Wimbo 98
Kuishindania Imani
(Yuda 3)
1. Yesu alivyotabiri,
Uovu umezidi.
Pendo la wengi baridi;
Imani haba sana.
Tuwe tukishindania
Imani lilipata
Kundi lile la Kikristo.
Neno liliamini.
2. Asidhoofishe hasha
Ibilisi imani;
Kwa funzo, sala, huduma
Tuishike imani.
Tukiwa twashindania
Tusishuku, kuhofu,
Sisi tutiane nguvu,
Hivyo wote wadumu.
3. Itumie kila njia,
Shindania imani.
Shuhudia kijasiri
Hata mufumo wishe.
Kwa kutetewa Yah ’ovu
Hautakuwapo la,
Wokovu utatujia,
Chini ya Theokrasi.