Wimbo 85
Yehova Ni Kimbilio Letu
1. Yah Kimbilio letu,
Tumaini letu.
Uvuli, ficho letu;
Na tukae humo.
Yeye atakuokoa
Na tauni, wategaji.
Yehova ni ngome na
Salama ya wa haki.
2. Japoanguka elfu,
Kwa upande wako.
Elfu kumi kulia;
Hutapata dhara.
Hutatetema kwa hofu,
Kana dhara lakujia.
Utaona kwa macho,
’Uwe mbawani mwake.
3. Hutapatwa na pigo,
Wala na musiba.
Mungu kwa malaika
’Takulinda wewe.
Mwana-simba hutahofu;
Fira utamukanyaga.
Hutakwazwa na jiwe
Umutumikiapo.
4. Kwa hiyo musifu Yah;
Haki zitangaze.
’Julishe njema zake,
Pasipo lawama.
’Jitoe nafusi yote;
Tujue wokovu wake.
Yah Kimbilio letu,
Ngome ni jina lake.