Wimbo 120
Uwe Imara Kama Ruthu
1. Japo ni huzuni Naomi,
Ahimiza Ruthu aende.
Sitarudi Moabu hasha,
Sababu apenda Naomi.
2. ’Hasha sitakuacha kamwe.
Uwapo nami ni papo tu.
Ulalapo, nami ni papo,
Ufapo, nife papo hapo.
3. ’Watu wako ni watu wangu,
Mungu wako, milele wangu.
Na azidishe Mungu wetu
Kitutenganishe kifo tu.
4. Lo! imani, pendo la Ruthu,
Ni kielelezo bora, we!
Hata sisi tuwe imara.
Tuwe na Mungu kwa imara.