisayo wafanya ili kutahini Yesu, na tokeo ni nini?
▪ Wakati wa huduma yake ya mwisho katika Yerusalemu, Yesu afundisha katika hekalu kwa siku ngapi, na tokeo ni nini?
-
-
Yesu Ashutumu Wapinzani WakeYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 109
Yesu Ashutumu Wapinzani Wake
YESU ametatanisha kabisa fikira za wapinzani wake wa kidini hivi kwamba wanahofu kumuuliza tena jambo lolote. Kwa hiyo yeye achukua hatua ya kwanza kufichua ukosefu wao wa maarifa. “Nyinyi mwafikiri nini kuhusu Kristo?” yeye auliza. “Ni mwana wa nani?”
“Wa Daudi,” Mafarisayo wajibu.
Ingawa Yesu hakani kwamba Daudi ndiye babu wa kale wa kimwili wa Kristo, au Mesiya, yeye auliza hivi: “Basi, ikoje kwamba Daudi kwa uvuvio [kwenye Zaburi 110] amwita ‘Bwana,’ akisema ‘Yehova alisema kwa Bwana wangu: “Keti kwenye mkono wangu wa kulia mpaka niweke adui zako chini ya nyayo zako”’? Ikiwa, basi, Daudi amwita ‘Bwana,’ yeye ni mwana wake jinsi gani?”
Mafarisayo wakaa kimya, kwa maana hawajui utambulisho wa kweli wa Kristo, au mpakwa-mafuta. Mesiya si mzao wa kibinadamu tu wa Daudi, kama ionekanavyo kuwa ndivyo Mafarisayo waamini, bali yeye alikuwa mbinguni na alikuwa mkuu wa Daudi, au Bwana.
Sasa akigeukia umati wa watu na wanafunzi wake, Yesu aonya kuhusu waandishi na Mafarisayo. Kwa kuwa hawa wafundisha Sheria ya Mungu, wakiwa ‘wamejiketisha wenyewe katika kiti cha Musa,’ Yesu ahimiza hivi: “Mambo yote ambayo wao waambia nyinyi, yatendeni na kuyashika.” Lakini aongezea: “Msitende kulingana na matendo yao, kwa maana wao husema lakini hawafanyi.”
Wao ni wanafiki, na Yesu awashutumu kwa usemi ule ule aliotumia alipokuwa anakula mlo katika nyumba ya Farisayo mmoja miezi kadhaa mapema. “Kazi zote ambazo wao hutenda,” yeye asema, “huzitenda ili waonwe na wanadamu.” Naye aandaa vielezi, akionelea hivi:
“Wao hupanua vikasha vyenye maandiko ambayo wao huvaa kama vilinda-usalama.” Vikasha hivi ambavyo ni vidogo kiasi, vyenye kuvaliwa katika kipaji cha uso au katika pingili ya mkono, vina visehemu vinne vya Sheria: Kutoka 13:1-10, 11-16; na Kumbukumbu 6:4-9; 11:13-21. Lakini Mafarisayo huongeza ukubwa wa vikasha hivi ili kutoa wazo la kwamba wao ni wenye bidii ya kuifuata Sheria.
Yesu aendelea kusema kwamba wao “hupanua matamvua ya mavazi yao.” Kwenye Hesabu 15:38-40 Waisraeli waamriwa wafanye matamvua katika mavazi yao, lakini Mafarisayo hufanya matamvua yao yawe makubwa kuliko ya mtu mwingine yeyote. Kila kitu hufanywa kwa kujionyesha! “Wao hupenda mahali penye umashuhuri mkubwa zaidi,” Yesu ajulisha wazi.
Kwa huzuni, wanafunzi wake mwenyewe wameathiriwa na tamaa hii ya umashuhuri. Kwa hiyo ashauri hivi: “Lakini nyinyi, nyinyi msiitwe Rabi, kwa maana ni mmoja aliye mwalimu wenu, hali nyinyi nyote ni ndugu. Zaidi ya hilo, msiite mtu yeyote baba duniani, kwa maana mmoja ni Baba yenu, yule Mmoja wa kimbingu. Wala msiitwe ‘viongozi,’ kwa maana Kiongozi wenu ni mmoja, aliye Kristo.” Ni lazima wanafunzi wajiondolee kabisa ile tamaa ya kuwa namba moja! “Aliye mkubwa zaidi miongoni mwenu nyinyi ni lazima awe mhudumu wenu,” Yesu aonya kwa upole.
Ndipo yeye atamka mfululizo wa ole juu ya waandishi na Mafarisayo, akiwaita wanafiki. Wao “hufunga kabisa ufalme wa mbingu mbele ya wanadamu,” yeye asema, na “wao ndio wenye kumeza nyumba za wajane na kwa kisingizio hufanya sala ndefu-ndefu.”
“Ole wenu, viongozi vipofu,” Yesu asema. Yeye ashutumu kukosa kwa Mafarisayo viwango vyenye thamani vya kiroho, kama inavyoshuhudiwa na mapambanuzi yenye ugeugeu ambayo wao wayafanya. Kwa kielelezo, wao wasema kwamba, ‘Si kitu mtu yeyote akiapa kwa hekalu, lakini mtu yuko chini ya wajibu akiapa kwa dhahabu ya hekalu.’ Kwa kutia mkazo mwingi juu ya dhahabu ya hekalu kuliko ule watiao juu ya thamani ya kiroho ya mahali hapo pa ibada, wao wafunua upofu wao wa kiadili.
