Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Majaliwa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • “Katika Babilonia na vilevile katika Ashuru, ufalme uliotokana moja kwa moja na utamaduni wa Babiloni . . . unajimu uko katika dini rasmi ukiwa mojawapo ya njia kuu mbili zilizotumiwa na makuhani . . . katika kutambua mapenzi na kusudi la miungu, njia nyingine ni kupitia uchunguzi wa ini la mnyama wa dhabihu. . . . Miendo ya jua, mwezi na sayari tano ilionwa kuwa inawakilisha utendaji wa miungu mitano inayohusika, pamoja na Sini, ambaye ni mungu-mwezi, na Shamashi, ambaye ni mungu-jua, katika kutayarisha matukio duniani.”—Encyclopædia Britannica (1911), Buku la Pili, uku. 796.

      Muumba wa wanadamu analionaje zoea hilo?

      Kum. 18:10-12: “Asipatikane ndani yako yeyote . . . anayefanya uaguzi, mwenye kufanya uchawi au yeyote anayetafuta ishara za bahati au mlozi . . . Kwa maana kila mtu anayefanya mambo hayo ni chukizo kwa Yehova.”

      Aliwaambia Wababiloni hivi: “Na wasimame, sasa, na kukuokoa, wanaoabudu mbingu, watazamaji wa nyota, ambao kwenye miezi mipya wanajulisha habari za mambo yatakayokuja juu yako. Tazama! Wamekuwa kama majani makavu. . . . Wale ambao umefanya kazi pamoja nao kama wachawi wako tangu ujana wako. Kwa kweli watatanga-tanga, kila mmoja kwenda katika eneo lake mwenyewe. Hakutakuwa na yeyote wa kukuokoa.”—Isa. 47:13-15.

  • Manabii wa Uwongo
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Manabii wa Uwongo

      Maana: Mtu mmoja-mmoja na mashirika yanayotangaza ujumbe ambao wanadai hautoki kwa wanadamu, lakini ujumbe huo hautoki kwa Mungu wa kweli na haupatani na mapenzi yake yaliyofunuliwa.

      Manabii wa kweli na wa uwongo wanaweza kutambuliwaje?

      Manabii wa kweli hutangaza imani yao katika Yesu, lakini mengi yanahitajiwa kuliko kudai kuhubiri katika jina lake

      1 Yoh. 4:1-3: “Yajaribuni maneno yaliyoongozwa na roho ili kuona kama yanatokana na Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uwongo wameingia ulimwenguni. Mnalijua neno lililoongozwa na roho kutoka kwa Mungu kwa njia hii: Kila neno lililoongozwa na roho linalomkiri Yesu Kristo kuwa alikuja katika mwili hutokana na Mungu, lakini kila neno lililoongozwa na roho ambalo halimkiri Yesu halitokani na Mungu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki