Wimbo 191
Ufanye Ukweli Uwe Mali Yako Mwenyewe
1. Maisha Mema ni njia ya ukweli.
Ndiyo njia bora sana.
Na Yesu Kristo katufunza kutoa,
Na furaha ienee.
Ukweli shika.
Imani iwe wazi.
Kupitia mwenendo wako
Ukweli uwe mali yako.
2. Tanguliza Yah na kumusifu yeye,
Uepuke ulimwengu.
Inashangaza wasio na imani
Kushika njia ya Mungu.
Ukweli shika.
Epuka ulimwengu.
Karibia Yehova Mungu,
Ukweli uwe mali yako.
3. Shetani yeye ni mudanganyi sana,
Bali mupinge kabisa.
Imani ngao Itakulinda wewe
Ukinge mashambulio.
Ukweli shika.
Hila zake twajua.
Vaa silaha zake Mungu,
Ukweli uwe mali yako.
4. Mwili dhaifu na moyo wadanganya.
Washindana na udhambi.
Uwe hakika unaweza kushinda,
Maana Mungu Rafiki.
Ukweli shika.
Ziache njia mbaya.
Ukiuweza mwili wako,
Ukweli uwe mali yako.