Ndipo, kama alivyofanya mapema, Yesu awalaani vikali Mafarisayo kwa kutoyajali “mambo ya Sheria yenye uzito zaidi, yaani, haki na rehema na uaminifu” na huku wakiweka uangalifu mkubwa juu ya kutoa zaka, au sehemu ya kumi ya mimea miteketeke isiyo na maana.
Yesu awaita Mafarisayo “viongozi vipofu, ambao huchuja inzi na kuakia ngamia!” Wao huchuja inzi atoke katika divai si kwa sababu tu ni mdudu, bali kwa sababu yeye si safi kisherehe. Na bado, kupuuza kwao mambo ya Sheria yaliyo mazito zaidi kwalingana na kumeza ngamia, ambaye pia ni mnyama asiye safi kisherehe. Mathayo 22:41–23:24; Marko 12:35-40; Luka 20:41-47; Walawi 11:4, 21-24, NW.
▪ Kwa nini Mafarisayo wakaa kimya Yesu awaulizapo kuhusu alivyoyasema Daudi katika Zaburi 110?
▪ Kwa nini Mafarisayo hupanua vikasha vyao vyenye Maandiko na kupanua matamvua ya mavazi yao?
▪ Yesu awapa wafuasi wake shauri gani?
▪ Nimapambanuzi gani yenye ugeugeu ambayo Mafarisayo hufanya, na Yesu awalaanije vikali kwa kutojali mambo mazito zaidi?
-
-
Huduma Kwenye Hekalu YakamilishwaYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 110
Huduma Kwenye Hekalu Yakamilishwa
YESU anaonekana hekaluni mara ya mwisho. Kwa uhakika, anamalizia huduma yake ya peupe akiwa duniani, isipokuwa matukio ya kujaribiwa na kuuawa kwake, ambayo yako siku tatu zijazo. Sasa aendelea kuwachambua vikali waandishi na Mafarisayo.
Yeye apaaza sauti mara tatu zaidi: “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki!” Kwanza, apiga mbiu ya ole juu yao kwa sababu wao husafisha sana “sehemu ya nje ya kikombe na ya sahani, lakini kwa ndani wao wamejaa uteka-nyara na ukosefu wa kiasi.” Kwa hiyo awaonya kwa upole hivi: “Kwanza safisheni sehemu ya ndani ya kikombe na ya sahani, ili kwamba sehemu ya nje pia ipate kuwa safi.”
Ndipo atamka ole juu ya waandishi na Mafarisayo kwa sababu ya ubovu wa ndani na kuoza ambako wao wajaribu kuficha kwa kuonyesha ufuataji-dini wa nje-nje. “Nyinyi mwashabihi makaburi yaliyopakwa chokaa,” yeye asema, “ambayo kwa nje huonekana kweli kweli kuwa na uzuri mwingi lakini ndani yamejaa mifupa ya wanadamu wafu na kila namna ya ukosefu wa usafi.”
Mwishowe, unafiki wao wadhihirishwa katika nia yao ya kujengea manabii maziara na kuyapamba ili kuvuta fikira kwenye matendo yao wenyewe ya fadhili. Hata hivyo, kama Yesu afunuavyo, wao “ni wana wa wale waliowaua manabii.” Kweli kweli, mtu yeyote ambaye athubutu kufunua unafiki wao yumo hatarini!
Akiendelea, Yesu atamka mashutumu yake yaliyo makali zaidi ya yote. “Manyoka, wazao wa vipiri,” yeye asema, “ni jinsi gani nyinyi mtakimbia hukumu ya Gehena?” Gehena ni bonde lenye kutumiwa kama mahali pa kutupia takataka za Yerusalemu. Kwa hiyo Yesu asema kwamba kwa kufuatia mwendo wao mwovu, waandishi na Mafarisayo watapata uharibifu wa milele.
Kwa habari ya wale ambao yeye awatuma wakiwa wawakilishi wake, Yesu asema hivi: “Baadhi yao nyinyi mtaua na kuwatundika juu ya mti wa mateso na baadhi yao nyinyi mtapiga mijeledi katika masinagogi yenu na kuwanyanyasa kutoka jiji hata jiji; kwamba ipate kuja juu yenu damu yote ya uadilifu iliyomwagwa duniani, kuanzia damu ya Abeli mwadilifu hadi damu ya Zekaria mwana wa Barakia [mwenye kuitwa Yehoyada katika Nyakati ya Pili], ambaye nyinyi mliua kimakusudi kati ya patakatifu na madhabahu. Kwa kweli mimi nasema kwenu nyinyi, Mambo yote haya yatakuja juu ya kizazi hiki.”
Kwa sababu Zekaria aliwasuta vikali viongozi wa Israeli, “wao walitunga hila dhidi yake na wakamtupia mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya Yehova.” Lakini, kama Yesu atabirivyo, Israeli watalipia damu yote hiyo ya uadilifu iliyomwagwa. Wao wailipia miaka 37 baadaye, katika 70 W.K., wakati majeshi ya Kiroma yaharibupo Yerusalemu na Wayahudi zaidi ya milioni moja waangamia.
Yesu afikiripo hali hii yenye kuogopesha, asononeka. “Yerusalemu, Yerusalemu,” yeye apiga mbiu kwa mara nyingine, “ni mara ngapi mimi nilitaka kukusanya watoto wako pamoja, jinsi kuku hukusanya vifaranga wake pamoja chini ya mabawa yake! Lakini nyinyi watu hamkutaka hivyo. Tazameni! Mmeachiwa nyumba yenu ukiwa.”
Ndipo Yesu akaongezea: “Kuanzia sasa hamtaniona mimi kwa vyovyote mpaka mseme, ‘Mbarikiwa ni yeye ambaye aja katika jina la Yehova!’” Siku hiyo itakuwa wakati wa kuwapo kwa Kristo ajapo katika Ufalme wake wa kimbingu na watu wamwonapo kwa macho ya imani.
Sasa Yesu asonga kwenda mahali ambapo aweza kutazama makasha ya hazina katika hekalu na umati wa watu wakitumbukiza pesa humo. Matajiri watumbukiza sarafu nyingi. Lakini ndipo mjane mmoja maskini aja pale na kutumbukiza sarafu ndogo mbili za thamani ndogo sana.
Akiwaita wanafunzi wake kwake, Yesu asema: “Kwa kweli mimi nasema kwenu nyinyi kwamba mjane maskini huyu alitumbukiza zaidi ya wote wale wenye kutumbukiza pesa ndani ya yale makasha ya hazina.” Ni lazima wao wawe washangaa yawezaje kuwa hivyo. Kwa hiyo Yesu aeleza: “Wote walitumbukiza kutokana na ziada yao, lakini yeye, kutokana na shida yake, alitumbukiza chote alichokuwa nacho, maishilio yake yote.” Baada ya kusema mambo haya, Yesu aondoka kwenye hekalu kwa mara ya mwisho.
Wakistaajabia ukubwa na uzuri wa hekalu, mmoja wa wanafunzi wake apaaza sauti hivi: “Mwalimu, ona! ni mawe ya namna gani na ni majengo ya namna gani!” Kweli kweli, yaripotiwa kwamba mawe hayo yana urefu wa zaidi ya meta 11, upana wa zaidi ya meta 5, na kimo cha zaidi ya meta 3!
“Je! nyinyi mwayaona majengo makubwa haya?” Yesu ajibu. “Kwa vyovyote hakuna jiwe ambalo litaachwa hapa juu ya jiwe na lisitupwe chini.”
Baada ya kusema mambo haya, Yesu na mitume wake wavuka Bonde la Kidroni na kupanda Mlima wa Mizeituni. Wakiwa hapa waweza kulichungulia hekalu hilo lenye uzuri mwingi mno. Mathayo 23:25–24:3; Marko 12:41–13:3; Luka 21:1-6; 2 Nyakati 24:20-22, NW.
▪ Yesu afanya nini wakati wa ziara yake ya mwisho kwenye hekalu?
▪ Unafiki wa waandishi na Mafarisayo wadhihirishwaje?
▪ Ni nini kinachomaanishwa na “hukumu ya Gehena”?
▪ Kwa nini Yesu asema kwamba mjane alichanga zaidi ya matajiri?
-
-
Ishara ya Siku za MwishoYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 111
Ishara ya Siku za Mwisho
KUFIKIA sasa ni alasiri ya Jumanne. Yesu anapoketi juu ya Mlima wa Mizeituni, akitazama hekalu lililo chini, Petro, Andrea, Yakobo, na Yohana wamjia kwa faragha. Wao wahangaikia hekalu, kwa kuwa Yesu ndipo tu ametabiri kwamba ndani yalo hamna jiwe ambalo litaachwa juu ya jiwe.
Lakini kwa wazi wao wana mengi hata zaidi katika akili zao wakaribiapo Yesu. Majuma machache mapema kidogo, yeye alikuwa amenena juu ya “kuwapo” kwake, wakati ambapo “Mwana wa binadamu apasa kufunuliwa.” Na katika pindi ya mapema kidogo, alikuwa amewaambia juu ya “umalizio wa mfumo wa mambo.” Kwa hiyo mitume wana hamu nyingi ya kutaka kujua.
“Tuambie,” wao wasema, “mambo hayo [yenye kutokeza uharibifu wa Yerusalemu na hekalu lalo] yatakuwa wakati gani, na ni nini itakayokuwa ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo?” Kwa kweli, swali lao ni la sehemu tatu. Kwanza, wao wataka kujua juu ya mwisho wa Yerusalemu na hekalu lalo, halafu kuhusu kuwapo kwa Yesu katika mamlaka ya Ufalme, na hatimaye juu ya mwisho wa mfumo mzima wa mambo.
Katika jibu lake refu, Yesu ajibu sehemu zote tatu za swali hilo. Yeye aandaa ishara ambayo yatambulisha wakati mfumo wa mambo ya Kiyahudi utaisha; lakini aandaa zaidi. Pia atoa ishara ambayo itawaweka chonjo wanafunzi wake wa wakati ujao ili waweze kujua kwamba wanaishi wakati wa kuwapo kwake na karibu na mwisho wa mfumo mzima wa mambo.
Miaka ipitapo, mitume waanza kuona utimizo wa unabiii wa Yesu. Ndiyo, mambo yale yale aliyotabiri yaanza kutukia katika siku yao. Hivyo, Wakristo walio hai miaka 37 baadaye, katika 70 W.K., hawashtukiwi na uharibifu wa mfumo wa Kiyahudi na hekalu lalo.
Hata hivyo, kuwapo kwa Kristo na umalizio wa mfumo wa mambo hakutukii katika 70 W.K. Kuwapo kwake katika mamlaka ya Ufalme kwatukia baadaye sana. Lakini wakati gani? Ufikirio wa unabii wa Yesu wafunua hilo.
Yesu atabiri kwamba kutakuwako “vita na ripoti za vita.” “Taifa litainuka dhidi ya taifa,” yeye asema, na kutakuwako upungufu wa chakula, matetemeko ya dunia, na magonjwa ya kipuku. Wanafunzi wake watachukiwa na kuuawa. Manabii wa bandia watainuka na kuongoza wengi vibaya. Kutotii sheria kutaongezeka, na upendo wa idadi iliyo kubwa zaidi utapoa. Wakati uo huo, habari njema za Ufalme wa Mungu zitahubiriwa kuwa ushahidi kwa mataifa yote.
Ingawa unabii wa Yesu unakuwa na utimizo wenye mipaka kabla ya uharibifu wa Yerusalemu katika 70 W.K., utimizo wao mkubwa hutukia wakati wa kuwapo kwake na umalizio wa mfumo wa mambo. Pitio la uangalifu la matukio ya ulimwengu tangu 1914 hufunua kwamba unabii wa Yesu wenye matukio makubwa umekuwa ukipata utimizo mkubwa kuanzia mwaka huo.
Sehemu nyingine ya ishara ambayo Yesu atoa ni kuonekana kwa “kitu cha kunyarafisha kinachosababisha uharibifu.” Katika 66 W.K. kitu hicho cha kunyarafisha (kuchukiza) chatokea kwa namna ya “majeshi yenye kupiga kambi” ya Roma ambayo yazunguka Yerusalemu na kufukua ukuta wa hekalu. Hicho “kitu cha kunyarafisha” chasimama kisipopaswa.
Katika utumizo mkubwa wa ishara, hicho kitu cha kunyarafisha ni Ushirika wa Mataifa na mwandamizi wao, Umoja wa Mataifa. Tengenezo hili kwa ajili ya amani ya ulimwengu huonwa na Jumuiya ya Wakristo kuwa badala ya Ufalme wa Mungu. Lo, ni jambo lenye kunyarafisha kama nini! Kwa hiyo, baada ya muda, mamlaka za kisiasa zenye kushirikiana na UM zitageukia Jumuiya ya Wakristo (Yerusalemu wa ufananisho) na kuiacha ukiwa.
Hivyo Yesu atabiri kwamba: “Kutakuwako dhiki kubwa ya namna ambayo haijatukia tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka sasa, la, wala haitatukia tena.” Ingawa uharibifu wa Yerusalemu katika 70 W.K. unakuwa dhiki kubwa kweli kweli, kukiwa na watu zaidi ya milioni moja wenye kuripotiwa kuwa waliuawa, si dhiki kubwa kuliko Gharika ya duniani pote katika siku za Noa. Kwa hiyo utimizo mkubwa wa kisehemu hiki cha unabii wa Yesu ungali utatimizwa.
Uhakika Katika Siku za Mwisho
Jumanne, Nisani 11, ikaribiapo kumalizika, Yesu aendelea kuzungumza na mitume wake ishara ya kuwapo kwake katika mamlaka ya Ufalme na ya mwisho wa mfumo wa mambo. Yeye awaonya juu ya kukimbilia Makristo wa bandia. Majaribio yatafanywa, yeye asema, ‘kuwaongoza vibaya, ikiwezekana, hata wale wateule.’ Lakini, kama tai wenye kuona mbali, wateule hawa watakusanyika mahali palipo na chakula cha kiroho kilicho cha kweli, yaani, pamoja na Kristo wa kweli wakati wa kuwapo kwake kusikoonekana. Hawataongozwa vibaya wakusanywe pamoja kwa Kristo wa bandia.
Makristo wa bandia waweza kutokea kwa njia yenye kuonekana tu. Kwa kutofautisha, kuwapo kwa Yesu kutakuwa kusikoonekana. Kutatukia wakati wenye kuogopesha sana katika historia ya kibinadamu, kama asemavyo Yesu: “Jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wao.” Ndiyo, hiki kitakuwa ndicho kipindi chenye giza lililo jeusi kupita vyote vya kuwako kwa ainabinadamu. Itakuwa kana kwamba jua lilitiwa giza wakati wa mchana, na kana kwamba mwezi haukutoa nuru yao wakati wa usiku.
“Nguvu za mbingu zitatikiswa,” Yesu aendelea. Hivyo aonyesha kwamba mbingu halisi zitakuwa na sura yenye dalili za matazamio mabaya. Mbingu hazitakuwa milki ya nyuni tu, bali zitajawa na ndege za vita, roketi, na vipekua anga za juu. Hofu na jeuri itazidi kitu chochote kilichoonwa katika historia iliyotangulia ya kibinadamu.
Kama tokeo, Yesu asema, kutakuwako “huzuni kuu ya mataifa, yasijue njia ya kutokea kwa sababu ya mngurumo wa bahari na msukosuko wayo, huku watu wakizirai kwa sababu ya hofu na taraja la mambo yanayokuja juu ya dunia inayokaliwa.” Kweli kweli, kipindi hicho cha giza jeusi kuliko vyote vya kuwako kwa binadamu kitaongoza kwenye wakati ambao, kama Yesu asemavyo, “ishara ya Mwana wa binadamu itaonekana katika mbingu, na ndipo makabila yote ya dunia yatajipiga-piga yenyewe kwa ombolezo.”
Lakini si wote watakaokuwa wanaomboleza wakati ‘Mwana wa binadamu ajapo na mamlaka’ kuharibu mfumo huu mbovu wa mambo. “Wateule,” wale 144,000 watakaoshiriki pamoja na Kristo katika Ufalme wake wa kimbingu, hawataomboleza, wala waandamani wao, wale ambao mapema kidogo Yesu aliwaita “kondoo wengine” wake. Wajapokuwa wanaishi katika kipindi kilicho na giza jeusi kuliko vyote vya historia ya kibinadamu, hawa waitikia kitia-moyo cha Yesu: “Mambo hayo yaanzapo kutukia, jiinueni wima na kuinua vichwa vyenu juu, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”
Ili wanafunzi wake ambao wangekuwa wanaishi katika siku za mwisho waweze kupambanua ukaribu wa mwisho, Yesu atoa kielezi hiki: “Utazameni mtini na miti mingine yote: Ikiisha kuchipuka tayari, kwa kuitazama nyinyi mwajua wenyewe kwamba sasa kiangazi kiko karibu. Kwa njia hiyo nyinyi pia, wakati mnapoona mambo haya yakitukia, jueni kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Kweli kweli, mimi nasema kwenu nyinyi, Kizazi hiki hakitapitilia mbali kwa vyovyote mpaka mambo haya yote yatukie.”
Hivyo, wanafunzi waonapo zile sehemu nyingi tofauti-tofauti za ishara zikitimizwa, yawapasa wang’amue kwamba mwisho wa mfumo wa mambo uko karibu na kwamba karibuni Ufalme wa Mungu utafutilia mbali uovu wote. Kwa uhakika, mwisho utatukia katika muda wa maisha wa watu waonao utimizo wa mambo ambayo Yesu atabiri! Akionya kwa upole wale wanafunzi ambao wangekuwa hai wakati wa siku za mwisho zenye umaana mkubwa, Yesu asema:
“Jiangalieni ili mioyo yenu isije ikalemewa na kula kupita kiasi na kunywa kupita kiasi na masumbufu ya maisha, na kwa ghafula siku ile iwafyatukie kama mtego. Kwa maana itawajilia wote wale wanaokaa juu ya uso wa dunia. Endeleeni kukesha, basi, wakati wote mkifanya dua ili nyinyi mpate kufaulu katika kuyakimbia mambo hayo yote ambayo yamekusudiwa yatukie, na katika kusimama mbele ya Mwana wa binadamu.”
Wale Wanawali Wenye Hekima na Wale Wapumbavu
Yesu amekuwa akijibu ombi la mitume wake la ishara ya kuwapo kwake katika mamlaka ya Ufalme. Sasa anaandaa mambo zaidi ya ishara kwa mifano au vielezi vitatu.
Utimizo wa kila kielezi ungekuwa wenye kuonekana kwa wale wanaoishi wakati wa kuwapo kwake. Yeye atanguliza cha kwanza kwa maneno haya: “Ndipo ufalme wa mbingu utafanana na wanawali kumi ambao walitwaa taa zao na kutoka wakamlaki bwana-arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano walikuwa wenye busara.”
Kwa usemi “ufalme wa mbingu utakuwa kama wanawali kumi,” Yesu hamaanishi kwamba nusu ya wale wanaorithi Ufalme wa kimbingu ni watu wapumbavu na nusu ni wenye busara! Sivyo, bali yeye amaanisha kwamba kuhusiana na Ufalme wa mbingu, kuna upande ulio kama hivi au kama vile, au kwamba mambo kuhusiana na Ufalme yatakuwa kama kitu fulani-fulani.
Wale wanawali kumi wafananisha Wakristo wote ambao wako katika mstari kwa au ambao hudai kuwa katika mstari kwa ajili ya Ufalme wa kimbingu. Ilikuwa wakati wa Pentekoste 33 W.K. kwamba lile kundi la Kikristo lilipewa ahadi ya ndoa kwa Yesu Kristo, Bwana-arusi aliyefufuliwa na kutukuzwa. Lakini ndoa hiyo ingetukia katika mbingu katika wakati fulani ujao usiodhihirishwa.
Katika kielezi kile, wale wanawali kumi wanatoka kwenda wakiwa na kusudi la kumlaki bwana-arusi na kujiunga pamoja naye katika mwandamano wa arusi. Awasilipo, wao wataangazia njia ya mwandamano kwa taa zao, hivyo kumheshimu aletapo bibi-arusi wake kwenye nyumba aliyotayarishiwa. Hata hivyo, Yesu aeleza: “Wale wapumbavu walitwaa taa zao lakini wasitwae mafuta pamoja nao, hali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Bwana-arusi alipokuwa anakawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.”
Ukawivu mwendelevu wa bwana-arusi huonyesha kwamba kuwapo kwa Kristo akiwa Mfalme anayetawala kungekuwa katika wakati ujao ulio mbali. Hatimaye anakuja kwenye kiti chake cha ufalme katika mwaka 1914. Wakati wa ule usiku mrefu kabla ya hapo, wale wanawali wote wanalala usingizi. Lakini hawakushutumiwa kwa sababu hiyo. Wale wanawali wapumbavu wanashutumiwa kwa kutokuwa na mafuta kwa ajili ya vyombo vyao. Yesu aeleza namna wale wanawali wanavyoamka kabla ya bwana-arusi kuwasili: “Katikati ya usiku barabara kukazuka kilio, ‘Bwana-arusi yupo hapa! Shikeni njia yenu kumlaki.’ Ndipo hao wanawali wote wakainuka na kutayarisha taa zao. Wale wapumbavu wakasema kwa wale wenye busara, ‘Tupeni baadhi ya mafuta yenu, kwa sababu taa zetu zakaribia kuzimika.’ Wale wenye busara wakajibu kwa maneno haya, ‘Labda hakuwezi kuwa yakututosha sisi na nyinyi. Badala ya hivyo, shikeni njia yenu, mwende kwa wale wenye kuyauza mkajinunulie.’”
Mafuta yafananisha kile kinachowaendeleza Wakristo wa kweli wakiwa wanaangaza wakiwa vimulikaji. Hilo ni Neno la Mungu lililovuviwa, ambalo Wakristo wanashika sana, pamoja na roho takatifu, ambayo huwasaidia katika kuelewa Neno hilo. Mafuta hayo ya kiroho huwezesha wale wanawali wenye busara waangaze nuru katika kumkaribisha bwana-arusi wakati wa mwandamano wa kwenda kwenye karamu ya ndoa. Lakini jamii ya wale wanawali wapumbavu haina ndani yao, katika vyombo vyao, yale mafuta ya kiroho yanayohitajiwa. Kwa hiyo Yesu aeleza linalotukia:
“Wakati [hao wanawali wapumbavu] walipokuwa wakienda zao kununua [mafuta], bwana-arusi akawasili, na wale wanawali ambao walikuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya ndoa; na mlango ukafungwa. Baadaye wale wengine wa wanawali wakaja pia, wakisema, ‘Bwana, bwana, tufungulie!’ Katika kujibu yeye akasema, ‘Mimi nawaambia ukweli, Mimi siwajui nyinyi.’”
Baada ya Kristo kuwasili akiwa katika Ufalme wake wa kimbingu, jamii ya wale wanawali wenye busara ya Wakristo wa kweli wapakwa-mafuta waamka kwenye pendeleo lao la kuangaza nuru katika ulimwengu huu uliotiwa giza katika kusifu Bwana-arusi aliyerudi. Lakini wale waliofananishwa na wale wanawali wapumbavu wanakuwa hawako tayari kuandaa sifa hii ya kukaribisha. Kwa hiyo wakati ufikapo, Kristo hawafungulii mlango wa karamu ya ndoa katika mbingu. Yeye awaacha nje katika weusi wa usiku mzito zaidi ya wote wa ulimwengu, wakapotee na wafanya kazi wengine wote wa uasi-sheria. “Endeleeni kukesha, basi,” Yesu amalizia, “kwa sababu nyinyi hamjui wala siku ile wala saa ile.”
Kile Kielezi cha Talanta
Yesu aendeleza mazungumzo pamoja na mitume wake katika Mlima wa Mizeituni kwa kuwaambia kielezi kingine, cha pili katika mfululizo wa vielezi vitatu. Siku chache mapema kidogo, alipokuwa Yeriko, alitoa kielezi cha mina kuonyesha kwamba Ufalme ulikuwa ungali mbali katika wakati ujao. Kielezi ambacho asimulia sasa, ingawa kina sehemu kadhaa zenye kufanana, chaeleza katika utimizo wacho utendaji mbalimbali wakati wa kuwapo kwa Kristo katika mamlaka ya Ufalme. Chatoa kielezi kwamba ni lazima wanafunzi wake wafanye kazi wakiwa wangali duniani ili kuongezea “mali zake.”
Yesu aanza hivi: “Kwa maana hiyo [yaani, hali zenye kuhusiana na Ufalme] ni kama wakati mtu, akiwa karibu kusafiri ng’ambo, aliita watumwa wake na kuwakabidhi mali zake.” Yesu ndiye mtu ambaye, kabla ya kusafiri ng’ambo mbinguni, akabidhi watumwa wake—wanafunzi walio katika mstari wa kupata Ufalme wa kimbingu—mali zake. Mali hizi si mali za kimwili, bali zawakilisha shamba lililolimwa ambamo yeye amejenga uwezekano wa kutokeza wanafunzi zaidi.
Yesu akabidhi mali zake kwa watumwa wake muda mfupi kabla ya kupaa mbinguni. Yeye afanyaje hivyo? Kwa kuwaagiza waendelee kufanya kazi katika shamba lililositawishwa kwa kuhubiri ujumbe wa Ufalme kwenye sehemu za mbali kabisa za dunia. Ni kama vile Yesu asemavyo: “Alimpa mmoja talanta tano, mwingine mbili, mwingine bado akampa moja, kila mmoja kulingana na uwezo wake mwenyewe, naye akaenda ng’ambo.”
Hivyo hizo talanta nane—mali za Kristo—zagawanywa kulingana na kadiri za uwezo, au kadiri za uwezekano wa kiroho, za watumwa. Watumwa hao wanasimamia jamii za wanafunzi. Katika karne ya kwanza, jamii iliyopokea talanta tano kwa wazi ilitia ndani mitume. Yesu aendelea kueleza kwamba wale watumwa waliopokea zile talanta tano na mbili walizirudufisha kwa kuhubiri kwao Ufalme na kufanya wanafunzi. Hata hivyo, mtumwa aliyepokea ile talanta moja aliificha katika ardhi.
“Baada ya muda mrefu,” Yesu aendelea kusema, “bwana-mkubwa wa watumwa hao alikuja akafanya hesabu nao.” Haikuwa mpaka karne ya 20, yapata miaka 1,900 baadaye, kwamba Kristo akarudi kufanya hesabu, kwa hiyo, ilikuwa kweli kweli, “baada ya muda mrefu.” Ndipo Yesu aeleza hivi:
“Yule mmoja aliyekuwa amepokea talanta tano akaja mbele na kuleta talanta tano za ziada, akisema, ‘Bwana-mkubwa, wewe ulinikabidhi talanta tano; ona, nilipata talanta tano zaidi.’ Bwana-mkubwa wake akamwambia, ‘Vema, mtumwa mwema na mwaminifu! Wewe ulikuwa mwaminifu juu ya vitu vichache. Mimi nitakuweka juu ya vitu vingi. Ingia ndani ya shangwe ya bwana-mkubwa wako.’” Vivyo hivyo mtumwa aliyepokea talanta mbili alirudufisha talanta zake, na alipokea pongezi na thawabu ile ile.
Ingawa hivyo, watumwa hawa waaminifu huingiaje ndani ya shangwe ya Bwana-mkubwa wao? Basi, shangwe ya Bwana-mkubwa wao, Yesu Kristo, ni ile ya kupokea umiliki wa Ufalme alipoenda ng’ambo kwa Baba yake mbinguni. Kwa habari ya watumwa waaminifu katika nyakati za ki-siku-hizi, wao wana shangwe kubwa katika kuaminishwa madaraka zaidi ya Ufalme, na wanapomaliza mwendo wao wa kidunia, watakuwa na shangwe ya upeo ya kufufuliwa kwenye Ufalme wa kimbingu. Lakini namna gani juu ya mtumwa wa tatu?
“Bwana-mkubwa, mimi nilikujua wewe kuwa u mtu mwenye kutoza sana,” mtumwa huyu alalamika. “Kwa hiyo mimi niliogopa nikaenda na kuficha talanta yako katika ardhi. Hii hapa chukua kilicho chako.” Mtumwa huyo alikataa kimakusudi kufanya kazi katika shamba lililositawishwa kwa kuhubiri na kufanya wanafunzi. Kwa hiyo bwana-mkubwa amwita “mwovu na goigoi” na kutamka hukumu: “Mpokonyeni talanta . . . na mmtupe mtumwa asiyefaa kitu nje ndani ya giza la nje. Huko ndiko kutakuwako kilio chake na kusaga meno yake.” Wale wa jamii hii ya mtumwa mwovu, kwa kutupwa nje, hunyimwa shangwe yoyote ya kiroho.
Hii hutokeza somo zito kwa wote ambao hudai kuwa wafuasi wa Kristo. Ni lazima wafanye kazi ili kuongezea mali za Bwana-mkubwa wao wa kimbingu kwa kuwa na ushiriki kamili katika kazi ya kuhubiri ikiwa wataona shangwe ya kupongezwa na kuthawabishwa, na ikiwa wataepuka kutupwa ndani ya giza lililo nje na uharibifu wa hatimaye. Je! wewe u mwenye bidii ya uendelevu katika habari hii?
Kristo Awasilipo Katika Mamlaka ya Ufalme
Yesu angali pamoja na mitume wake juu ya Mlima wa Mizeituni. Katika kujibu ombi lao la ishara ya kuwapo kwake na ya umalizio wa mfumo wa mambo, sasa awaambia kielezi kilicho cha mwisho katika mfululizo wa vielezi vitatu. “Awasilipo Mwana wa binadamu katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye,” Yesu aanza, “ndipo atakapoketi juu ya kiti cha ufalme chake chenye utukufu.”
Wanadamu hawawezi kuona malaika katika utukufu wao wa kimbingu. Kwa hiyo kuwasili kwa Mwana wa binadamu, Yesu Kristo, pamoja na malaika ni lazima kuwe kusikoonekana kwa macho ya kibinadamu. Kuwasili huko kwatukia katika mwaka 1914. Lakini kwa kusudi gani? Yesu aeleza hivi: “Mataifa yote yatakusanywa mbele zake, naye atatenga watu mmoja kutoka kwa mwingine, kama vile mchungaji atengavyo kondoo kutoka kwa mbuzi. Naye ataweka kondoo katika mkono wake wa kulia, bali mbuzi katika kushoto kwake.”
Akisimulia litakalopata wale waliotengwa wawe upande wenye kupendelewa, Yesu asema hivi: “Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, ‘Njooni nyinyi wenye kubarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme uliotayarishwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi ya ulimwengu.’” Kondoo wa kielezi hiki hawatatawala pamoja na Kristo mbinguni bali watarithi Ufalme katika maana ya kuwa raia zao za kidunia. “Kuwekwa msingi wa ulimwengu” kulitukia wakati Adamu na Hawa walipozaa kwanza watoto ambao wangeweza kunufaika na uandalizi wa Mungu wa kufidia ainabinadamu.
Lakini kwa nini kondoo hutengwa wawe kwenye mkono wa kulia wenye upendeleo wa Mfalme? “Kwa maana mimi nilipata kuwa na njaa,” ajibu mfalme, “na nyinyi mlinipa kitu cha kula; nilipata kuwa na kiu na nyinyi mlinipa kitu cha kunywa. Nilikuwa mgeni na nyinyi mkanipokea kwa ukaribishaji wageni; uchi, na nyinyi mkanivika mavazi. Nilipata kuwa mgonjwa na nyinyi mkanitunza. Nilikuwa gerezani na nyinyi mlinijia.”
Kwa kuwa kondoo wapo duniani, wao wataka kujua ni jinsi gani wangeweza kuwa walimfanyia Mfalme wao wa kimbingu matendo mema jinsi hiyo. Wao wauliza, “Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa nasi tukakulisha wewe,” wao wauliza, “au mwenye kiu, nasi tukakupa kitu cha kunywa? Ni lini sisi tulipokuona wewe u mgeni na tukakupokea wewe kwa ukaribishaji wageni, au uchi, na kukuvika mavazi wewe? Ni lini tulipokuona wewe u mgonjwa au gerezani na kuja kwako?”
“Kweli kweli, mimi nawaambia nyinyi,” Mfalme ajibu, “kwa kadiri ambayo nyinyi mlifanya hivyo kwa mmoja aliye mdogo zaidi ya wote wa hawa ndugu zangu, nyinyi mlifanya hilo kwangu mimi.” Ndugu za Kristo ni wale waliosalia duniani kati ya wale 144,000 watakaotawala pamoja naye mbinguni. Na kuwafanyia mema, Yesu asema, ni sawa na kumfanyia yeye mema.
Halafu, Mfalme ahutubia wale mbuzi. “Nendeni zenu kutoka kwangu mimi, nyinyi mliolaaniwa, mkaingie katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika zake. Kwa maana mimi nilipata kuwa na njaa, lakini nyinyi hamkunipa chochote cha kula, na nilipata kuwa na kiu, lakini nyinyi hamkunipa chochote cha kunywa. Nilikuwa mgeni, lakini nyinyi hamkunipokea kwa ukaribishaji wageni; uchi, lakini nyinyi hamkunivika mavazi; mgonjwa na katika gereza, lakini nyinyi hamkunitunza mimi.”
Hata hivyo, mbuzi wale walalamika hivi: “Bwana, ni lini tulipokuona wewe ukiwa na njaa au kiu au mgeni au uchi au mgonjwa au gerezani na hatukukuhudumia wewe?” Mbuzi wahukumiwa vikali kwa msingi ule ule ambao kondoo wahukumiwa kwa njia yenye kupendelewa. “Kwa kadiri ambayo nyinyi hamkufanya hivyo kwa mmoja aliye mdogo zaidi ya wote [wa ndugu zangu],” Yesu ajibu, “nyinyi hamkunifanyia mimi hilo.”
Kwa hiyo kuwapo kwa Kristo katika mamlaka ya Ufalme, kabla tu ya mwisho wa huu mfumo mbovu wa mambo katika ile dhiki kubwa, utakuwa wakati wa hukumu. Wale mbuzi “wataondoka wakaingie katika kukatiliwa mbali milele, bali wale wenye uadilifu [kondoo] wakaingie katika uhai wa milele.” Mathayo 24:2–25:46; 13:40, 49; Marko 13:3-37; Luka 21:7-36; 19:43, 44; 17:20-30; 2 Timotheo 3:1-5; Yohana 10:16; Ufunuo 14:1-3, NW.
▪ Ni kitu gani kinachowasukuma mitume waulize swali lao, lakini kwa wazi ni kitu gani kingine walicho nacho katika akili zao?
▪ Ni sehemu gani ya unabii wa Yesu inatimizwa katika 70 W.K., lakini ni nini hakitukii wakati huo?
▪ Unabii wa Yesu wapata utimizo wa kwanza lini, lakini ni lini unapokuwa na utimizo mkubwa?
▪ Ni nini kitu cha kunyarafisha katika utimizo wacho wa kwanza na wa mwisho?
▪ Kwa nini dhiki kubwa haiwi na utimizo wa mwisho kwa uharibifu wa Yerusalemu?
▪ Ni hali gani za ulimwengu zatia alama kuwapo kwa Kristo?
▪ Ni wakati gani ‘makabila yote ya dunia yanapojipiga-piga yenyewe kwa ombolezo,’ lakini wafuasi wa Yesu watakuwa wakifanya nini?
▪ Yesu aandaa kielezi gani kusaidia wanafunzi wake wa wakati ujao kufahamu wakati mwisho uko karibu?
▪ Ni shauri gani ambalo Yesu aandalia baadhi ya wanafunzi wake ambao wangekuwa wakiishi katika siku za mwisho?
▪ Ni nani wanafananishwa na wale wanawali kumi?
▪ Kundi la Kikristo liliahidiwa ndoa kwa bwana-arusi wakati gani, lakini bwana-arusi awasili wakati gani apeleke bibi-arusi wake kwenye karamu ya ndoa?
▪ Mafuta yawakilisha nini, na kuwa nayo kwawezesha wale wanawali wenye busara wafanye nini?
▪ Karamu ya ndoa inatukia wapi?
▪ Wale wanawali wapumbavu wakosa thawabu gani tukufu, nao wapatwa na nini?
▪ Kielezi cha talanta chafundisha somo gani?
▪ Watumwa ni nani, na mali wanazoaminishwa ni nini?
▪ Ni wakati gani bwana-mkubwa aja kufanya hesabu, naye apata nini?
▪ Ni shangwe gani ambamo watumwa waaminifu waingia, na mtumwa wa tatu, yule mwovu apatwa na nini?
▪ Kwa nini kuwapo kwa Kristo lazima kuwe kusikoonekana, na ni kazi gani ambayo afanya wakati huo?
▪ Kondoo warithi Ufalme katika maana gani?
▪ “Kuwekwa msingi wa ulimwengu” kulitukia wakati gani?
▪ Watu wahukumiwa kuwa kondoo au mbuzi kwa msingi gani?
-
-
Sikukuu ya Kupitwa Iliyo ya Mwisho kwa Yesu YakaribiaYule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
-
-
Sura 112
Sikukuu ya Kupitwa Iliyo ya Mwisho kwa Yesu Yakaribia
JUMANNE, Nisani 11, ikaribiapo, Yesu amaliza kufundisha mitume juu ya Mlima wa Mizeituni. Lo, imekuwa siku yenye mikazo na shughuli kama nini! Sasa, labda akiwa anarudi Bethania akakae huko usiku huo, awaambia hivi mitume wake: “Nyinyi mwajua kwamba siku mbili kuanzia sasa sikukuu ya Kupitwa yatukia, na Mwana wa binadamu atatolewa atundikwe.”
-