Wimbo 125
“Yehova Yuko Upande Wangu”
1. Moyo wangu kwa Yehova
Ni imara, thabiti.
Natamani njia zake
Nizifuate sana.
Kwenye njia ya uzima
Huenda kuwe shida,
Mungu ni upande wangu.
Upendo wake mwema!
(Korasi)
2. Najua imani yangu
Itapata jaribu.
Na jeshi la Ibilisi
Kama nyuki wakali.
Naweza kuwafukuza,
Kwa kinga ya kimungu.
Mungu awapenda watu
Wa lile jina lake.
(Korasi)
3. Yehova amepanua
Mipaka ya taifa.
Wengi wanamiminika
Wafanya penzi lake.
Na anawategemeza;
Anapendezwa nao.
Nami niwe na bidii
Inijae kabisa.
(KORASI)
Yehova upande wangu;
Nitamusifu Yah daima.