Wimbo Na. 83
Tunahitaji Sifa ya Kujizuia
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova kwa moyo twakupenda;
Hata hivyo sisi dhambi twatenda.
Ya kimwili tusikazie.
Ya kiroho tuzingatie.
2. Twajaribiwa naye Shetani.
Na sheria ya dhambi imo ndani.
Neno Lake linatulinda.
Tuna hakika tutashinda.
3. Kwa neno na tendo tumusifu,
Jina la Mungu tusilikashifu.
Mambo yote tuzingatie.
Sikuzote tujizuie.
(Ona pia 1 Kor. 9:25; Gal. 5:23; 2 Pet. 1:6.)