Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 11/15 uku. 32
  • Una Jina la Aina Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Una Jina la Aina Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 11/15 uku. 32

Una Jina la Aina Gani?

KATIKA Biblia, nyakati nyingine neno “jina” hurejezea sifa ya mtu. Kwa kielelezo, Mfalme Solomoni mwenye hekima aliandika hivi: “Heri sifa njema [“jina,” NW] kuliko marhamu nzuri; na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.” (Mhubiri 7:1; linganisha Mithali 22:1.) Kulingana na maneno ya Solomoni, mtu hazaliwi akiwa na jina jema. Badala yake, maishani mwake ndipo apatapo sifa yenye maana halisi. Jina lake humhusianisha na sifa zake binafsi, awe mkarimu au mwenye ubinafsi, mwenye huruma au asiye na huruma, mnyenyekevu au mwenye kiburi, hata mwadilifu au mwovu.

Mfikirie Daudi. Alipokuwa mfalme, alijithibitisha kuwa mwenye nguvu na asiyeyumbayumba. Wakati huohuo, Daudi alikiri kwa unyenyekevu makosa yake na kutubu dhambi zake nzito. Akiwa na sababu nzuri, Nabii wa Yehova alionyesha kwamba Daudi alikuwa “mtu aupendezaye moyo” wa Mungu. (1 Samweli 13:14) Tayari Daudi mchanga alikuwa na jina jema pamoja na Mungu.

Tofauti naye, Mfalme Myudea Yehoramu alijifanyia jina baya. Aliwageuza raia wake wasimwabudu Yehova na hata akaagiza ndugu zake sita na baadhi ya wakuu wa Yuda wauawe. Hatimaye, Yehova alimpiga Yehoramu kwa ugonjwa wenye maumivu uliomuua. Biblia yasema kwamba Yehoramu ‘alifariki bila kutamaniwa,’ au kama vile Biblia Habari Njema isemavyo, “alipofariki, hakuna mtu yeyote aliyemsikitikia.”—2 Mambo ya Nyakati 21:20.

Maisha ya Daudi na ya Yehoramu huonyesha ukweli wa mithali hii ya Biblia: “Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; bali jina la mtu mwovu litaoza.” (Mithali 10:7) Kwa hiyo kila mmoja wetu apaswa kufikiria kwa makini swali hili, ‘Najifanyia jina la aina gani pamoja na Mungu na wanadamu wenzangu?’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki