Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr21 Novemba kur. 1-4
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2021
  • Vichwa vidogo
  • NOVEMBA 1-7
  • NOVEMBA 8-14
  • NOVEMBA 15-21
  • DESEMBA 13-19
  • DESEMBA 20-26
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2021
mwbr21 Novemba kur. 1-4

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

NOVEMBA 1-7

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YOSHUA 18-19

“Yehova Agawa Nchi kwa Hekima”

it-1 359 ¶1

Mpaka

Hivyo, inaonekana kwamba mgawanyo wa ardhi kati ya makabila ulitegemea mambo mawili: matokeo baada ya kupiga kura, na ukubwa wa kabila. Huenda kura ilionyesha mahali ambapo kila kabila lingepewa urithi wa ardhi, na hivyo kuonyesha upande ambao urithi wao ungekuwa katika nchi, kwa mfano, Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi, kando ya bahari, au eneo la milimani. Uamuzi wa kura ulitoka kwa Yehova na hilo lingezuia makabila yasioneane wivu au kubishana. (Met 16:33) Kwa njia hiyo pia, Mungu angeongoza mambo ili hali za kila kabila zipatane na unabii unaopatikana kwenye Mwanzo 49:1-33 ambao mzee wa ukoo Yakobo alitoa alipokuwa akikaribia kufa.

it-1 1200 ¶1

Urithi

Ardhi zilizorithiwa. Yehova ndiye aliyewapa Waisraeli urithi na kumwonyesha Musa mipaka ya nchi hiyo. (Hes 34:1-12; Yos 1:4) Musa ndiye aliyewagawia wana wa Gadi, wana wa Rubeni na nusu ya kabila la Manase ardhi yao. (Hes 32:33; Yos 14:3) Makabila yale mengine yalipewa urithi wao kwa kutegemea kura kwa mwongozo wa Yoshua na Eleazari. (Yos 14:1, 2) Kupatana na unabii wa Yakobo kwenye Mwanzo 49:5, 7, Simeoni na Lawi hawakupaswa kupewa ardhi kuwa urithi wao. Maeneo ambayo kabila la Simeoni lilipewa (pamoja na majiji yaliyozungukwa) yalikuwa katikati ya urithi wa Yuda (Yos 19:1-9), na kabila la Lawi lilipewa majiji 48 katika eneo lote la Israeli. Kwa kuwa Walawi waliwekwa rasmi katika utumishi wa pekee kwenye madhabahu, Yehova alisemwa kuwa urithi wao. Walipokea sehemu ya kumi ikiwa kama posho au urithi wao kwa sababu ya utumishi waliofanya. (Hes 18:20, 21; 35:6, 7) Familia zilipewa migawo ndani ya eneo la kabila lao. Kadiri ambavyo familia zingeongezeka na wana wangepewa urithi, ardhi ingeendelea kugawanywa katika mafungu madogo-madogo zaidi.

it-1 359 ¶2

Mpaka

Baada ya kupiga kura kufahamu eneo la kijiografia la kila kabila, kungekuwa na uhitaji wa kutambua ukubwa wa eneo lake kwa msingi wa sababu ya pili: idadi ya watu katika kabila hilo. “Mtaigawanya nchi hiyo kwa kura na kuimiliki kulingana na familia zenu. Kundi kubwa litapokea urithi mkubwa zaidi na kikundi kidogo kitapokea urithi mdogo. Kila mtu atapokea urithi wake mahali ambapo kura yake itaangukia.” (Hes 33:54) Uamuzi wa kura kuhusu upande wa kijiografia haungebadilika, hata hivyo, badiliko lingeweza kufanywa kuhusiana na ukubwa wa urithi. Kwa hiyo, eneo la Yuda lilipoonekana kuwa kubwa sana, lilipunguzwa kwa kuwagawia watu wa kabila la Simeoni maeneo ndani ya ardhi hiyo.​—Yos 19:9.

Hazina za Kiroho

it-1 359 ¶5

Mpaka

Simulizi kuhusu kugawanya kwa ardhi magharibi mwa Yordani linaonyesha kwamba kwanza kura ilipigwa kwa ajili ya makabila ya Yuda (Yos 15:1-63), Yosefu (Efraimu) (Yos 16:1-10), na nusu ya kabila la Manase ambao wangekaa magharibi mwa Yordani (Yos 17:1-13), na mipaka na majiji yao ikahesabiwa. Baada ya hapo, inaonekana shughuli ya kugawa ardhi ilisitishwa kwa muda kwa kuwa inaonekana kwamba kambi ya Israeli ilihamishwa kutoka Gilgali kwenda Shilo. (Yos 14:6; 18:1) Muda uliopita hautajwi lakini hatimaye Yoshua aliyakemea makabila saba kwa mtazamo wao wa kukawia kuimiliki nchi. (Yos 18:2, 3) Maelezo mbalimbali yametolewa kuhusu sababu ya mtazamo huo wa makabila hayo saba. Wasomi fulani wanasema kwamba huenda makabila hayo yalihisi hakuna haraka ya kumiliki sehemu iliyobaki ya ardhi kwa sababu ya nyara nyingi walizokuwa wamekusanya wakati wa vita na kwa sababu walihisi hakukuwa na tisho la kushambuliwa na Wakanaani. Huenda pia uwezekano wa kukabiliana na maadui wachache wenye nguvu waliokuwa wamesalia uliwafanya wakawie kumiliki ardhi iliyosalia. (Yos 13:1-7) Pia, huenda walijua mengi zaidi kuhusu sehemu ya Nchi ya Ahadi iliyokuwa imegawanywa kuliko sehemu waliyopaswa kumiliki.

NOVEMBA 8-14

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YOSHUA 20-22

Hazina za Kiroho

it-1 402 ¶3

Kanaani

Ingawa Wakanaani wengi sana hawakufa wakati wa vita na hawakukubali kufanywa watumwa, bado inaweza kusemwa kwamba “Yehova [aliwapa] Waisraeli nchi yote ambayo aliapa kwamba angewapa mababu zao,” kwamba aliwapa “amani katika nchi yote,” na kwamba “hakuna ahadi hata moja iliyokosa kutimia kati ya ahadi zote nzuri ambazo Yehova aliwaahidi Waisraeli; zote zilitimia.” (Yos 21:43-45) Maadui wote waliozunguka Israeli waliogopa sana hivi kwamba hawangeweza kuwatisha. Mungu alikuwa amesema mapema kwamba angewafukuza Wakanaani “hatua kwa hatua” ili wanyama wa mwituni wasiongezeke katika nchi iliyoachwa ukiwa ghafla. (Kut 23:29, 30; Kum 7:22) Licha ya kwamba Wakanaani walikuwa na vifaa bora zaidi vya vita, kutia ndani magari ya vita yenye miundu ya chuma, haingeweza kusemwa kwamba Yehova ameshindwa kutimiza ahadi yake kwa sababu tu Waisraeli hawakuweza kumiliki maeneo fulani. (Yos 17:16-18; Amu 4:13) Badala yake, maandiko yanaonyesha kwamba pindi chache ambazo Waisraeli walishindwa na maadui wao ilikuwa kwa sababu ya ukosefu wao wa uaminifu.​—Hes 14:44, 45; Yos 7:1-12.

NOVEMBA 15-21

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YOSHUA 23-24

“Yoshua Alihimiza Taifa kwa Mara ya Mwisho”

it-1 75

Mapatano

Hali tofauti ilijitokeza taifa la Israeli lilipoingia Kanaani, ile Nchi ya Ahadi. Mungu Mwenye Enzi Kuu alikuwa amewapa Waisraeli haki ya kumiliki nchi hiyo ili kutimiza ahadi aliyowapa mababu zao. Hivyo, hawakuwa wakiingia wakiwa wageni, kwa hiyo, Yehova aliwaonya dhidi ya kufanya mapatano na mataifa ya kipagani ya nchi hiyo. (Kut 23:31-33; 34:11-16) Walipaswa kutii masharti na sheria za Mungu peke yake, na si zile za mataifa waliyokuwa wakiyafukuza. (Law 18:3, 4; 20:22-24) Walionywa kihususa dhidi ya kufanya mapatano ya ndoa na mataifa hayo. Mapatano ya aina hiyo yangewafanya wawe na uhusiano wa karibu na wake wa kipagani, watu wao wa ukoo, na wangejihusisha katika mazoea na desturi za dini za uwongo. Hilo lingewafanya wawe waasi-imani na lingekuwa mtego kwao.​—Kum 7:2-4; Kut 34:16; Yos 23:12, 13.

DESEMBA 13-19

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | WAAMUZI 8-9

Hazina za Kiroho

it-1 753 ¶1

Efodi, Sehemu ya 1

Licha ya nia nzuri ya Gideoni ya kukumbuka ushindi ambao Yehova alikuwa amewapa Waisraeli na kumtukuza Mungu, efodi hiyo “ikawa mtego kwa Gideoni na kwa nyumba yake,” kwa sababu Waisraeli walifanya ukahaba wa kiroho kwa kuiabudu. (Amu 8:27) Hata hivyo, Biblia haisemi kwamba Gideoni aliiabudu. Badala yake mtume Paulo alimtaja kihususa akiwa miongoni mwa ‘wingu kubwa’ la mashahidi waaminifu wa Yehova walioishi kabla ya kutaniko la Kikristo kuanzishwa.​—Ebr 11:32; 12:1.

DESEMBA 20-26

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | WAAMUZI 10-12

“Yeftha—Mwanamume wa Kiroho”

it-2 27 ¶2

Yeftha

Yeftha, mwanamume jasiri, hakupoteza muda wa kutenda kama kiongozi mwenye bidii. Alimtumia Mfalme wa Amoni ujumbe, akisema kwamba Waamoni walikuwa wamewachokoza Waisraeli kwa kuvamia nchi yao. Mfalme huyo akajibu kwa kusema kwamba Waisraeli walikuwa wamechukua nchi hiyo kutoka kwa Waamoni. (Amu 11:12, 13) Katika pindi hiyo Yeftha alionyesha kwamba hakuwa tu mpiganaji mkatili asiye na ustaarabu, bali alikuwa mwanafunzi wa historia na hasa wa jinsi Mungu alivyoshughulika na watu wake. Alipinga madai ya Mfalme wa Waamoni kwa kusema kwamba (1) Waisraeli hawakuwachokoza Waamoni, Wamoabu, au Waedomu (Amu 11:14-18; Kum 2:9, 19, 37; 2Nya 20:10, 11); (2) ardhi hiyo haikuwa ya Waamoni wakati ambapo Waisraeli waliingia katika nchi hiyo, kwa sababu ilikuwa mikononi mwa Waamori walioishi nchini Kanaani na Mungu aliwasaidia Waisraeli kumshinda Mfalme Sihoni na kuwapa ardhi yake; (3) Waamoni hawakuwa wamedai ardhi hiyo kwa miaka 300 ambayo Waisraeli waliimiliki; hivyo, walikuwa na msingi gani wa kufanya hivyo sasa?​—Amu 11:19-27.

it-2 27 ¶3

Yeftha

Yeftha alionyesha kiini cha tatizo aliposema kwamba tendo hilo lilihusu ibada. Alisema kwamba Yehova Mungu aliwapa Waisraeli nchi hiyo na kusema kwamba hawangewapa watu walioabudu mungu wa uwongo sehemu yoyote ya nchi hiyo. Alimwita Kemoshi kuwa mungu wa Waamoni. Watu fulani wamesema kwamba hilo lilikuwa kosa. Ingawa mungu wa Waamoni alikuwa Milkomu, na ingawa Kemoshi alikuwa mungu wa Wamoabu, mataifa hayo yaliyokuwa na uhusiano wa kifamilia yaliabudu miungu mingi. Hata Sulemani alikosea kwa kuingiza ibada ya Kemoshi nchini Israeli kwa sababu ya wake zake wa kigeni. (Amu 11:24; 1Fa 11:1, 7, 8, 33; 2Fa 23:13) Isitoshe, wasomi fulani wanasema kwamba jina “Kemoshi” linaweza kumaanisha “Anayetiisha, Mshindi.” (Ona kitabu Gesenius’s Hebrew and Chaldee Lexicon, kilichotafsiriwa na S. Tregelles, 1901, uku. 401.) Huenda Yeftha alitaja jina la mungu huyo kwa kuwa ndiye aliyesifiwa na Waamoni kuwa aliwasaidia ‘kuwatiisha’ au ‘kuwashinda’ wengine na kuwapa ardhi.

Hazina za Kiroho

it-2 26

Yeftha

Yeftha Hakuwa Mwanaharamu. Mama ya Yeftha alikuwa “kahaba.” Hata hivyo, hilo halimaanishi kwamba Yeftha alizaliwa kutokana na ukahaba au kwamba alikuwa mwanaharamu. Hapo awali mama yake alikuwa kahaba kabla ya kuolewa akiwa mke wa pili wa Gileadi, kama tu Rahabu alivyokuwa kahaba wakati fulani lakini baadaye akaolewa na Salmoni. (Amu 11:1; Yos 2:1; Mt 1:5) Kinachothibitisha Yeftha hakuwa mwanaharamu ni kwamba ndugu nusu wake waliozaliwa na mke wa kwanza wa Gileadi walimfukuza ili asipate urithi. (Amu 11:2) Kwa kuongezea, baadaye Yeftha alikubaliwa kuwa kiongozi wa watu wa Gileadi (ambao inaonekana waliongozwa na ndugu nusu wake walipokuwa wakimchagua). (Amu 11:11) Isitoshe, alimtolea Mungu dhabihu kwenye hema la ibada. (Amu 11:30, 31) Hangeweza kufanya yoyote kati ya mambo hayo ikiwa angekuwa mwanaharamu kwa sababu sheria ilisema hivi waziwazi: “Hakuna mwanaharamu anayepaswa kuingia katika kutaniko la Yehova. Hata kufikia kizazi cha kumi, hakuna mzao wake yeyote anayepaswa kuja katika kutaniko la Yehova.”​—Kum 23:2.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki