Wimbo 18
Bariki Udugu wa Kikristo Wetu
1. Yesu kwa fadhili
Na saburi pia,
Wafwasi kafunza
Kawapa amani.
Alionyesha upendo,
Kapenda adili,
Unyenyekevu kafunza,
Na kuaminika.
(Korasi)
2. Tu wenye furaha
Tukitii Mungu!
Wapole baraka,
Wanashika Neno!
Wafuasi wake Yesu
Kapenda udugu,
Wakatangaza Ufalme
Wakapenda ndugu.
(Korasi)
3. Hubiri wapenda
Ukweli Ufalme,
Uwasaidie
Wachague Mungu.
Watafute Mungu leo,
Apatikanapo,
Wajiunge na udugu,
Wafurahi sana.
(KORASI)
Yehova twasifu;
Kweli wewe mwema.
E Yehova, Baba yetu,
Bariki udugu wetu.