Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • rr uku. 212
  • Kuigawa Nchi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuigawa Nchi
  • Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mahali na mgawo wenye thamani
  • Urithi ulio sawa
  • ‘Mtaigawa Nchi Iwe Urithi’
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
  • ‘Weka Moyoni Mwako’ Hekalu la Mungu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • “Jina la Jiji Hilo . . . Litakuwa, Yehova Yupo Hapo”
    Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
  • Lile “Hekalu” na Yule “Mkuu” Leo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Hatimaye Ibada Safi ya Yehova Yarudishwa!
rr uku. 212
Mwanamume anayeonekana kama shaba akimwonyesha Ezekieli urithi wa nchi.

SANDUKU LA KUFUNDISHIA LA 20A

Kuigawa Nchi

Ufafanuzi kuhusu vipimo hususa vya mipaka uliwahakikishia kabisa wahamishwa kwamba nchi yao waliyoipenda ingerudishwa. Tunapata masomo gani leo kutokana na maono hayo? Fikiria mambo mawili kuhusu maono hayo:

Ramani inayoonyesha sehemu ambazo wahamishwa waliorudi waligawiwa, kama Ezekieli alivyonakili. Urithi kulingana na makabila umepangwa kutoka kaskazini kwenye kusini kuanzia Dani, Asheri, Naftali, Manase, Efraimu, Rubeni, Yuda, Mchango (eneo la usimamizi), Benjamini, Simeoni, Isakari, Zabuloni, na Gadi.

Mahali na mgawo wenye thamani

Kila mtu kati ya watu waliorudi kutoka uhamishoni angekuwa na urithi katika Nchi ya Ahadi iliyorudishwa. Vivyo hivyo, leo paradiso ya kiroho ina nafasi kwa ajili ya watumishi wote wa Yehova. Hata iwe tunatimiza jukumu dogo kadiri gani katika tengenezo, tuna mahali na mgawo wenye thamani katika nchi ya kiroho. Yehova anawaona watumishi wake wote kuwa wenye thamani.

Urithi ulio sawa

Katika maono ya Ezekieli, wakaaji wa maeneo yote ya Nchi ya Ahadi iliyorudishwa wangepata mazao mengi ya nchi kwa usawa. Vivyo hivyo, leo Yehova amewapa watumishi wake wote nafasi sawa za kupata baraka katika paradiso ya kiroho.

Angalia sura ya 20, fungu la 5-11

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki