Wimbo 20
Imba Wimbo wa Uchangamshi wa Ufalme
1. Mwimbe wimbo wa Ufalme,
Watu duniani.
Imba kwa sauti kuu;
tangaza Ufalme.
Ni mizuri miguu ya
Waleta Injili!
Wanatangazia watu,
‘Mungu ni Mwokozi.’
2. Wimbo wetu wa Ufalme,
Twasifu Yehova.
Tunamwabudu kwa hofu
Twatakasa jina.
Sanamu za watu hoi
Haziwafaidi.
Tumwabudu Yehova tu;
Yeye ni wa kweli.
3. Twimbe wimbo wa Ufalme:
“Yehova Mufalme”
Kupitia kwa Mwanaye;
Mbingu zafurahi.
Yehova ndiye hakimu,
wa uadilifu,
Atawabariki wema
Wakiaminika.