Wimbo 143
Jipange Upande wa Yehova!
1. Kwanza tulivurugwa moyoni,
Tukanyweshwa uwongo wa dini;
Tulipendezwa ajabu gani
Na Ufalme mwanzoni (mwanzoni).
(Korasi)
2. Tutumikie Mungu kwa moyo,
Kweli ya Mungu na tueneze.
Ndugu zetu tuwasaidie.
Jina lake wasifu (wasifu).
(Korasi)
3. Ibilisi hatutamwogopa
Yehova Mungu ‘tatuokoa.
Japo wengi, sisi ni wachache,
Mungu ni nguvu yetu (ni yetu).
(KORASI)
Jipange naye Yah;
Mupende yeye.
Hakuachi kamwe;
Enda nuruni.
Habari za mema
Sema tu, sema.
Ufalme wa Yesu
Kuongezeka.