Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g03 12/22 uku. 32
  • Uhai wa Yesu Unathaminiwa Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uhai wa Yesu Unathaminiwa Sana
  • Amkeni!—2003
Amkeni!—2003
g03 12/22 uku. 32

Uhai wa Yesu Unathaminiwa Sana

Yapata miaka 2,000 iliyopita, Mungu aliwapa wanadamu zawadi kubwa zaidi, yaani, uhai wa Mwana wake Yesu Kristo, unaotuwezesha kuishi milele. (Yohana 3:16) Kwa sababu ya kuthamini zawadi hiyo, wengi wamewapa marafiki na watu wa ukoo kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi, kinachoelezea uhai wa Yesu kulingana na zile Injili nne.

Hivi majuzi mwanamume mmoja alisema kwamba yeye huwapatia kitabu hicho watu ambao humtumia kadi za Krismasi. Yeye huwaandikia na kuwaelezea kifupi kwa nini aliacha kusherehekea Krismasi, na hutumia habari kutoka kwenye ensaiklopidia, kamusi, na Biblia. Kisha yeye hutia ndani kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi.

Mtu huyo alisema kwamba maprofesa wawili wa chuo kikuu walimwandikia barua zenye kutia moyo sana. Barua moja inasema: “Nilipokea zawadi yako yenye kuvutia ya kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Tunakifurahia sana. Kina mambo mengi mazuri. Tayari tumekitumia sana.”

Kitabu hiki kinazungumzia mahubiri, mifano, na miujiza ya Yesu. Kadiri ilivyowezekana, jitihada ilifanywa kuyapanga matukio yote katika utaratibu ambao yalitukia. Isitoshe kina picha nzuri zilizofanyiwa utafiti ili kuonyesha hisia za Yesu na watu wa siku zake.

Ikiwa unataka kitabu hicho cha kurasa 448, jaza sehemu iliyo hapa chini na uitume ukitumia anwani iliyoonyeshwa au anwani ifaayo kati ya zile zilizoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Ningependa kupokea kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi bila malipo.

□ Ningependa kujifunza Biblia nyumbani kwangu bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki