Wimbo Na. 45
Songa Mbele!
Makala Iliyochapishwa
1. Songa mbele, fikia ukomavu!
Mungu ataka tujipatie ujuzi.
Boresha ustadi wako shambani,
Mungu akubariki.
Sote twapaswa kuhubiri.
Yesu aliweka mufano.
Mwombe Mungu akupe nguvu zake,
Usimame imara.
2. Songa mbele, uwe na ujasiri!
Tangazia watu wote habari njema.
Tumusifu Yehova kwa furaha,
Tuhubiripo kote.
Adui wajapotutisha.
Usihofu; tangaza kote
Kwamba Ufalume unatawala.
Hubiri kwa bidii.
3. Songa mbele, wasaidie wapya,
Uwe na ustadi, kazi ni nyingi sana.
Roho ya Mungu na ikuchochee.
Nawe upate shangwe.
Upendezwe na watu wote.
Usikose kuwarudia.
Uwasaidie wasonge mbele.
Ukweli uangaze.
(Ona pia Flp. 1:27; 3:16; Ebr. 10:39.)