Wimbo 126
Kutangaza Ukweli wa Ufalme
1. Tunauthamini Ufalme;
Unafurahisha wapole.
Twauhubiri bila hofu,
Kwani Ufalme watawala.
2. Tunaenda nyumba kwa nyumba;
Twataka kupanda ukweli.
Mungu yu pamoja na sisi.
Na tuwake kwa roho yake.
3. Tuna mugawo wa ajabu.
Tufanye yote tuwezayo,
Tufariji wenye taabu.
Ukweli utawapa raha.
4. Tuhubiri Ufalme kote
Yesu akawa mutawala.
Ufalme kufanya wajue
Jina lake Bwana Yehova.