WIMBO NA. 39
Jifanyie Jina Zuri Mbele za Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Tunatamani kupendeza Mungu.
Tuwe na jina zuri mbele zake.
Tukifanya mambo yampendezayo,
Twafurahisha moyo wake.
2. Ulimwenguni watu hutafuta,
Kujifanyia jina mashuhuri.
Tukifuatia ulimwengu huu,
Kibali cha Yah, tutakosa.
3. Twataka jina, libaki katika
Kumbukumbu ya Yehova milele.
Basi sikuzote tumtii Mungu,
Na tudumishe jina zuri.
(Ona pia Mwa. 11:4; Met. 22:1; Mal. 3:16; Ufu. 20:15.)