Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr23 Septemba kur. 1-3
  • Marejeo ya “Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya “Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha”
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2023
  • Vichwa vidogo
  • SEPTEMBA 11-17
  • OKTOBA 9-15
  • OKTOBA 30–NOVEMBA 5
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2023
mwbr23 Septemba kur. 1-3

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

© 2023 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania

SEPTEMBA 11-17

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | ESTA 3-5

“Wasaidie Wengine Wafikie Uwezo Wao Kamili”

it-2 431 ¶7

Mordekai

Akataa Kumwinamia Hamani. Baada ya mambo hayo, Ahasuero alimweka Hamani Mwagagi kuwa waziri mkuu, naye aliagiza watu wote waliokuwa katika lango la mfalme wamsujudie Hamani kwa sababu alikuwa amepandishwa cheo. Mordekai alisema kwamba yeye ni Myahudi na kwa sababu hiyo alikataa katakata kumsujudia. (Est 3:​1-4) Inaonekana sababu hiyo ambayo Mordekai alitaja ilihusu uhusiano wake pamoja na Mungu wake, Yehova, kwa kuwa Mordekai alikuwa sehemu ya taifa la Kiyahudi ambalo lilikuwa wakfu kwa Yehova. Alitambua kwamba kumsujudia Hamani kulihusisha mengi zaidi ya kumwinamia mtawala kama Waisraeli wengi walivyokuwa wamefanya katika nyakati zilizopita ili tu kuonyesha kwamba walitambua cheo cha juu cha mtawala huyo. (2Sa 14:4; 18:28; 1Fa 1:16) Katika kisa cha Hamani kulikuwa na sababu nzuri kwa nini Mordekai hakumwinamia. Inaelekea Hamani alikuwa Mwamaleki, na Mordekai alijua kwamba Yehova alikuwa amesema atapigana vita na Waamaleki “kizazi baada ya kizazi.” (Kut 17:16; ona HAMANI.) Mordekai aliona hilo kuwa suala la utimilifu kwa Mungu na si suala la kisiasa.

it-2 431 ¶9

Mordekai

Alitumiwa Kuokoa Waisraeli. Agizo la kuwaangamiza Wayahudi wote katika milki ilipotolewa, kwa imani Mordekai alimwambia Esta kwamba alikuwa amewekwa kuwa malkia kwa kusudi la kuwaokoa Wayahudi. Mordekai alimweleza Esta kwamba ana jukumu zito na akamwambia aende kumwomba mfalme kibali na msaada. Ingawa kufanya hivyo kungehatarisha maisha yake, Esta alitii.—Est 4:7–5:2.

SEPTEMBA 25–OKTOBA 1

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | ESTA 9-10

“Alitumia Mamlaka Yake Bila Ubinafsi”

it-2 432 ¶2

Mordekai

Mordekai alichukua nafasi ya Hamani ya kuwa waziri mkuu na mfalme akampa pete yake ya muhuri iliyotumiwa kuidhinisha hati za serikali. Mfalme alikuwa amempa Esta nyumba ya Hamani, naye Esta akamweka Mordekai kuwa msimamizi wa nyumba hiyo. Vilevile, Mordekai alitumia mamlaka ambayo alipewa na mfalme kutoa agizo lingine lililowapa Wayahudi haki ya kisheria ya kujilinda. Agizo hilo liliwaletea Wayahudi shangwe na kuwahakikishia kwamba wataokoka. Wengi katika milki ya Uajemi walijiunga na Wayahudi, na Adari 13, yaani, siku ambayo maagizo hayo yangetekelezwa, Wayahudi walikuwa tayari. Kwa sababu ya cheo cha juu cha Mordekai, maofisa wa serikali pia waliwaunga mkono Wayahudi. Katika Shushani, Wayahudi waliruhusiwa kupigana kwa siku nyingine moja. Kote katika milki ya Uajemi zaidi ya maadui 75,000 wa Wayahudi waliangamizwa, kutia ndani wana kumi wa Hamani. (Est 8:1–9:18) Huku akishirikiana na Esta, Mordekai aliagiza siku ya 14 na ya 15 ya mwezi wa Adari, yaani, “siku za Purimu” ziadhimishwe kila mwaka kwa karamu na kushangilia na kupeana zawadi bila kusahau kuwapa maskini zawadi pia. Wayahudi walikubali kufanya hivyo na wakaamua kwamba wazao wao na watu wote waliojiunga nao wataendelea kuadhimisha siku hizo. Mordekai alikuwa wa pili kutoka kwa mfalme na kwa sababu hiyo aliheshimiwa na Wayahudi waliompenda Mungu, na aliendelea kutetea masilahi yao.—Est 9:​19-22, 27-32; 10:​2, 3.

it-2 716 ¶5

Purimu

Kusudi. Wasomi fulani husema kwamba leo, Sherehe ya Purimu inayoadhimishwa na Wayahudi imepunguza maana yake ya kidini, na mara nyingine watu wanapita kiasi, lakini hali haikuwa hivyo sherehe hiyo ilipoanzishwa. Mordekai na Esta walikuwa watumishi wa Mungu wa kweli, Yehova, na walianzisha sherehe hiyo ili kumtukuza Yeye. Tunaweza kusema kwamba Yehova ndiye aliyewaokoa Wayahudi wakati huo kwa sababu suala hilo lilizuka kutokana na utimilifu wa Mordekai na jinsi alivyokuwa ameazimia kumwabudu Yehova pekee. Inaelekea Hamani alikuwa Mwamaleki, na Yehova alikuwa amelaani Waamaleki na kuapa kwamba atawaangamiza. (Est 3:​2, 5; Kut 17:​14-16) Isitoshe, maneno ambayo Mordekai alimwambia Esta (Est 4:14) yalionyesha kwamba alitumaini Wayahudi watakombolewa na Mungu, Esta naye alifunga kabla ya kuwasilisha ombi lake mbele ya mfalme na kumwalika kwenye karamu, na hilo lilionyesha kwamba alitegemea msaada kutoka kwa Mungu.—Est 4:16.

OKTOBA 9-15

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | AYUBU 4-5

“Jilinde Dhidi ya Habari za Uwongo”

it-1 713 ¶11

Elifazi

2. Mmoja kati ya marafiki watatu wa Ayubu. (Ayu 2:11) Alikuwa Mtemani na hivyo huenda alikuwa mzao wa Elifazi aliyetajwa kwenye Na. 1 hapo juu, hilo linamaanisha alikuwa mzao wa Abrahamu na pia alikuwa mtu wa ukoo wa Ayubu. Yeye na wazao wake walijivunia hekima yao. (Yer 49:7) Kati ya “wafariji” hao watatu inaonekana Elifazi ndiye aliyekuwa mwenye kuheshimika zaidi na mwenye uvutano zaidi na huenda pia aliwazidi umri wenzake. Yeye ndiye aliyetangulia kuzungumza na maongezi yake yalikuwa marefu zaidi.

OKTOBA 30–NOVEMBA 5

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | AYUBU 11-12

“Njia Tatu za Kupata Hekima na Kunufaika Nayo”

it-2 1190 ¶2

Hekima

Hekima ya Kimungu. Hekima iliyo kamili ni ya Yehova Mungu tu, kwa njia hiyo yeye “peke yake ndiye mwenye hekima.” (Ro 16:27; Ufu 7: 12) Ujuzi unatokana na kuelewa mambo ya msingi, na kwa kuwa Yehova ndiye Muumba, yeye amekuwepo “tangu milele hadi milele” (Zb 90:​1, 2), na anajua kila kitu kuhusu ulimwengu, jinsi ambavyo umefanyizwa na pia vitu vyote vilivyomo, na hata historia ya ulimwengu kufikia sasa. Yehova ndiye aliyeweka sheria za asili, mizunguko mbalimbali, na viwango ambavyo wanadamu wanategemea wanapofanya utafiti na kubuni vitu, na iwapo vyote hivyo havingekuwepo wanadamu hawangeweza kufanya chochote na hawangefanya maendeleo yoyote. (Ayu 38:​34-38; Zb 104:24; Met 3:19; Yer 10:​12, 13) Haishangazi kwamba, wanadamu wanapokosa kufuata viwango vyake vya maadili, maisha yao yanakuwa yenye misukosuko na wanashindwa kufanya maamuzi mazuri na kwa ujumla wanakosa furaha. (Kum 32:​4-6; ona YEHOVA [Mungu mwenye viwango vya maadili].) Yehova anaelewa kila kitu. (Isa 40:​13, 14) Ingawa anaweza kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na viwango vyake vya uadilifu yatukie au hata kusitawi kwa muda, hatimaye yeye ndiye anayeamua jinsi mambo yatakavyokuwa wakati ujao na hakika yatafanyika kulingana na mapenzi yake, na kila jambo ambalo amesema “hakika litafanikiwa.”—Isa 55:​8-11; 46:​9-11.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki