Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb18 Februari uku. 7
  • Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma​—Kutumia Maswali Vizuri

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma​—Kutumia Maswali Vizuri
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Habari Zinazolingana
  • Kutumia Maswali Vizuri
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Timiza Jukumu Lako Ukiwa Mweneza-Injili
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Kutumia Maswali
    Boresha Uwezo Wako wa Kusoma na Kufundisha
  • Fundisha kwa Ufahamu Wenye Kina na Ushawishi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
mwb18 Februari uku. 7

MAISHA YA MKRISTO

Kuboresha Ustadi Wetu katika Huduma​—Kutumia Maswali Vizuri

KWA NINI NI MUHIMU: Ikiwa “mawazo yaliyo moyoni mwa mtu ni kama maji yenye kina,” basi maswali ni kama ndoo inayotumiwa kuyateka. (Met 20:5) Maswali yanatusaidia kuwahusisha wasikilizaji. Majibu ya maswali yaliyoteuliwa vizuri yanatusaidia kupata habari muhimu. Yesu alitumia maswali kwa njia inayofaa. Tunaweza kumwigaje?

Yesu amwuliza mwanafunzi wake swali

JINSI YA KUFANYA HIVYO:

  • Uliza maswali ya maoni. Yesu aliuliza mfululizo wa maswali ili kujua maoni ya wanafunzi wake. (Mt 16:13-16; be 238 ¶3-5) Unaweza kuuliza maswali gani ya maoni?

  • Uliza maswali ya kumsaidia mtu kufikiri. Ili kurekebisha kufikiri kwa Petro, Yesu aliuliza maswali na kumweleza mambo kadhaa ambayo yangemsaidia Petro kufikia mkataa unaofaa. (Mt 17:24-26) Unaweza kuuliza maswali gani yatakayomsaidia mtu kufikiri na kufikia mkataa unaofaa?

  • Mpongeze msikilizaji wako. Baada ya mwandishi fulani “[kujibu] kwa kutumia akili,” Yesu alimpongeza. (Mk 12:34) Unaweza kumpongeza jinsi gani mtu anayejibu swali ulilouliza?

Onyesha heshima. Hatuna mamlaka kama ya Yesu. Kwa hiyo, ni lazima tuwaonyeshe heshima waliozeeka, watu tusiowajua, na wengine walio na mamlaka.—1Pe 2:17.

TAZAMENI SEHEMU YA KWANZA YA VIDEO FANYA KAZI AMBAYO YESU ALIFANYA—FUNDISHA, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Ingawa habari zilizozungumziwa ni sahihi, kwa nini huo ni mfano mbaya wa ufundishaji?

  • Kwa nini hatupaswi kueleza tu habari?

TAZAMENI SEHEMU YA PILI YA VIDEO, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Ndugu huyo alitumiaje maswali kwa njia yenye matokeo?

  • Ni mambo gani mengine tunayoweza kuiga kutokana na ufundishaji wake?

Mwanamume analemewa/anahangaika anapofundishwa vibaya; mtu anaona kweli waziwazi anapofundishwa vizuri

Ufundishaji wetu utawaathiri wengine jinsi gani? (Lu 24:32)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki