Wimbo 112
Ndipo Watajua
1. Adui ’kasuta jina lako,
Wakanajisi patakatifu.
Uadilifu utajulishwa;
Utawala wa Shetani wishe.
(Korasi)
2. Shetani ’kapinga uwezako.
Karibuni utauonyesha.
Jeshi lake litaharibiwa,
Penye vita ya Har–Magedoni.
(Korasi)
3. Mioyo isiyo na huruma
Yataka kuwatawala watu.
Mukono wako ‘tavunja kongwa.
Wachokozi wako watoweke.
(KORASI)
Ndipo wajue wewe ni Yehova;
Wajue njia zako za haki.
Watajua uumbajini mwote,
Makusudi yako utafanya.