Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hatutakana Imani Yetu
    2016 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • INDONESIA

      Hatutakana Imani Yetu

      Daniel Lokollo

      • ALIZALIWA 1965

      • ALIBATIZWA 1986

      • HISTORIA FUPI Painia wa pekee aliyesimama imara wakati wa mnyanyaso.

      Daniel Lokollo

      MNAMO Aprili 14, 1989, Nilikuwa naongoza mkutano katika mji wa Maumere, katika Kisiwa cha Flores, maofisa wa serikali walipoingia kwa nguvu na kunikamata pamoja na ndugu wengine watatu.

      Walinzi wa gereza walitulazimisha kusalimu bendera. Tulipokataa, walituchapa, kutupiga mateke na kutuweka kwenye jua kali kwa siku tano. Usiku tulitetemeka kwa sababu ya kulala kwenye sakafu baridi na chafu ya seli ndogo, tukiwa tumechoka na kuhisi maumivu makali ya majeraha. Mara kwa mara mlinzi wa gereza alisisitiza kwamba tukane imani yetu, lakini tulijibu, “Hata ikiwa tutakufa, hatutasalimu bendera.” Kama Wakristo wengine waliotutangulia, tuliona ni pendeleo “kuteseka kwa ajili ya uadilifu.”—1 Pet. 3:14

  • Kutii Mwongozo Kulitusaidia Kuokoka!
    2016 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • INDONESIA

      Kutii Mwongozo Kulitusaidia Kuokoka!

      Blasius da Gomes

      • ALIZALIWA 1963

      • ALIBATIZWA 1995

      • HISTORIA FUPI Mzee aliyechunga kundi kwa upendo wakati wa mgogoro wa kidini huko Ambon, ambacho ni sehemu ya Visiwa vya Maluku.

      Blasius da Gomes

      MNAMO Januari 19, 1999, mgogoro uliongezeka kati ya Waislamu na Wakristo na ulisababisha vurugu kubwa kilomita tatu kutoka nyumbani kwangu. Hali ilikuwa mbaya sana.a

      Baada ya kuhakikisha kwamba familia yangu iko salama, niliwapigia simu wahubiri wengine ili kujua hali zao. Niliwasihi watulie na wasiende kwenye maeneo hatari. Baadaye, wazee waliwatembelea ili kuwaimarisha kiroho na kuwatia moyo wafanye mikutano katika vikundi vidogo.

      Ofisi ya tawi ilipendekeza kwamba wahubiri wote wanaoishi katika maeneo hatari waondoke, hivyo tukazijulisha familia kadhaa kuhusiana na mwongozo huo. Ndugu mmoja aliyepuuza maagizo hayo aliuawa na kundi la wahalifu. Hata hivyo, waliofuata mwongozo wa ofisi ya tawi waliokoka.

      a Mgogoro huo ulienea katika jimbo lote la Maluku kwa zaidi ya miaka miwili na maelfu ya watu walikimbia nyumba zao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki