Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Utasimamaje Mbele ya Kiti cha Hukumu?
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Oktoba 15
    • za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.”—Wakolosai 1:13; 3:1.

      15, 16. (a) Kwa nini tunasema kwamba Yesu hakuwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu katika 33 W.K.? (b) Ni lini Yesu alianza kutawala katika Ufalme wa Mungu?

      15 Hata hivyo, wakati huo Yesu hakutenda akiwa Mfalme na Hakimu juu ya mataifa. Alikuwa ameketi kando ya Mungu, akingojea wakati wa kutenda akiwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu. Paulo aliandika hivi juu yake: “Je! yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?”—Waebrania 1:13.

      16 Mashahidi wa Yehova wamechapisha uthibitisho mwingi kwamba kipindi cha Yesu cha kungojea kiliisha 1914, alipokuja kuwa mtawala wa Ufalme wa Mungu katika mbingu zisizoonekana. Ufunuo 11:15, 18 lasema: “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.” “Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja.” Ndiyo, mataifa yalionyeshana ghadhabu katika Vita ya Ulimwengu 1. (Luka 21:24) Vita, matetemeko ya dunia, magonjwa ya kuambukiza, upungufu wa chakula, na mambo kama hayo, ambayo tumeona tangu 1914 yathibitisha kwamba Yesu anatawala sasa katika Ufalme wa Mbinguni, na mwisho kabisa wa ulimwengu u karibu.—Mathayo 24:3-14, NW.

      17. Ni mambo gani makuu ambayo tumethibitisha kufikia sasa?

      17 Kwa kupitia kifupi: Mungu aweza kusemwa kuwa ameketi katika kiti cha ufalme akiwa Mfalme, lakini kwa maana nyingine anaweza kuketi katika kiti chake cha ufalme ili kuhukumu. Katika 33 W.K., Yesu aliketi upande wa kuume wa Mungu, naye sasa ni Mfalme wa Ufalme. Lakini, je, Yesu, anayetawala sasa akiwa Mfalme, pia atumika akiwa Hakimu? Na kwa nini jambo hili lituhusu, hasa wakati huu?

      18. Kuna uthibitisho gani kwamba Yesu angekuwa Hakimu pia?

      18 Yehova, ambaye ana haki ya kuweka rasmi mahakimu, alimchagua Yesu kuwa Hakimu anayefikia viwango Vyake. Yesu alionyesha hilo alipokuwa akisema juu ya watu kuwa hai kiroho: “Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote.” (Yohana 5:22) Lakini, fungu la Yesu la kihukumu lapita aina hiyo ya hukumu, kwani yeye ni hakimu wa walio hai na wafu. (Matendo 10:42; 2 Timotheo 4:1) Pindi moja Paulo alitangaza: “[Mungu] ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule [Yesu] aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.”—Matendo 17:31; Zaburi 72:2-7.

      19. Kwa nini ni sahihi kusema juu ya Yesu kuwa anaketi akiwa Hakimu?

      19 Basi, je, tuna haki ya kukata kauli kwamba Yesu aketi katika kiti cha ufalme chenye utukufu katika fungu hususa la Hakimu? Ndiyo. Yesu aliwaambia mitume: “Katika uumbaji-upya wakati Mwana wa binadamu aketipo juu ya kiti chake cha ufalme chenye utukufu, nyinyi ambao mmenifuata mtaketi nyinyi wenyewe pia juu ya viti vya ufalme kumi na viwili, mkihukumu yale makabila kumi na mawili ya Israeli.” (Mathayo 19:28, NW) Ingawa Yesu sasa ni Mfalme wa Ufalme, utendaji wake wa ziada unaotajwa katika Mathayo 19:28 utatia ndani kuketi katika kiti cha ufalme ili kuhukumu katika Mileani. Wakati huo atahukumu wanadamu wote, waadilifu na wasio waadilifu. (Matendo 24:15) Yafaa kukumbuka hili tugeuziapo fikira zetu mmojawapo mifano ya Yesu unaohusu wakati wetu na maisha zetu.

      Mfano Huu Wasema Nini?

      20, 21. Mitume wa Yesu waliuliza nini kinachohusu wakati wetu, kikitokeza swali gani?

      20 Muda mfupi kabla ya Yesu kufa, mitume wake walimwuliza hivi: “Mambo haya yatakuwa wakati gani, nayo ni nini itakuwa ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo?” (Mathayo 24:3, NW) Yesu alitabiri matukio muhimu ambayo yangetokea duniani kabla ya ‘mwisho kuja.’ Muda mfupi kabla ya mwisho huo, mataifa “yatamwona Mwana wa binadamu akija juu ya mawingu ya mbinguni na nguvu na utukufu mkubwa.”—Mathayo 24:14, 29, 30, NW.

      21 Lakini, itakuwaje kwa watu katika mataifa hayo Mwana wa binadamu afikapo katika utukufu wake? Ebu tuone kutokana na mfano wa kondoo na mbuzi, unaoanza kwa maneno haya: “Wakati Mwana wa binadamu awasilipo katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti chake cha ufalme chenye utukufu. Na mataifa yote yatakusanywa mbele yake.”—Mathayo 25:31, 32, NW.

      22, 23. Ni mambo yapi yaonyeshayo kwamba mfano wa kondoo na mbuzi haukuanza kutimizwa katika 1914?

      22 Je, mfano huu unahusu wakati Yesu alipoketi katika mamlaka ya kifalme katika 1914, kama ambavyo tumeelewa kwa muda mrefu? Naam, Mathayo 25:34 lasema juu yake akiwa Mfalme, kwa hiyo kwa kupatana na akili mfano huu wahusu tangu wakati Yesu alipokuwa Mfalme katika 1914. Lakini ni hukumu gani aliyofanya upesi baadaye? Haikuwa hukumu ya “mataifa yote.” Badala ya hivyo, alielekeza uangalifu wake kwa wale wanaodai kufanyiza “nyumba ya Mungu.” (1 Petro 4:17, italiki ni zetu.) Kwa kupatana na Malaki 3:1-3, Yesu, akiwa mjumbe wa Yehova, alikagua kihukumu Wakristo watiwa-mafuta waliosalia duniani. Pia ulikuwa wakati wa kutoa adhabu ya kihukumu juu ya Jumuiya ya Wakristo, waliodai kwa uwongo kuwa “nyumba ya Mungu.”c (Ufunuo 17:1, 2; 18:4-8) Lakini hakuna chochote kionyeshacho kwamba wakati huo, au tangu wakati huo, Yesu aliketi ili kuhukumu watu wa mataifa yote hatimaye kuwa kondoo au mbuzi.

      23 Tukichanganua utendaji wa Yesu katika mfano huu, twamwona hatimaye akihukumu mataifa yote. Mfano huu hauonyeshi kwamba kuhukumu huko kungeendelea kwa kipindi kirefu cha miaka mingi, kana kwamba kila mtu aliyekufa katika miongo hii ambayo imepita alihukumiwa kustahili kifo kidumucho milele au uhai udumuo milele. Yaonekana kwamba wengi ambao wamekufa katika miongo ya majuzi wameenda katika kaburi la kawaida la wanadamu. (Ufunuo 6:8; 20:13) Hata hivyo, huu mfano waonyesha wakati ambapo Yesu ahukumu watu wa “mataifa yote” ambao wakati huo wako hai na wanakabili utekelezaji wa adhabu yake ya kihukumu.

      24. Ni lini mfano wa kondoo na mbuzi utakapotimizwa?

      24 Kwa maneno mengine, mfano huu waelekezea wakati ujao ambapo Mwana wa binadamu atakuja katika utukufu wake. Ataketi ili kuhukumu watu wanaoishi wakati huo. Hukumu yake itategemea kile ambacho wamejidhihirisha wenyewe kuwa. Wakati huo ‘upambanuzi kati ya wenye haki na waovu’ utakuwa umethibitishwa wazi. (Malaki 3:18) Kule kutangaza hasa na kutekeleza hukumu kutafanywa kwa kipindi kifupi. Yesu atatoa maamuzi yenye haki yanayotegemea yale ambayo watu mmoja-mmoja watakuwa wamedhihirisha wazi.—Ona pia 2 Wakorintho 5:10.

