Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr22 Julai kur. 1-4
  • Marejeo ya “Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya “Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha”
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2022
  • Vichwa vidogo
  • JULAI 11-17
  • JULAI 25-31
  • AGOSTI 1-7
  • AGOSTI 15-21
  • AGOSTI 22-28
  • AGOSTI 29–SEPTEMBA 4
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2022
mwbr22 Julai kur. 1-4

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

JULAI 11-17

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 20-21

“Yehova Ni Mungu wa Haki”

it-1 932 ¶1

Gibeoni

Kwa karne nyingi, jamii ya Wagibeoni iliendelea kuwepo, ingawa Mfalme Sauli alipanga njama ya kuwaangamiza. Hata hivyo, kwa subira, Wagibeoni waliendelea kumngojea Yehova afunue ukosefu huo wa haki. Yehova alifanya hivyo wakati wa utawala wa Daudi kwa kuleta njaa ya miaka mitatu. Daudi alipomuuliza Yehova kuhusu jambo hilo, alitambua kwamba hatia ya damu ilihusika. Kwa hiyo, akawauliza Wagibeoni jambo ambalo wangependa lifanywe ili kuondoa hatia ya damu. Wagibeoni walimjibu kwa usahihi kwamba hilo halikuwa “suala la fedha wala dhahabu,” kwa sababu kulingana na Sheria, fidia haikupaswa kuchukuliwa kwa ajili ya muuaji. (Hes 35:30, 31) Pia, Wagibeoni walitambua kwamba hawangeweza kumuua mtu yeyote bila kuruhusiwa kisheria. Hivyo, ni baada tu ya Daudi kuwauliza ndipo walipoomba wakabidhiwe “wana” saba wa Sauli. Kwa hatia ya damu kuwekwa juu ya Sauli na pia juu nyumba yake kunadokeza kwamba ingawa huenda Sauli ndiye aliyeongoza katika mauaji hayo, inawezekana kwamba “wana” wa Sauli pia walishiriki moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja. (2Sa 21:1-9) Ikiwa ndivyo ilivyokuwa, basi wana hao hawakuuawa kwa sababu ya dhambi ya baba yao, (Kum 24:16) bali haki ilitekelezwa kupatana na Sheria iliyosema “uhai utatolewa kwa uhai.”​—Kum 19:21.

JULAI 25-31

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 2 SAMWELI 23-24

“Je, Unachotoa Ni Dhabihu?”

it-1 146

Arauna

Inaelekea Arauna alimpa Daudi uwanja, pamoja na ng’ombe, na vifaa vya mbao ambavyo vingetumiwa kama kuni kwa ajili ya dhabihu, bila malipo. Lakini Daudi alisisitiza kwamba lazima avigharimie. Andiko la 2 Samweli 24:24 linaonyesha kwamba Daudi alinunua uwanja huo wa kupuria na ng’ombe hao kwa shekeli 50 za fedha (dola 110 za Marekani). Hata hivyo, 1 Mambo ya Nyakati 21:25 inasema kwamba Daudi alilipa shekeli 600 za dhahabu (karibu dola 77,000 za Marekani) kwa ajili ya uwanja huo. Mwandikaji wa Kitabu cha Pili cha Samweli anazungumzia tu kuhusu ununuzi wa eneo ambalo madhabahu ilijengwa pamoja na vifaa vya kutoa dhabihu, na inaonekana kwamba bei aliyotaja ilikuwa ya vitu hivyo peke yake. Kwa upande mwingine, mwandikaji wa Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati anazungumzia mambo yanayohusiana na hekalu ambalo lilijengwa baadaye katika eneo hilo, na hivyo anahusianisha ununuzi wa eneo hilo na ujenzi wa hekalu. (1Nya 22:1-6; 2Nya 3:1) Kwa kuwa eneo lote la hekalu lilikuwa kubwa sana, inaonekana kwamba shekeli 600 za dhahabu zilitumiwa kununua eneo hilo kubwa na si eneo lile dogo lililohitajika kwa ajili ya madhabahu ya kwanza iliyojengwa na Daudi.

AGOSTI 1-7

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 1 WAFALME 1-2

“Je, Unajifunza Kutokana na Makosa Yako?”

it-2 987 ¶4

Sulemani

Adoniya na wote waliokuwa wakimuunga mkono walikimbia wakiwa wamechanganyikiwa waliposikia sauti ya muziki na ya watu wakipaza sauti wakisema: “Mfalme Sulemani na aishi muda mrefu!” ikitokea Gihoni, eneo ambalo halikuwa mbali sana. Sulemani alipowekwa rasmi kuwa mfalme alikataa kuchafua pindi hiyo kwa kulipiza kisasi na hivyo kuonyesha kwamba utawala wake ungekuwa wenye amani. Hata hivyo, ikiwa hali zingekuwa kinyume na Adoniya ndiye angewekwa rasmi kuwa mfalme, inaelekea sana kwamba Sulemani angeuawa. Adoniya alikimbilia kwenye madhabahu akitafuta ulinzi, kwa hiyo Sulemani akaagiza kwamba Adoniya aletwe mbele yake. Sulemani alimjulisha kwamba angeendelea kuishi ikiwa atatenda kwa njia inayofaa, kisha akamruhusu aende nyumbani kwake.​—1Fa 1:41-53.

it-1 49

Adoniya

Hata hivyo, Daudi alipokufa, Adoniya alienda kwa Bath-sheba na kumshawishi amwakilishe mbele za Mfalme Sulemani na kumwomba ampe Abishagi, aliyekuwa muuguzi na mwandamani wa Daudi, awe mke wake. Adoniya aliposema “ufalme ulipaswa kuwa wangu, na Waisraeli wote walitarajia niwe mfalme” alionyesha kwamba alihisi amepokonywa haki yake hata ingawa alionekana ni kama amekubali kwamba Mungu ndiye aliyempa ndugu yake ufalme. (1Fa 2:13-21) Ingawa Adoniya aliomba hilo kwa sababu alitaka kulipwa kwa kupoteza ufalme, ombi lake linaonyesha kwamba bado alikuwa na tamaa ya kujitakia makuu kwa sababu kwa kawaida katika Mashariki ya kale, wake na masuria wa mfalme walipaswa kumilikiwa tu na mrithi wake. (Linganisha 2Sa 3:7; 16:21.) Hivyo ndivyo Sulemani alivyoliona ombi hilo lililofanywa kupitia mama yake, na hivyo akaagiza Adoniya auawe. Benaya alitekeleza amri hiyo mara moja.​—1Fa 2:22-25.

AGOSTI 15-21

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 1 WAFALME 5-6

“Walijenga kwa Mikono na Mioyo Yao Pia”

it-1 424

Mierezi

Kwa kuwa mierezi ilitumiwa sana, maelfu ya wafanyakazi walihitajika kukata miti na kuisafirisha hadi Tiro au Sidoni kwenye pwani ya bahari ya Mediterania. Walifunga magogo katika mafungu na kuyaacha yaelee baharini, huenda hadi Yopa. Kisha yalibebwa hadi Yerusalemu. Kazi hiyo ilifanywa kwa mkataba kati ya Sulemani na Hiramu. (1Fa 5:6-18; 2Nya 2:3-10) Mbao hizo ziliendelea kupelekwa Yerusalemu hata baada ya kipindi hicho, hivi kwamba ingeweza kusemwa kwamba wakati wa utawala wake, Sulemani alifanya “mbao za mierezi ziwe nyingi kama mikuyu.”​—1Fa 10:27; linganisha Isa 9:9, 10.

it-2 1077 ¶1

Hekalu

Sulemani alipokuwa akipanga kazi, aliwaandikisha wanaume 30,000 kutoka Israeli, akiwapeleka wanaume 10,000 Lebanoni kila mwezi kwa zamu. Wanaume hao walikaa miezi miwili nyumbani kabla ya zamu yao kufika. (1Fa 5:13, 14) Aliwaandikisha vibarua 70,000 kutoka miongoni mwa “wakaaji wageni” katika nchi, na wanaume 80,000 kuwa wakataji wa mawe. (1Fa 5:15; 9:20, 21; 2Nya 2:2) Sulemani aliwaweka wanaume 550 kuwa wasimamizi wa kazi na wengine 3,300 ambao inaonekana walikuwa wasaidizi wao. (1Fa 5:16; 9:22, 23) Inaelekea kwamba wanaume 250 kati yao walikuwa Waisraeli na wanaume 3,600 walikuwa “wakaaji wageni” katika Israeli.​—2Nya 2:17, 18.

AGOSTI 22-28

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | 1 WAFALME 7

“Mambo Tunayojifunza Kutokana na Nguzo Mbili”

it-1 348

Boazi, wa Pili

Nguzo ya shaba iliyosimamishwa kaskazini mwa ukumbi wa hekalu la Sulemani lenye utukufu, iliitwa Boazi, jina ambalo huenda lilimaanisha “Katika Nguvu.” Nguzo ya kusini iliitwa Yakini, jina ambalo huenda lilimaanisha “Naye [yaani, Yehova] Aimarishe Kabisa.” Kwa hiyo, maneno hayo yakiunganishwa na kusomwa kuanzia kushoto hadi kulia, mtu akiwa amesimama kuelekea upande wa mashariki angeweza kupata maana hii, ‘Naye [yaani, Yehova] aimarishe kabisa [hekalu] katika nguvu.’​—1Fa 7:15-21; ona KIFUNIKO.

Hazina za Kiroho

it-1 263

Kuoga

Usafi wa kimwili ni takwa ili kumwabudu Yehova kwa utakatifu na usafi. Hilo lilionekana kuhusiana na hema la ibada na baadaye kwenye utumishi wa hekalu. Kuhani Mkuu Haruni na wana wake walipowekwa rasmi, walioga kabla ya kuvaa mavazi yao rasmi. (Kut 29:4-9; 40:12-15; Law 8:6, 7) Ili kuosha mikono na miguu, makuhani walitumia maji yaliyokuwa kwenye beseni la shaba lililokuwa kwenye ua wa hema la ibada, na baadaye, kwenye hekalu la Sulemani, walitumia maji yaliyokuwa kwenye tangi kubwa lililoitwa Bahari. (Kut 30:18-21; 40:30-32; 2Nya 4:2-6) Siku ya Kufunika Dhambi kuhani mkuu alioga mara mbili. (Law 16:4, 23, 24) Wale waliopeleka mbuzi wa Azazeli, masalio ya dhabihu za wanyama, na ng’ombe mwekundu wa dhabihu nje ya kambi walipaswa kuoga na kufua nguo zao kabla ya kurudi kambini.​—Law 16:26-28; Hes 19:2-10.

AGOSTI 29–SEPTEMBA 4

Hazina za Kiroho

it-1 1060 ¶4

Mbingu

Sulemani, aliyejenga hekalu la Yerusalemu, alisema kwamba “mbingu, naam, mbingu za mbingu,” haziwezi kumtosha Mungu. (1Fa 8:27) Yehova akiwa Muumba wa mbingu, yuko juu ya mbingu zote na “jina lake peke yake liko juu sana lisiweze kufikiwa. Ukuu wake uko juu ya dunia na mbingu.” (Zb 148:13) Yehova huzipima mbingu halisi kwa urahisi kama vile tu mtu hupima kitu kwa kutumia kiganja chake, hivi kwamba kitu hicho kinakuwa kati ya kidole gumba na kidole kidogo. (Isa 40:12) Maneno ya Sulemani hayamaanishi kwamba Yehova hana makao hususa. Wala hayamaanishi kwamba yuko kila mahali na katika kila kitu. Tunaweza kuthibitisha hilo kutokana na maneno ya Sulemani alipomwomba Yehova asikilize “kutoka mbinguni, makao yako,” yaani, mbingu ambako viumbe wa roho wanaishi.​—1Fa 8:30, 39.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki