Wimbo 197
Mwimbieni Yehova Wimbo Mtamu!
1. Twamwimbia Mungu wimbo,
Tukiwa na hekima.
Dunia sasa ni mali
Yake Yesu Mwanaye.
Tunaimba kwa ushindi.
Mungu ni mwema sana!
Tunasifu kwa sauti
Tukiimba pamoja.
Mataifa yataona
Yesu atawala.
Umeanza utawala.
Tujulishe hilo.
2. Ni wakati wa taabu,
Huzuni, shida pia;
Uharibifu ni mwingi.
Lakini utawala
Wa Mileani wa Kristo,
Ni karibu kabisa.
Paradiso irudishwe.
Wote washangilie.
Twangojea siku hiyo
Vyote viwe vipya.
Ili tuyaone hayo
Tuwe na adili.
3. Mungu afanya makubwa
Kwa hofu mataifa
Yaona ulinzi wake
Mungu kwa washuhuda.
Mungu Mwenye Enzi Kuu,
Atubariki sisi.
Na hivyo tunamwimbia.
Kutoka mioyoni.
Ndugu wapendwao sote
Tumwimbie Mungu
Juu ya kiti cha enzi
Afaa heshima.