SOMO LA 5
Kusoma kwa Usahihi
1 Timotheo 4:13
MUHTASARI: Soma kwa sauti kile hasa kilichoandikwa kwenye ukurasa.
JINSI YA KUFANYA HIVYO:
- Tayarisha vizuri. Elewa kusudi la kuandikwa kwa simulizi hilo. Jizoeze kusoma mafungu ya maneno, si neno mojamoja. Epuka kuongeza, kurukaruka, au kubadilisha maneno. Zingatia alama za vituo. 
- Tamka kila neno kwa usahihi. Ikiwa hujui jinsi neno linavyotamkwa, liangalie katika kamusi, sikiliza rekodi ya chapisho lililosomwa, au uombe msaada kutoka kwa msomaji mzuri. 
- Zungumza waziwazi. Tamka maneno waziwazi, inua kichwa chako na ufumbue kabisa kinywa unapoongea. Jitahidi kutamka kila silabi.