Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hasira Yasababisha Mauaji
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
    • Kaini anakasirika Abeli anapomtolea Yehova dhabihu

      SOMO LA 4

      Hasira Yasababisha Mauaji

      Baada ya Adamu na Hawa kufukuzwa katika bustani ya Edeni, walizaa watoto wengi. Mtoto wa kwanza aliitwa Kaini, naye alikuwa mkulima, na mtoto wa pili, Abeli, alikuwa mchungaji wa wanyama.

      Siku moja Kaini na Abeli walimtolea Yehova dhabihu. Je, unajua dhabihu ni nini? Ni zawadi ya pekee. Yehova alifurahishwa na dhabihu ya Abeli, lakini alichukizwa na dhabihu ya Kaini. Jambo hilo lilimkasirisha sana Kaini. Yehova alimwonya Kaini kwamba hasira ingeweza kusababisha afanye jambo baya. Hata hivyo, Kaini hakusikiliza.

      Badala yake Kaini alimwambia Abeli hivi: ‘Twende shambani.’ Walipokuwa peke yao shambani, Kaini alimshambulia ndugu yake na kumuua. Yehova angefanya nini kuhusu jambo hilo? Yehova alimwadhibu Kaini kwa kumfukuza aende mbali na familia yao. Kaini hakuruhusiwa kurudi tena nyumbani.

      Kaini anamkaribia Abeli wakiwa shambani

      Tunajifunza nini? Tunajifunza kwamba tunaweza kukasirika mambo yanapoenda kinyume na matarajio yetu. Tunapoona kwamba tumeanza kukasirika—au tunapoonywa na wengine kuhusu hasira—tunapaswa kukubali kurekebishwa na kujitahidi kudhibiti hisia hizo kabla hazijaanza kututawala.

      Kwa sababu Abeli alimpenda Yehova na alifanya mambo mema, sikuzote Yehova atamkumbuka. Mungu atamfufua Abeli wakati atakapoifanya dunia kuwa paradiso.

      “Kwanza fanya amani na ndugu yako, kisha urudi na kutoa zawadi yako.”​—Mathayo 5:24

      Maswali: Watoto wawili wa kwanza wa Adamu na Hawa walikuwa nani? Kwa nini Kaini alimuua ndugu yake?

      Mwanzo 4:1-12; Waebrania 11:4; 1 Yohana 3:11, 12

  • Safina ya Noa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
    • Noa na familia yake wakijenga safina

      SOMO LA 5

      Safina ya Noa

      Watu walizidi kuongezeka duniani na wengi walikuwa wakifanya mambo mabaya. Hata baadhi ya malaika wa mbinguni wakawa wabaya. Waliacha makao yao huko mbinguni na kuja duniani. Je, unajua ni kwa nini walifanya hivyo? Ili wavae miili ya wanadamu na kujichukulia wanawake.

      Malaika walijichukulia wanawake na kuzaa watoto. Watoto hao walikuwa watu wenye nguvu sana na wajeuri. Waliwapiga watu. Yehova hangeruhusu hali hiyo iendelee. Hivyo, aliamua kuwaharibu watu wabaya kupitia gharika.

      Noa na familia yake wakijenga safina na kuandaa chakula

      Lakini kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa tofauti na watu hao. Alimpenda Yehova. Jina lake ni Noa. Alikuwa na mke na watoto watatu, yaani, Shemu, Hamu, na Yafethi, na kila mtoto alikuwa na mke. Yehova alimwambia Noa wajenge safina, ili yeye na familia yake waokoke Gharika. Safina ilikuwa sanduku kubwa lililoelea majini. Pia, Yehova alimwambia Noa awaingize wanyama ndani ya safina ili wao pia waokoke.

      Mara moja, Noa alianza kujenga safina. Noa na familia yake walijenga safina kwa karibu miaka 50. Walijenga safina kulingana na maagizo ya Yehova. Katika kipindi hicho, Noa aliwaonya watu kuhusu Gharika. Lakini hakuna mtu aliyemsikiliza.

      Hatimaye, muda wa kuingia ndani ya safina ukafika. Acha tuone kile kilichotokea baadaye.

      “Kama siku za Noa zilivyokuwa, ndivyo kuwapo kwa Mwana wa binadamu kutakavyokuwa.”​—Mathayo 24:37

      Maswali: Kwa nini Yehova alileta Gharika? Yehova alimpa Noa maagizo gani?

      Mwanzo 6:1-22; Mathayo 24:37-41; 2 Petro 2:5; Yuda 6

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki