Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 3/8 uku. 32
  • “Ina Kweli Nyingi Muhimu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Ina Kweli Nyingi Muhimu”
  • Amkeni!—2004
Amkeni!—2004
g04 3/8 uku. 32

“Ina Kweli Nyingi Muhimu”

Ndivyo alivyosema mkurugenzi wa hospitali ya wagonjwa mahututi huko Illinois, Marekani, kuhusu broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa. Shahidi mmoja wa Yehova aliposoma Amkeni!, aliona kwamba wazee wengi sana walijiua, hivyo akamtumia mkurugenzi huyo broshua hiyo na gazeti la Amkeni!. Mkurugenzi huyo alipovipokea, aliandika barua mara moja.

Mkurugenzi huyo alipotambua kwamba broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa ina kweli nyingi muhimu, aliandika hivi: “Ningefurahi ikiwa . . . familia zingepata broshua hii ili zifarijiwe na hekima, maandiko, na mazungumzo ya Biblia yaliyomo.”

Bila kukawia, Shahidi huyo alimpigia simu mkurugenzi huyo na kupanga kumtembelea. Mkurugenzi huyo aliomba broshua 20 na kusema kwamba angependa hospitali yake ipelekewe broshua zaidi baada ya kila miezi miwili au mitatu.

Huenda wewe au mtu unayemjua akafarijiwa pia kwa kusoma broshua hiyo ya kurasa 32. Unaweza kuiomba kwa kujaza sehemu iliyo hapa chini na uitume ukitumia anwani iliyoonyeshwa au anwani ifaayo kati ya zile zilizoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Ningependa kupokea broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa bila malipo. Andika lugha unayotaka.

□ Ningependa kujifunza Biblia nyumbani kwangu bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki