Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sikukuu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Ni kanuni gani za Biblia zinazoonyesha maoni ya Wakristo kuhusu sherehe za kukumbuka matukio mbalimbali katika historia ya kisiasa ya taifa?

      Yoh. 18:36: “Yesu akajibu [gavana Mroma]: ‘Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu.’”

      Yoh. 15:19: “Kama [ninyi wafuasi wa Yesu] mngekuwa sehemu ya ulimwengu, ulimwengu ungependa kilicho chake. Sasa kwa sababu ninyi si sehemu ya ulimwengu, bali nimewachagua ninyi kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukia ninyi.”

      1 Yoh. 5:19: “Ulimwengu mzima unakaa katika nguvu za yule mwovu.” (Linganisha na Yohana 14:30; Ufunuo 13:1, 2; Danieli 2:44.)

      Sikukuu nyingine za sehemu mbalimbali na za kitaifa

      Kuna sikukuu nyingi. Zote haziwezi kuzungumziwa hapa. Lakini historia ambayo imetolewa, inaonyesha mambo tunayoweza kuzingatia kuhusiana na sikukuu yoyote, na kanuni za Biblia zilizozungumziwa zinatoa mwongozo wa kutosha kwa ajili ya wale wanaotamani kufanya mapenzi ya Yehova Mungu.

  • Sikukuu ya Kuzaliwa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Sikukuu ya Kuzaliwa

      Maana: Siku ya kuzaliwa kwa mtu au ukumbusho wa siku hiyo. Katika sehemu mbalimbali sikukuu ya kuzaliwa kwa mtu, hasa kule kwa mtoto, husherehekewa kwa kufanya karamu na kutolewa kwa zawadi. Hilo si zoea la Kibiblia.

      Je, Biblia inapotaja kuhusu sherehe za sikukuu ya kuzaliwa, inaonyesha kwamba zinafaa? Biblia inataja sherehe mbili tu za aina hiyo:

      Mwa. 40:20-22: “Basi siku ya tatu ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawafanyia karamu . . . Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji kwenye cheo chake cha kunywesha . . . Lakini akamtundika mkuu wa waokaji.”

      Mt. 14:6-10: “Sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode ilipokuwa ikisherehekewa binti ya Herodia alicheza dansi na kumpendeza sana Herode hivi kwamba akaahidi kwa kiapo kumpa chochote kile ambacho angeomba. Ndipo yeye, chini ya mwelekezo wa mama yake, akasema: ‘Nipe hapa juu ya sahani kichwa cha Yohana Mbatizaji.’ . . . Akatuma watu wakamkate Yohana kichwa huko gerezani.”

      Kila jambo katika Biblia limo humo kwa sababu fulani. (2 Tim. 3:16, 17) Mashahidi wa Yehova huepuka sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwa kuwa wanafahamu kwamba Neno la Mungu hutaja mambo yasiyofaa kuhusiana na sikukuu hizo.

      Wakristo wa kwanza na Wayahudi wa nyakati za Biblia walionaje sherehe za sikukuu ya kuzaliwa?

      “Kwa ujumla Wakristo wa kipindi hicho hawakuwa wakisherehekea sikukuu ya kuzaliwa.”—The History of the Christian Religion and Church, During the Three First Centuries (New York, 1848), Augustus Neander (kilichotafsiriwa na Henry John Rose), uku. 190.

      “Waebrania wa baadaye waliziona sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kuwa sehemu ya ibada ya sanamu, jambo ambalo lilithibitishwa kabisa na yale waliyoona katika sherehe zilizopendwa ambazo zilihusianishwa na sikukuu hizo.”—The Imperial Bible-Dictionary (London, 1874), kilichohaririwa na Patrick Fairbairn, Buku la 1, uku. 225.

      Desturi zinazopendwa na wengi zinazohusiana na sherehe za sikukuu ya kuzaliwa zilitoka wapi?

      “Desturi mbalimbali ambazo watu leo hutumia kusherehekea sikukuu zao za kuzaliwa ni za tangu zamani. Zilitokana na uchawi na dini. Desturi za kutoa pongezi, zawadi na kusherehekea—pamoja na mishumaa iliyowashwa—nyakati za kale zilikusudiwa kumlinda anayesherehekea sikukuu ya kuzaliwa asiumizwe na roho waovu na kuhakikisha usalama wake mwaka ujao. . . . Kufikia karne ya nne Wakristo walikataa kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa kuwa ni desturi ya kipagani.”—Schwäbische Zeitung (nyongeza ya gazeti Zeit und Welt), Aprili 3/4, 1981, uku. 4.

      “Wagiriki waliamini kwamba kila mtu alikuwa na roho au daemon mwenye kumlinda aliyekuwapo wakati wa kuzaliwa kwake na kumlinda maishani. Roho huyo alikuwa na uhusiano wa kifumbo pamoja na mungu ambaye mtu huyo alizaliwa katika sikukuu yake ya kuzaliwa. Waroma pia waliunga mkono wazo hilo. . . . Wazo hilo liliendelezwa katika imani ya binadamu na linaonekana katika malaika mlinzi, mama wa ubatizo na mtakatifu mlezi. . . . Desturi ya kuwasha mishumaa juu ya keki ilianzishwa na Wagiriki. . . . Keki za asali za mviringo kama mwezi na zenye kuwashwa kwa mishumaa midogo ziliwekwa juu ya madhabahu za hekalu la [Artemi]. . . . Mishumaa ya sikukuu za kuzaliwa, katika hekaya za watu, ina uwezo wa pekee wa kuwapa watu yale wanayotamani. . . . Mishumaa midogo iliyowashwa na mioto ya dhabihu imekuwa na maana ya pekee ya kifumbo tangu mwanadamu alipoisimamishia miungu yake madhabahu mara ya kwanza. Kwa hiyo mishumaa ya sikukuu ya kuzaliwa ni heshima na sifa kwa mtoto wa sikukuu hiyo ya kuzaliwa na huleta bahati njema. . . . Salamu za sikukuu ya kuzaliwa na heri njema ni sehemu muhimu ya sikukuu hiyo. . . . Mwanzoni wazo hilo lilianzia katika uchawi. . . . Salamu za sikukuu ya kuzaliwa zinaweza kuleta mema au mabaya kwa sababu mtu huwa karibu zaidi na ulimwengu wa roho katika siku hiyo.”—The Lore of Birthdays (New York, 1952), Ralph na Adelin Linton, uku. 8, 18-20.

      Si vibaya familia na marafiki kukusanyika ili kula, kunywa, na kufurahi

      Mhu. 3:12, 13: “Hakuna jambo lingine bora kwao kuliko mtu kufurahi na kufanya mema maishani mwake; na pia kwamba kila mtu ale, naam, anywe na kuona mema kwa ajili ya kazi yake yote iliyo ngumu. Hiyo ndiyo zawadi ya Mungu.”

      Ona pia 1 Wakorintho 10:31.

  • Siku za Mwisho
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Siku za Mwisho

      Maana: Biblia hutumia maneno haya “siku za mwisho” kurejezea kipindi cha kumalizia kinachoelekeza kwenye kutekelezwa kwa hukumu iliyowekwa na Mungu. Huo ndio utakaokuwa mwisho wa

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki