Wimbo 144
Ni Lazima Tuwe na Imani!
1. Mungu akawa anena zamani
Akitumia manabii chini.
Mwisho Mwana wa mbingu katumia;
Tutasalimika tukisikia.
(Korasi)
2. Uhuru wa kusema tusitupe,
Kwa huo tuhubiri, tufundishe.
Kwa imani tukifuata Bwana,
Yehova kututhawabisha sana.
(Korasi)
3. Haturudi nyuma tuharibiwe.
Twatumaini tutumiwe naye.
Hata wawe wengi adui zetu,
Yehova bado tutamwamini tu.
(KORASI)
Imani ni ya lazima kwetu sisi
Ili vita ya Mungu tupone sisi.
Je! ni ya matendo imani yetu?
Ndiyo iokoayo nafusi.