Wimbo 219
Kiti cha Ufalme Mbinguni cha Yehova
(Ufunuo 4)
1. Ewe Yehova, ndiwe Mungu.
Utukufu wa kiti chako mwingi.
Upinde-mvua waonyesha.
U Mungu wa amani, Mutulivu.
2. “Wazee ishirini na nne,”
Ni wafalme makuhani na Kristo!
Viumbe wanne wakusifu:
U haki, na hekima—Na upendo.
3. Watokeza radi, umeme.
Wote wausikilize ukweli.
Bahari-kioo, usafi.
Na tuoge katika Neno lako.
4. Njozi hii inatufanya
Tukusifu Mungu Mutakatifu.
Yesu Mwokozi atawala.
Na kupitia kwake Twakujia.