Wimbo Na. 91
Baba Yangu, Mungu Wangu, Rafiki Yangu
Makala Iliyochapishwa
1. Maisha ni magumu.
Maumivu, huzuni tele.
Lakini ninajua,
“Maisha si bure.”
(KORASI)
Mungu ni mwadilifu,
Upendo wangu akumbuka.
Hataniacha kamwe;
Mungu wangu yuko nami.
Ndiye huniruzuku
na kunilinda sikuzote.
Baba yangu, Mungu wangu,
Na Rafiki.
2. Miaka imesonga;
Nguvu za ujanani sina.
Kwa imani naona,
Tumaini langu.
(KORASI)
Mungu ni mwadilifu,
Upendo wangu akumbuka.
Hataniacha kamwe;
Mungu wangu yuko nami.
Ndiye huniruzuku
na kunilinda sikuzote.
Baba yangu, Mungu wangu,
Na Rafiki.
(Ona pia Zab. 71:17, 18.)