WIMBO NA. 65
Songa Mbele!
Makala Iliyochapishwa
	- 1. Songa mbele, fikia ukomavu! - Angaza kote nuru ya habari njema. - Boresha ustadi wako shambani, - Mtegemee Mungu. - Sote twaweza kuhubiri. - Yesu aliweka mfano. - Mwombe Mungu akupe nguvu zake, - Usimame imara. 
- 2. Songa mbele, uwe na ujasiri! - Tangazia watu wote habari njema. - Tumsifu Yehova kwa furaha, - Tuhubiripo kote. - Adui wajapotutisha. - Usihofu; tangaza kote, - Kwamba Ufalme watawala sasa. - Hubiri kwa bidii. 
- 3. Songa mbele, wasaidie wapya, - Uwe na ustadi, - kazi ni nyingi sana. - Roho ya Mungu na ikuchochee. - Nawe upate shangwe. - Upendezwe na watu wote. - Usikose kuwarudia. - Uwasaidie wasonge mbele. - Ukweli uangaze. 
(Ona pia Flp. 1:27; 3:16; Ebr. 10:39.)