      25. Mathayo 25:31 laonyesha nini likisema juu ya Mwana wa binadamu akiketi katika kiti cha utukufu?

      25 Basi, hii yamaanisha kwamba ‘kuketi kwa Yesu katika kiti chake cha utukufu’ ili kutoa hukumu, kunakotajwa katika Mathayo 25:31, kwahusu wakati ujao wakati Mfalme huyu mwenye nguvu atakapoketi kutangaza na kutekeleza hukumu dhidi ya mataifa. Ndiyo, mandhari ya hukumu inayohusu Yesu katika Mathayo 25:31-33, 46 yalingana na mandhari iliyo katika Danieli sura ya 7, ambamo Mfalme anayetawala, Mkale wa Siku, aliketi ili kutekeleza fungu lake akiwa Hakimu.

      26. Ni maelezo gani mapya ya huu mfano yanayodhihirika?

      26 Kuelewa huu mfano wa kondoo na mbuzi kwa njia hii kwaonyesha kwamba kutoa hukumu juu ya kondoo na mbuzi ni kwa wakati ujao. Kutatokea baada ya “dhiki” inayotajwa katika Mathayo 24:29, 30 kufyatuka na Mwana wa binadamu ‘kufika katika utukufu wake.’ (Linganisha Marko 13:24-26, NW.) Ndipo, mfumo huu wote ukiwa umefikia mwisho wao, Yesu atafanya mahakama na kutoa na kutekeleza hukumu.—Yohana 5:30; 2 Wathesalonike 1:7-10.

      27. Tunapaswa kupendezwa kujua nini kuhusu mfano wa mwisho wa Yesu?

      27 Hili lasahihisha uelewevu wetu juu ya wakati wa utimizo wa mfano wa Yesu, unaoonyesha wakati kondoo na mbuzi watakapohukumiwa. Lakini hilo latuhusuje sisi tunaohubiri kwa bidii habari njema ya Ufalme? (Mathayo 24:14) Je, hilo lafanya kazi yetu isiwe na umaana zaidi, au laleta daraka kubwa zaidi? Ebu tuone katika makala ifuatayo jinsi tunavyohusika.

  • Kuna Wakati Ujao Gani kwa Kondoo na Mbuzi?
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Oktoba 15
    • Kuna Wakati Ujao Gani kwa Kondoo na Mbuzi?

      “Atatenganisha watu, kama vile mchungaji atenganishavyo kondoo na mbuzi.”—MATHAYO 25:32, NW.

      1, 2. Kwa nini mfano wa kondoo na mbuzi utupendeze?

      HAKIKA Yesu Kristo alikuwa Mwalimu mkubwa kupita wote duniani. (Yohana 7:46) Mojayapo njia zake za kufundisha ilikuwa kutumia mifano, au vielezi. (Mathayo 13:34, 35) Mifano hiyo ilikuwa sahili lakini yenye nguvu sana katika kujulisha kweli za ndani za kiroho na za kiunabii.

      2 Katika mfano wa kondoo na mbuzi, Yesu alielekezea wakati wake wa kutenda katika fungu la kipekee: “Wakati Mwana wa binadamu awasilipo katika utukufu wake, na . . . ” (Mathayo 25:31, NW) Hili lapaswa litupendeze kwa sababu hicho ndicho kielezi ambacho Yesu amalizia katika kujibu lile swali: “Ni nini itakuwa ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo?” (Mathayo 24:3, NW) Lakini hili lamaanisha nini kwetu?

      3. Mapema katika maneno yake, Yesu alisema nini kingetukia mara tu baada ya dhiki kubwa kuanza?

      3 Yesu alitabiri matukio makubwa ambayo yangetukia “mara baada ya” kufyatuka kwa dhiki kubwa, matukio tunayongoja. Alisema kwamba ndipo “ishara ya Mwana wa binadamu” itatokea. Hili litaathiri kabisa “makabila yote ya dunia” ambayo “yatamwona Mwana wa binadamu akija juu ya mawingu ya mbinguni na nguvu na utukufu mkubwa.” Mwana wa binadamu ataandamana na “malaika zake.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki