Makala Iliyochapishwa
Wimbo Na. 49
Yehova Ni Kimbilio Letu
1. Yehova, kimbilio,
Ndiye twatumai.
Yeye ni ngome yetu;
Kwake twajificha.
Mungu atatuokoa,
Kamwe hatutaogopa.
Yehova, kimbilio,
Kwa waadilifu wote.
2. Maelfu waanguka,
Kando yako wewe.
Kati ya wa’minifu,
Kuna usalama.
Hutatetema kwa woga,
Hutapatwa na madhara.
Utaona mwenyewe,
Chini ya mbawa za Mungu.
3. Yehova yuko nawe,
Ili kukulinda.
Hataki ujikwae,
Wala kuogopa.
Mwana-simba hutahofu;
Swila utamukanyaga.
Yehova Kimbilio,
Atuongoza milele.
(Ona pia Zab. 97:10; 121:3, 5; Isa. 52:12.)