Wimbo 113
Sisi Ni Mashahidi wa Yehova!
1. Watu hufanya mungu,
Wa miti na wa mawe.
Nao hawajui
Mungu wa kweli.
Miungu mingineyo,
Haioni yajayo.
Hiyo haina mashahidi,
Kwani haina uungu.
(Korasi)
2. ‘Mu mashahidi wangu,’
Musihofu miungu.
Yehova ni mimi,
Na Mwenye Enzi.
Mimi niliwaponya
Miungu hamujui.
Litangazeni jina langu;
Ninyi Mashahidi wangu.’
(Korasi)
3. Kushuhudia jina
Huondoa lawama.
Bali kwa waovu
Onyo twatoa.
Warudiao Mungu
Awasamehe Mungu.
Hivyo twatumaini sisi
Uzima usiokoma.
(KORASI)
Sisi ni Mashahidi
Wa Yehova; twasema.
Mungu wetu wa unabii;
Wa kweli unabii.